LUGOLA AMPA WIKI MBILI KAMISHINA UHAMIAJI NCHINI KUWAONDOA WAHAMIAJI HARAMU MIKOA YA KAGERA NA KIGOMA KABLA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

Na Mwandishi wetu-Karagwe Kagera. WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amempa wiki mbili Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini (CGI) Dkt Anna Makakara, awe amefika Mikoa ya Kagera na Kigoma kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kufanya operesheni kubwa ya kuwaondoa Wahamiaji haramu katika Mikoa hiyo kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu. Akizungumza na mamia ya wananchi wa Mji wa Karagwe katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Changarawe mjini humo, Lugola alisema kuna idadi kubwa ya wahamiaji haramu katika…

Soma Zaidi >>

KOCHA MBELGIJI WA SIMBA AMEPANIA AISEE ,AZIPANGA BUNDUKI HIZI HATARI KWENYE MECHI YA KMKM.

Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems ameamua kupanga kikosi Full Masinondo katika mechi ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya KMKM, ikielezwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi yao ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya JS Saoura ya Algeria. Mashabiki wengi walishangazwa baada ya kikosi cha Simba kuonekana kikiwa sawa na kile ambacho Simba hukitumia kwenye Ligi Kuu Bara. Sehemu ya benchi la ufundi la Simba limeeleza: “Kocha ameamua kufanya match fitness. Kutaka wachezaji wawe fiti zaidi. Baada ya mechi hiyo wataendelea na mazoezi. “Lengo ni kujiandaa na Waalgeria halafu pia…

Soma Zaidi >>

TAASISI YA PROJEKT INSPIRE YAENDELEA KUWAINUA WANAFUNZI KUPENDA MASOMO YA SAYANSI.

  Na, Karoli Vinsent. Serikali ya Uingereza kwa kushirikiana na Taasisi ya Projekt Inspire imehaidi kuwainua wanafunzi Katika somo la teknolojia ili kuondokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili. Akizungumza mwishoni mwa wiki kwa niaba ya barozi wa Uingereza Marc Thayre ambani ni Mkuu wa Masuala ya siasa, Habari na mambo ya ndani alisema wamehamua kuwainua vijana kwa sababu ndiyo nguvu kazi ya baadae. Alisema wapo kwa ajili ya kuwainua vijana kupitia mawazo yao mpya ya teknolojia ambayo ambayo yataweza kuleta maendeleo Katika jamii. “Tupo kwa ajira ya kuwainua vijana kupitia teknolojia…

Soma Zaidi >>

UKIMSHIKA HAPA AUNT EZEKIEL USHAMMALIZA

SUPASTAA wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel, amesema kama unataka kumjua upande wake wa pili wa shilingi, jaribu kuyafuatilia mapenzi yake na mzazi mwenzake, Moses Iyobo ambaye ni dansa wa kutegemewa katika Kundi la Wasafi Classic Baby (WCB), utakiona cha mtemakuni. “Hivi kwa nini uhangaike kuyajua maisha yangu na mpenzi wangu? Leo tumegombana au tumepatana au tunaelekea kuachana, inakuhusu nini wewe? Maana hata tulivyoanza uhusiano watu walishtukizia tuko kwenye uhusiano hivyo hata kama tukiachana wataona hivyohivyo,” alisema wakati akizungumza na Ijumaa hivi karibuni. Aliongeza: “Nimekuwa nikisikia minon’gono mingi kuhusu kuachana…

Soma Zaidi >>

ALIKIBA KWENYE TUHUMA NZITO ZA WIZI

Msanii mkonge wa muziki wa Bongo Fleva, Domo Kaya amesema kuwa wasanii wapya kwenye muziki huo wanatakiwa kuwa wabunifu, baada ya msanii Alikiba kutumia kidokezo ‘Yebaba’ ambacho alikuwa alikitumia yeye mwanzo. Domo Kaya amefunguka hayo kupitia FRIDAY NIGHT LIVE ya EATV, ambapo amesema kuwa Alikiba kutumia neno hilo sio vibaya lakini alitakiwa kuomba ruhusa kwanza kwake. “Nawasihi wadogo zetu kuwa wabunifu, na kuacha ujanja ujanja maana kutumia kitu hukatazwi lakini uombe kwa muhusika akupe baraka zake”, amesema Domo Kaya. Hivi karibuni msanii Alikiba ameonesha kutumia msemo huo ‘yebaba’ katika wimbo…

