SERIKALI YATOA BILIONI 2.5 KWA AJILI YA UJENZI WA JENGO LA MAMA NA MTOTO HOSPITALI YA RUFAA SHINYANGA.

NA WAMJW-SHINYANGA Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa kiasi cha shilingi bilioni 2.5 zitakazotumika katika ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, lengo likiwa ni kutoa huduma za kibingwa kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga. Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu wakati alipotembelea ujenzi wa hospitali hiyo na kukuta jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na utawala likiwa limekamilika. Waziri Ummy amesema fedha hizo…

Soma Zaidi >>

WATUMISHI WATAKAOCHEZEA FEDHA ZA SERIKALI KUTUMBULIWA.

Na Heri Shaaban, Dar es salaam. Watumishi wa manispaa ya Ilala watakaotumia vibaya fedha za serikali watachukuliwa hatua za kisheria. Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa manispaa ya Ilala Jumanne Shauri wakati wa semina maalum ya force account kwa watumishi wa Ilala, maofisa watendaji kata, walimu wakuu wa msingi ,sekondari na TAKUKURU ambapo wawezeshaji wametoka mamlaka za zabuni za umma (PPAA). Alisema dhumuni la mafunzo hayo kuwajengea uwezo watendaji wa Halmashauri ya Ilala katika matumizi ya fedha za serikali pindi wanapopewa watumie Kwa dhumuni lililokusudiwa na wale watakaokwenda kinyume wachukulie hatua…

Soma Zaidi >>

WATU WATATU WAMEFARIKI KWA AJALI YA GARI KAGERA.

Na,Mwandishi wetu-Muleba Watu watatu wamefariki papo hapo hii leo kwa kugongwa na gari eneo la daraja nane kata ya Kimwani wilaya ya Muleba mkoani Kagera wakati wakisafiri kwa kutumia pikipiki wakitokea kijiji cha Kangaza kuelekea Kyamyorwa wilayani humo. Mkuu wa wilaya ya Muleba mhandisi Richard Riyango ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama amethibitisha kutokea kwa vifo vya watu hao na kwamba amepata taarifa kutoka jeshi la polisi wilayani Muleba leo mchana. Mwenyekiti wa kijiji cha Kizilamuyaga kata ya kimwani Adrian Philipo amewataja waliofariki kuwa ni Alisen Amon…

Soma Zaidi >>

SUBIRA MGALU:MALENGO YA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI UTUMIKE KAMA FURSA KIUCHUMI,KUBORESHA MAISHA NA HUDUMA ZA JAMII

Wizara ya nishati kupitia wakala wa umeme vijijini (REA) wamewasha umeme kwenye vijiji sita vilivyopo wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani ikiwa ni mradi wa ujazilizi wenye malengo ya kuwakwamua wananchi kiuchumi. Akizungumza kwenye ziara hiyo naibu waziri wa nishati Mhe Subira Mgalu amesema kuwa mradi huo wa ujazilizi ambao umeunganisha umeme kwenye vijiji sita wilayani Kisarawe ni utekelezaji wa serikali katika kuhakikisha wananchi wote wanapata nishati hiyo muhimu kwa ajili ya maisha yao na maendeleo kwa ujumla huku akisema kauli mbiu ya ‘zima kibatari’. “Tumewasha umeme kwenye vijiji hivi sita…

Soma Zaidi >>

BAADA YA BARUTI KUUA MMOJA MGODINI VIONGOZI WAZINDUKA

Siku moja baada ya mtu mmoja kufa na mwingine kujeruhiwa kwa kulipukiwa na baruti ndani ya Mgodi wa dhahabu wa Maguye wilaya ya Serengeti ,sasa ukaguzi kufanywa migodi yote. Tukio hilo linadaiwa kutokea januari 22 mwaka huu limethibitishwa na Mkuu wa wilaya hiyo Nurdin Babu na Mganga Mkuu wa Hospitali Teule ya Nyerere,na kumtaja aliyekufa kuwa ni Sifa Augustino (23)mkazi wa Ilemela Mwanza na majeruhi Limbu Sangija ambaye ameruhusiwa kutoka. . Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo jina limehifadhiwa alisema walikuwa wanatarajia kulipua mwamba kwa kutumia baruti ili iwawezeshe…

Soma Zaidi >>

WAKULIMA WA PARACHICHI NJOMBE WAJIPANGA NA MSIMU WA MAVUNO.

