BENKI KUU YA TANZANIA YATOA MAAGIZO

BENKI Kuu ya Tanzania(BoT) imetoa tangazo kwa umma kupitia tovuti yake (www.bot.go.tz) likiwataka watu na taasisi zote zinazofanya biashara ya huduma ndogo za fedha zilizoko Tanzania Bara (isipokuwa vyama vya ushirika vya akiba na mikopo – SACCOS) kutoa taarifa zitakazotumika katika utayarishaji wa Kanuni za Usimamizi wa Huduma Ndogo za Fedha. “Bali ni kukusanya taarifa za awali kuhusu huduma hizo, kama amnavyo ilivyoainishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kupitisha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018, lengo la sheria hiyo ni kuwalinda wadau…

Soma Zaidi >>

HUYU NDIO KOCHA ZAHERA AJA NA MPANGO HUU WA KUONDOA NJAA KWA WACHEZAJI WAKE WA YANGA

HUKU mashabiki wa Yanga wakiiona timu yao haina fedha na masikini kumbe wanajidanganya  baada ya kocha mkuu wao kipenzi, Mwinyi Zahera, kutamka wazi kwamba anaweza kuifanya klabu hiyo kumaliza ukata wa kifedha ndani ya miezi miwili kutokana na hazina kubwa ya wanachama na mashabiki iliyonayo. Yanga ni klabu kongwe nchini, lakini imekuwa ikishindwa kutumia rasilimali ilizonazo katika kujiletea maendeleo, huku baadhi ya wadau wakidai tatizo hilo linasababishwa na viongozi wanaojali masilahi yao binafsi na si ya klabu. Pamoja na kuwa na majengo mawili katika ya Jiji la Dar es Salaam,…

Soma Zaidi >>

SIMBA YAMUANDAA BEKI HUYU KISIKI KUBEBA MIKOBA YA NYONI KWENYE MECHI NA WAARABU ,KOCHA MBELGIJI AFUMUA KIKOSI CHAKE

KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems, ameanza kumwandaa beki wake, Jjuuko Murushid, kuchukua nafasi ya Erasto Nyoni, ambaye hatakuwepo katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura ya Algeria Jumamosi ya wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. katika Mechi hiyo Simba wanahitaji kila aina ya njia kuwakalisha waarabu ambapo Nyoni ameondolewa katika mipango ya  kocha huyo katika mchezo huo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuumia goti wakati wa mechi ya juzi ya Kombe la Mapinduzi…

Soma Zaidi >>

SHAMBULIO LA AIBU LAMFIKISHA MAHAKAMANI MWINGINE ASHITAKIWA KWA KUJARIBU KUBAKA

Watu wawili wamefikishwa mahakama ya wilaya ya Serengeti kujibu mashtaka katika kesi mbili tofauti mmoja akijaribu kubaka na mwingine akifanya shambulio la Aibu Mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya Ismael Ngaile mwendesha mashtaka wa Jamhuri Renatus Zakeo alisema katika shauri la jinai namba 2/2019 mshitakiwa Manyama Machota(36) mkazi wa kijiji cha Robanda wilayani hapa anashitakiwa kwa kosa moja la Shambulio la aibu Zakeo alisema mshitakiwa alitenda kosa hilo Juni 9 mwaka 2018 katika kijiji cha Robanda baada ya kumshika binti aitwaye Zawadi Peter(16) sehemu mbalimbali za mwili wake bila…

Soma Zaidi >>

YANGA WAANZA MIPANGO YA KUMTAFUTA MRITHI WA MANJI,WANACHAMA WAPEWA NENO HILI

WAKATI suala la Uchaguzi wa Yanga likiwa bado kizungumkuti huku ikitajwa uwenda siku ya uchaguzi kukatokea fujo ya kupinga uchaguzi,wanachama wa Yanga wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye kampeni za uchaguzi ambazo zimezinduliwa rasmi leo katika Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na viongozi wa Yanga pamoja na wale wa TFF kwa ajili ya kujaza nafasi zilizo wazi kuanzia ile ya Mwenyekiti iliyokuwa wazi baada ya Yusuf Manji kujiuzulu pamoja na Makamu Mwenyekiti na wajumbe wengine. Uchaguzi wa Yanga unatarajiwa kufanyika Januari 13 katika ukumbi wa Polisi Messi Oysterbay kuanzia…

