UWEKEZAJI BILA SIASA UNAWEZEKANA :ISSA SAMMA

Na Mwandishi wetu -NGARA KAGERA Msemaji wa wawekezaji kutoka Korea Kusini katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera Issa Samma amesema wakazi wa wilaya hiyo na viongozi wao wanaweza kukubali au kukataa uwekezaji bila kulumbana kwa kutanguliza siasa, ukanda na ukabila. Samma ametoa kauli hiyo siku chache baada ya mbunge wa jimbo la Ngara Alex Gashaza kunusurika kupigwa na wananchi wa kijiji cha Kazingati akipinga utaratibu uliotumika wa kuwagawia ardhi wawekezaji wa Korea Kusini wilayani Ngara. Amesema wawekezaji walijitokeza kutaka ardhi ya kilimo na kujenga viwanda Kuanza katika kijiji cha Kazingati…

Soma Zaidi >>

WAFANYABIASHARA WANAOKWEPA KODI WAPEWA SOMO KAGERA

Na Allawi Kaboyo-Bukoba Kagera. Mkuu wa mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amewataka wafanyabiashara mkoani humo kuacha tabia ya kufunga maduka yao palea wanapowaona maafisa wa TRA wakija katika maduka yao na kumuagiza meneja TRA wa mkoa huo kujenga mahusiano mazuri na wafanyabiashara pamoja na kutoa elimu ya kutosha ya umuhimu wa kulipa kodi. Mkuu wa mkoa ametoa agizo hilo katika kikao chake na wadau wa kodi,maafisa wa TRA pamoja na wafanyabiashara kilichofanyika january 11 mwaka huu kwenye ukumbi wa manispaa ya Bukoba kikiwa na lengo la kujua hali ya…

Soma Zaidi >>

ATOROKA KIFUNGO BAADA YA USHAHIDI KUMMBANA

Na Stephen Noel Mpwapwa -Dodoma. Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Julias Lwagila (51)aliyekuwa anakabiliwa na tuhuma za kulima zao la Bangi Heka tatu atoroka kifungo. Mtuhumiwa huyo hakuonekana mahakamani wakati wa kusomewa hukumu hiyo kitu kinachopelekea kuaminika kuwa ametoroka hukumu Hiyo baada ya kuona kesi inamwendea vibaya. Pamoja na kutokuwapo mahakamani lakini Mahakama ya Hakimu mkazi ya wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma imewahukumu watuhumiwa wengine kifungo cha miaka thelathini (30) bwana Julius Lwagila mkazi wa kijiji cha Wota, Kata Lwihomelo na wilaya ya Mpwapwa. Kesi hizo zilikuwa zinasikilizwa na…

Soma Zaidi >>

SERIKALI YAINGIA MKATABA NA KAMPUNI NNE ZA KUBANGUA KOROSHO

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga jana (10 Januari 2019) ameshuhudia hafla ya utiaji saini mikataba ya ubanguaji korosho kati ya Bodi ya nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania na wenye viwanda vya ndani. Mkurugenzi wa Bodi ya nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania Dkt Hussein Mansoor ndiye ametia saini kwa niaba ya serikali na Kampuni nne zimesaini mikataba ya awali kuanza kazi hiyo ambazo ni kampuni ya Hawte Investment Co. Ltd, Micronix Mtwara, Korosho Afrika, na Micronix-Newala. Kampuni hizo zimeingia mikataba ya Jumla ya Tani 7500 ambapo kampuni ya Hawte Investment Co.…

Soma Zaidi >>

MWILI WA MTOTO ALIYEPOTEA WIKI MBILI ZILIZOPITA WAKUTWA KATIKA PORI NJOMBE

Mwili wa mtoto wa miaka 6 anayefahamika kwa jina la Godluck Mfugale aliyepotea wiki mbili zilizopita mkoani Njombe wakutwa katika pori lililopo karibu na shule ya sekondari Njombe (NJOSS) ukiwa umeharibika. Akizungumza wakati wa Ibada ya kuuaga mwili huo iliyofanyika katika kanisa la KKKT mtaa wa Melinze mjini Njombe,mchungaji wa KKKT jimbo la Njombe Bernad Sagaya amesema kuwa mwili wa mtoto huyo ulipatika siku ya jana ukiwa umeharibika hali ambayo imewashtua wakazi wa mji wa Njombe kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya mauaji ya watoto. Aidha kiongozi huyo wa kanisa…

Soma Zaidi >>

WAHANDISI WA MAJI WASIOKUWA NA SIFA WAKALIA KUTI KAVU.

Na mwandishi wetu-Bukoba Naibu waziri wa Maji na Mbunge wa Jimbo la Pangani Mh. Jumaa Aweso amewataka wahandisi wasiokuwa na sifa na Vigezo ndani ya wizara hiyo hususani wahandisi wababaishaji, kujitathimini mapema kwani msasa utapita kwa ajili yao. Aweso ametoa tamko hilo akiwa Mkoani Kagera katika ziara Mahususi iliyoanzia katika Ofisi za Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Mjini Bukoba (BUWASA), kisha kutembelea kituo cha uzalishaji maji kilichopo Bunena, Bukoba Manispaa na baadae kukagua tanki la Maji lililopo Kashura na lile linalojengwa Ihungo ndani ya Manispaa ya Bukoba. Katika…

Soma Zaidi >>

MBUNGE LUPEMBE APELEKA MABILIONI YA FEDHA JIMBONI KWAKE WAPIGAKURA WAELEZA.

Na Maiko Luoga Njombe Wananchi wa Jimbo la Lupembe katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Mkoani Njombe Wamempongeza Mbunge wa Jimbo Hilo Mh. Joramu Hongoli Kwakile walichoeleza Kuwa Mbunge Huyo Anafanya Kazi kwa Umoja na Mshikamano na Wananchi wake Ikiwemo Kufika Mara kwa Mara Jimboni humo na Kusikiliza Kero zinazowakabili. Wakizungumza na Mwandishi wetu Aliyetembelea Baadhi ya Kata jimboni humo Ikiwemo kata za Lupembe, Matembwe, Ikuna, Kidegembye Pamoja na Idamba Wananchi hao Walisema Kuwa Kupitia Msukumo na Ufuatiliaji wa Mbunge Huyo Tayari Serikali Kupitia Rais Magufuli Imetoa Fedha Kiasi cha…

Soma Zaidi >>