Na. mwandishi wetu-Njombe Viongozi wa mtandao wa wakulima wa zao la parachichi mkoa wa Njombe wamekutana na kufanya mazungumzo na wakulima wa zao hilo wanaounda kikundi cha Uamawi kilichopo katika mtaa wa Wikichi kata ya Ramadhani mjini Njombe. Akizungumza na wakulima hao waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano uliofanyika nje ya Ofisi ya mtaa wa Wikichi Mratibu wa mtandao wa wakulima wa Parachichi mkoa wa Njombe ndg. Erasto Ngole (Shikamoo parachichi) amesema kuwa lengo la kukutana pamoja na wakulima hao ni kuwahamasisha kujipanga na msimu mpya wa mavuno pamoja na kupanga…

Soma Zaidi >>

OLESENDEKA AAGIZA WATEKAJI WATOTO WASAKWE POPOTE NJOMBE

Na Amiri kilagalila Mkuu wa mkoa wa Njombe ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Christopher Olesendeka amesema vyombo vya ulinzi na usalama vitawasaka popote walipo watekaji wa watoto watatu wa familia moja wanaodaiwa kutekwa january 20 na kusababisha taharuki kwa wakazi wa mkoa huo. Wimbi la kutekwa kwa watoto wadogo limezidi kutanda mkoani Njombe tangu liibuke desemba mwaka jana ambapo hadi sasa inaelezwa zaidi ya watoto 10 wametekwa huku wachache wanaopatikana wanakutwa wakiwa wamefariki dunia. Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ikando kata ya Kichiwa wilaya…

Soma Zaidi >>

WATAHINIWA 57 WAFUTIWA MATOKEO SEKONDARI YA TUMAINI LUTHERAN SEMINARY

Baraza la mitihani  la Tanzania limefuta matokeo yote ya watahiniwa 57 wa shule ya sekondari tumaini Lutheran Seminary (SO983) iliyopo katika wilaya ya malivyi mkoani morogoro   kwa kufanya vitendo vya udangafu  katika mitihani. Hayo yamesemwa na  katibu wa baraza la mitihani la Tanzania Dkt Charles Msonde  Jijini Dodoma ,wakati akitangaza matokeo ya kidato cha nne yaliofanyika  tarehe 5  hadi tarehe 23 novemba, 2018, ambapo amesema kuwa uongozi wa shule kwa kushirikiana na walimu wa shule hiyo 6 , watahiniwa wa kidato cha nne , baadhi ya wanafunzi wa kidato cha…

Soma Zaidi >>

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE: NECTA YA WEKA WAZI SHULE 10 ZILIZOFANYA VIZURI ZAIDI

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), leo limetangaza matokeo ya kidato cha nne na kuorodhesha shule kumi za sekondari zilizofanya vizuri zaidi. Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dkt. Charles Msonde ameeleza kuwa shule binafsi ndizo zilizoongoza kwa kufanya vizuri zaidi katika matokeo hayo. Amezitaja shule kumi zilizopata ufaulu wa juu zaidi Francis Girls (Mbeya), Kemebos (Kagera), Marian Boys (Pwani), Marian Girls (Pwani), Ahmes (Pwani), Canossa (Dar es Salaam), Bright Future Girls (Dar es Salaam), Maua Seminary (Kilimanjaro), Precious Blood (Arusha) na Bethel Sabs Girls (Iringa). Aidha, Dkt. Msonde amemtaja Hope Mwaibanje…

Soma Zaidi >>

MWAKITINYA AWANYOOSHEA KIDOLE WAPINZANI AMFAGILIA JPM

NA DANSON KAIJAGE, DODOMA MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM (NEC) Mussa Mwakitinya maarufu kwa jina la Mwana wa Mungu amewashambulia wabunge wa upinzani na kueleza kuwa wana nia mbaya na amani ya taifa. Mwakitinya ambaye kwa mara ya kwanza amejitokeza hadharani na kuzungumza na vyombo vya habari amesema kuwa wanasiasa hao ni Mbunge wa Kigoma Mjini na Mwenyekiti wa Chama cha ACT -Wazalendo, Zitto Kabwe na mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu. Mnec huyo alisema kuwa wanasiasa hao wamekuwa wakifanya siasa za kulitia doa taifa kwa…

Soma Zaidi >>