Soma Zaidi >>

RC MAKONDA KUWAKAMATA WANAFUNZI WATORO

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam amewataka wanafunzi wote waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kuripoti shuleni bila kisingizio chochote. Agizo hilo amelitoa mapema leo ofisini kwake wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuwataka wazazi kuwapeleka watoto wao mashuleni kujiandikisha kidato cha kwanza kwa wale waliofaulu na ikibainika mwanafunzi yeyote amefaulu kisha ameacha kwenda shuleni atakamatwa. “Tukibaini wewe ni mwanafunzi umefaulu halafu umeacha kwenda kwa sababu yoyote ile ya kisingizio tutakukamata,tunachotaka tutumie fursa hii watoto wote wa kitanzania na wanyonge ambao Rais Magufuli amekusudia wapate elimu…

Soma Zaidi >>

SPIKA NDUGAI ASUTWA KILA KONA,NI BAADA YA KUMTAKA CAG AJISALIMISHE ,WENGI WATAMANI KUONA CV YAKE

NI siku moja kupita tangu spika wa Bunge Job Ndugai akimtaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG)profesa MUSA ASSAD kufika mbele ya kamati ya Haki,Maadili na Madaraka ya Bunge Januari 21 mwaka huu  ili akajieleze na kuthibitisha maneno yake aliyoyatoa nchini Marekani wakati akihojiwa na chombo kimojawapo cha habari.Lakini hali na mapokeo kwa baadhi ya wasomi,viongozi na wanasiasa mbali mbali  nchini wamekuwa na mapokeo tofauti na kukosoa wazi wazi katika mitandao ya kijamii  juu ya agizo hilo kwa mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali.Agizo la Spika NDUGAI linatokana…

Soma Zaidi >>

WENYEVITI WAGOMEA KIKAO KISA DIWANI KUKAIMISHA NAFASI YAKE KIMYA KIMYA

Na.Amiri kilagalila Wenyeviti wa serikali za mitaa kata ya kivavi halmashauri ya mjini makambako wamegoma kushiriki kikao cha kujadili maendeleo ya kata hiyo (KAMAKA) kwa kile kilicho elezwa kuwa ni kutokana na diwani wao kutokuhudhuria vikao. Wakizungumza na mtandao huu wenyeviti hao wamesema kuwa diwani wa kata hiyo BARAKA KIVAMBE ameshindwa kuhudhulia takribani vikao vinne pasipo kuwa na sababu za msingi, hali ambayo imepelekea shughuli za kimaendelo kukwama ndani ya kata hiyo hususani ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari DEO SANGA. “Tumefika hivi leo ni kwasababu ya…

Soma Zaidi >>

Mbunge Ritta Kabati Mgeni rasmi mchezo kati ya Panama Girls fc na Evergeen kesho uwanja wa Samora

NA mwandishi wetu , IRINGA MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) kesho jumatano kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa ligi kuu ya mpira wa miguu wanawake Tanzania maarufu kwa jina la Serengeti Lite Wome’s Premier League 2018/2018 kati ya wenyeji Panama Girls FC (Iringa ) na Evergreen Queens (Dar Es Salaam) Afisa habari wa Panama Girls Fc, Francis Godwin alisema kuwa mchezo huo ambao ni wa tatu kuchezwa nyumbani utachezwa katika uwanja wa Samora majira ya saa 10 jioni na wamemualika mbunge Kabati pamoja na viongozi…

Soma Zaidi >>

MBUNGE NYAMAGANA ATOA SH. 7,230,000.00 KUBORESHA SEKTA YA ELIMU KATA YA PAMBA NA BUTIMBA

Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula ametoa msaada wa shilingi 7,230,000.00 kuboresha sekta ya elimu Katika Kata mbili za halmshauri ya Jiji la Mwanza ikiwemo Kata ya Pamba na Butimba, msaada uliolenga ukarabati wa madarasa mawili shule ya Msingi Butimba B, ukamilishaji wa ujenzi wa darasa moja shule ya Msingi Amani pamoja na ujenzi wa uzio kudhibiti utoro kwa wanafunzi Shule ya Sekondari Mlimani. Mhe. Mabula akikabidhi msaada huo kwa nyakati tofauti amefafanua shilingi 4,000,000.00 fedha taslimu zimetolewa kupitia mfuko wa Jimbo na vifaa vya ujenzi Bati na Saruji…

Soma Zaidi >>