MIEZI MITATU MICHUNGU KWA TAKUKURU NJOMBE SASA IMEKWISHA.

Na Amiri kilagalila Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru Mkoa wa Njombe imefanikiwa kufuatilia na kukagua miradi mikubwa mitano ya maendeleo ukiwemo mradi wa maji wa Lugenge wenye thamani ya Tshs 3,642,817 355 bilioni. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kaimu Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Njombe Charles Mulebya Alisema Kuwa Takukuru mkoa ndani ya kipindi cha miezi mitatu ya Octoba hadi Disemba 2018 waliweza kufuatilia na kukagua miradi mikubwa mitano ya maendeleo kwa lengo la kuhakiki ubora na thamani ya fedha za umma. Mulebya alisema licha…

Soma Zaidi >>

DKT SHEIN AWATAKA WAHITIMU WA CHUO KUTUMIA UJUZI WAO KUJIAJIRI

RAIS wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe.Dk Ali Mohamed Shein amewataka wahitimu wa Chuo cha Abdul Rahman Al Sumait kutumia ujuzi walioupata chuoni hapo kwa kujiajiri wenyewe bila ya kusubiri ajira kutoka Serikalini. Akisoma hotuba kwa niaba yake huko Chukwani, katika mahafali ya 18 ya chuo hicho, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Riziki Pembe Juma amesema tatizo la upungufu wa ajira si la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pekee bali ni kilio cha dunia nzima. Aidha Dk. Shein ameupongeza uongozi wa chuo cha Alsumait…

Soma Zaidi >>

MBUNGE ZANZIBAR AMKINGIA KIFUA NDUGAI

NA DANSON KAIJAGE,DODOMA MBUNGE wa Viti Maalum kutoka Zanzibar Tahuida Nyimbo (CCM) amesema kuwa siku zote maamuzi ya Spika Job Ndugai hayajawahi kuwa ya kukurupuka. Nyimbo alisema kutokana na hilo ni jambo la aibu kuona baadhi ya wanasiasa kumkebei na kumdhalilisha huku wakiwa wanatamani kukwanisha utendaji wake wa kazi. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya sakata la Spika Ndugai kutoa agizo la CAG kufika mbele ya kamati ya Bunge ili kuhojiwa kwa madai ya kutoa kauli ya kulidhalilisha Bunge alipokuwa akihojiwa na kituo…

Soma Zaidi >>

VIONGOZI WA DINI WAPEWA SOMO.

Na,Danson Kaijage-Dodoma ASKOFU wa Jimbo la Dodoma kanisa la Mlima wa Moto,Silvanusi Komba amewataka viongozi wadini kuhakikisha wanawafundisha waumini wao juu ya kufanya kazi kwa bidii badala ya kufundisha masomo ya utoaji tu. Akihubiri katika ibada ya Jumapili askofu Komba alisema mwaka 2019 ni Mwaka pekee wa watanzania kutambua umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii badala ya kukaa vijiweni na kuilalamikia serikali. Kiongozi huyo wa Kiroho alisema kuwa apendezwi kuona waumini wa kanisani lake kuendelea kulalamika kwa madai kuwa maisha ni magumu. Akiwahutubia maelfu ya waumini kanisani hapo alisema kuwa…

Soma Zaidi >>

KIKUNDI CHA VYAMA VYA SIASA CHAJITOSA KUSAIDIA DAMU HOSPITAL YA NYERERE

Na,Naomi Milton Serengeti Kikundi cha ujamaa na ujirani mwema Serengeti (KICHAUMWESE) kinachoundwa na vyama vitano vya siasa kimejitokeza na kuchangia unit 18 za damu kusaidia wahitaji mbalimbali katika Hospitali Teule ya Nyerere ddh Hospital hiyo bado ina changamoto kubwa ya uhitaji wa damu hasa kwa makundi maalum kama vile mama wajawazito na watoto lakini pia kwa watu majeruhi ambao hupata ajali Katika mkutano wao mkuu uliofanyika wilayani Serengeti wanakikundi walikabidhi hati ya usajili kwa katibu Tawala wilaya Cosmas Qamara aliyemwakilisha Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu na kuahidi kuendeleza…

Soma Zaidi >>

TUNDU LISSU ADAI ANATAKA KUVULIWA UBUNGE…SPIKA NDUGAI AKIRI LISSU NI MTORO NA ANAZURULA NJE YA NCHI.

Na,Mwandishi Wetu. Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, (Chadema), amedai kuwa kuna mkakati wa kutaka kumvua Ubunge kwa madai kuwa ni mtoro bungeni. Akizungumzia kwa undani mkakati wa kutaka kumvua Ubunge, kupitia waraka wake alioutoa, Lissu amedai kuwa kuna hoja inajengwa kuwa Mbunge huyo ni mtoro kwani hajaonekana Bungeni na hajamwandikia barua Katibu wa Bunge taarifa yoyote ya maandishi kuhusu kuumwa kwake wala matibabu yake. Mbunge huyo ameeleza kuwa hana sababu yoyote ya kutilia shaka taarifa hizi kwani waliomtonya ni watu wenye dhamana kubwa Bungeni na Serikalini ambao amedai hawaridhishwi…

Soma Zaidi >>

SHULE ILIYOATHIRIWA NA BOMU KAGERA YAJENGEWA MIUNDOMBINU.

Na,Mwandishi wetu-Ngara Taasisi ya Tumain Fund mkoani Kagera imetoa msaada wa vyumba viwili vya madarasa , ofisi ya walimu na madawati 30 vyenye thamani ya Sh76 milioni kwa shule ya msingi Kihinga wilayani Ngara ailiyoathiriwa na bomu Novemba 2017 na kusababisha wanafunzi watano kufariki na wengine 43 kujeruhiwa. Mratibu wa taasisi hiyo Alex Nyamkara akiambatana na Mwenyekiti wa mfuko huo Dkt Suzan Wilson kutoka nchini Uingereza wamekabidhi miundombinu hiyo leo kwa shule hiyo baada ya tukio la bomu lililoharibu madarasa manne. Nyamkara amesema licha ya vyumba hivyo, wakati wa tukio…

Soma Zaidi >>