WAZIRI MKUU: BENKI YA KILIMO IHARAKISHE MALIPO YA KOROSHO HATUJAVUKA HATA NUSU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Benki ya Kilimo Tanzania (TADB) ihakikishe inabadilisha mfumo wake ili iweze kuharakisha malipo kwa wakulima wa korosho ambao wameshahakikiwa. Ametoa agizo hilo Jumatano, 16 Januari, 2019) wakati akizungumza na Wakuu wa Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TADB kwenye kikao alichokiendesha kwa njia ya video (video conferencing) kutokea ofisini kwake Mlimwa, Dodoma. Wakuu wa mikoa hiyo mitatu walikuwa kwenye mikoa yao na Mkurugenzi Mkuu wa TADB, alikuwa Dar es Salaam. “Hakikisha mnaharakisha malipo ya wakulima lakini pia suala la uhakiki…

Soma Zaidi >>

RADI YAJERUHI WANAFUNZI 14 MKOANI KAGERA

Na Mwandishi wetu,Kagera. Wanafunzi 14 wa shule ya sekondari Rulongo muleba mkoani Kagera, wamelazwa katika hospitali ya Rubya baada ya kujeruhiwa na radi iliyoambatana na mvua leo saa 7:15 mchana kati yao wanafunzi watatu wanatajwa hali zao ni mbaya kiafya. Mganga mkuu wa hospitali ya Rubya wilayani Muleba George Kasibante amesema wanaotajwa kuwa na hali mbaya wameungua sehemu mbalimbali za miili yao na mwingine mmoja amepoteza fahamu na kwamba madaktari wanafanya liwezekanalo kuokoa maisha yao Amesema radi hiyo ilipiga vyumba vya madarasa, kidato cha pili na tatu ambapo baadhi ya…

Soma Zaidi >>

CHADEMA YATUMA SALAMU ZA POLE NCHINI KENYA KUFUATIA SHAMBULIZI LILILOFANYWA JANA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA)kupitia kwa mkuu wa idara ya habari na mawasiliano Tumaini Makene kimetuma Salamu za pole kwa Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta na wananchi kwa ujumla kufuatia shambulio lililotokea jana january 15 na watu 14 kufariki. Taarifa iliyotolewa leo kwa waandishi wa habari imesema,CHADEMA imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za tukio la shambulizi linalohusishwa na ugaidi, lililofanyika kwenye eneo lenye shughuli mbalimbali za kijamii, katika Hoteli ya DusitD2, Nairobi, nchini Kenya, siku ya Jumanne, Januari 15, mwaka huu. “Kipekee CHADEMA inatuma salaam za pole kwa watu wote…

Soma Zaidi >>

MWANAFUNZI ALIYEBAKA NA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI MWENZIE AKANA MAELEZO YA AWALI.

Na,Naomi Milton Serengeti Mathayo Songalaeli (21) mkazi wa kijiji cha Natambiso Wilaya ya Serengeti, amekana maelezo ya awali mara baada ya kusomewa maelezo hayo katika kesi yake ya Jinai namba 94/2018. Kabla ya kusomewa maelezo ya awali Hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya Ismael Ngaile alimtaka mwendesha mashtaka wa Jamhuri Faru Mayengela kumkumbusha mshitakiwa mashtaka yake. Akisoma mashtaka Faru alisema makosa yanayomkabili mshitakiwa ni mawili kosa la kwanza ni kubaka kinyume na kifungu 130(1)(2)(e) na 131(1)cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 Kosa la pili ni…

Soma Zaidi >>

BUNGE LASITISHA KUFANYA KAZI NA CAG

Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema kwa sasa Bunge limesitisha kufanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad. Aidha Ndugai amewatawanya wajumbe wa Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na ile ya Hesabu za Serikali za Tawala za Mikoa na Mitaa (LAAC) kufanya kazi katika kamati nyingine. Hatua ya usitishaji huo inatokana na kauli ya Profesa Assad aliyoitoa Desemba mwaka jana katika mahojiano na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, Arnold Kayanda. Mtangazaji huyo alimuuliza CAG kuwa ni…

Soma Zaidi >>

DC NJOMBE AAGIZA KUSHUSHWA VYEO AFISA ELIMU,MRATIBU ELIMU KATA YA RAMADHANI

Na Amiri kilagalila Mkuu wa Wilaya ya NJOMBE RUTH MSAFIRI ameagiza kushushwa vyeo afisa elimu kata ya Ramadhani ESTER MJUJULU, Mratibu Elimu wa kata hiyo HURUMA MGEYEKWA pamoja na Mkuu wa Shule ya Sekondari MAHEVE, VALENO KITALIKA kwa Tuhuma za kuwatoza wazazi michango ya madawati kiasi cha shilingi Elfu Thelathini. Hayo yameibuka wakati Mkuu wa wilaya ya Njombe alipokuwa akikagua ujenzi wa madarasa yanayojengwa kwa ajili ya kidato cha kwanza Katika Shule hiyo ambapo amesema kitendo hicho ni kinyume na maelekezo ya Rais JOHN MAGUFULI ya kukataza watendaji kuchangisha michango…

Soma Zaidi >>

MAKAMBA AITA NEMC KUIGA UTENDAJI WA TFS

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira ) Mhe. January Makamba ameitaka bodi ya NEMC kuiga utendaji kazi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Makamba aliyasema hayo wakati akimkabidhi rasmi vitendea kazi Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo mara baada ya kuzindua Bodi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere mapema siku ya jana Prof. Silayo ni miongoni mwa wajumbe nane walioteuliwa kuunda bodi…

Soma Zaidi >>

MILIPUKO NA MILIO YA RISASI YASIKIKA JIJINI NAIROBI, MAGARI YACHOMWA MOTO,WENGI WAJERUHIWA.

Na,Jovine Sosthenes. Taharuki iliibuka jana mjini Nairobi kufuatia shambulio la milipuko na risasi inayosadikiwa kufanywa na magaidi katika eneo la 14 Riverside Drive, katika Hoteli ya Dusit D2 jijini Nairobi, Kenya na kusababisha vifo vya watu watano na kujeruhi wengine tisa. Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Kenya, Shambulio hilo linadaiwa kutokea Januari 15,2019. Mda, saa 9 alasiri na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa huku magari manne yakichomwa moto na milio ya risasi ikidaiwa kusikika kutoka eneo la tukio. Bado wahusika wa shambulio hilo hawajajulikana lakini askari wa Kitengo cha…

Soma Zaidi >>