Soma Zaidi >>

MWANAMKE AKIKUJIBU HIVI,KIMBIA HARAKA

Ukiona umemtumia mpenzi wako/mchumba wako/mchepuko wako/mke wako au hata rafiki wa kike wakati mwingine SMS ya kawaida tu kwaajili ya kumsalimia lakini yeye akakujibu moja kati ya majibu yafuatayo, tafadhali sana usiendelee kuchat nae maana kinachofuata hapo ni majanga tu. KWA MFANO: 1. Ukimtumia sms ”Mambo mpenzi wangu?” akikujibu ”mambo mabaya”, usimuulize kwanini mambo mabaya, ukimuuliza atakwambia kuwa ”sina hela dear” 2. Ukimtumia sms ”Maisha yanasemaje kipenzi changu” akikujibu ”maisha magumu hubby wangu we acha tu” usimuulize kwanini, ukimuuliza kwanini atakwambia ”nimefulia mwenzio kama nini sijui” 3. Ukimtumia sms ”Mbona…

Soma Zaidi >>

DKT. BASHIRU ASHAURI WAKUU WA MIKOA KUJIFUNZA SIMIYU

  Na Stella Kalinga, Simiyu Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally amewashauri Wakuu wa Mikoa hapa nchini kwenda(kuja) kujifunza namna ya kufanya kazi kwa umoja na mshikamano kati ya Chama na Serikali sambamba na ubunifu na uchapakazi wa viongozi wa mkoa huo.   Dkt. Bashiru ameyasema hayo Januari 05, 2019 wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM pamoja na Viongozi na watendaji wa Serikali, Mjini Bariadi wakati akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu.   Dkt. Bashiru amewapongeza Viongozi wa Serikali wakingozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,…

Soma Zaidi >>

MGOGORO WA UUZAJI VIWANJA VYA KKKT WAMFIKISHA LUKUVI NJOMBE

Na Maiko Luoga Njombe. Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.Willium Lukuvi Amewataka Watumishi wa Wizara hiyo Nchini kuwafikia Wananchi Katika Maeneo yao Ili kutatua Kero zinazowakabili Ikiwemo Kumaliza Migogoro ya Ardhi Inayowakabili Wananchi Kote nchini. Waziri Lukuvi Ametoa Agizo hilo katatika Ukumbi wa Turbo Njombe Mjini wakati Akizungumza na Mamia ya Wananchi waliojitokeza katika Ukumbi huo na Kuwasilisha Kero zao Kupitia Program ya Funguka kwa Waziri Ambapo Baada ya Kuona Kero nyingi za Wananchi wa Njombe zaidi ya 300 Ndipo Mh. Lukuvi Aliamua kutoa Maagizo hayo kwa…

Soma Zaidi >>

DKT. BASHIRU AWAONYA VIONGOZI WALIOANZA KUTAFUTA UBUNGE KABLA YA WAKATI.

  Na Stella Kalinga, Simiyu Katibu Mkuu wa Chama cha Mpinduzi (CCM) Taifa Dkt. Bashiru Ally amewaonya baadhi ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, na Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma, ambao wameanza kukaa vikao kwa ajili ya kutafuta majimbo kabla ya wakati wa Chama hicho kutangaza mchakato wa kutafuta wagombea wapya wa ubunge na udiwani.   Dkt. Bashiru ameyasema hayo Januari 05, 2019 wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM pamoja na Viongozi na watendaji wa Serikali katika wilaya…

Soma Zaidi >>

MABULA AMFAGILIA MHE. MAGUFULI KWA KASI YA UTENDAJI WA TARURA KWENYE MIRADI 10 INAYOGHARIMU BI. 5.8

Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula amempongeza Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa uanzishwaji wa Wakala wa barabara Mjini na Vijijini TARURA ambacho kimekuwa chapa halisi ya ukombozi kwenye sekta ya miundombinu ya barabara Wilayani Nyamagana kwa kutekeleza miradi 10 yenye thamani ya shilingi 5,822,854,934.00 kwa kasi na kiwango katika mwaka wa fedha 2018 hadi 2019. Mhe. Mabula akiwa ameambatana na Mjumbe kamati ya siasa CCM wilaya ya Nyamagana ambaye pia ni Mwenyekiti wa UWT Wilaya Mhe. Witness Makale walilakiwa na mwenyeji wao Meneja TARURA wilaya ya Nyamagana Mhandisi…

Soma Zaidi >>