UPEPO MKALI NA MAWIMBI YAVIKUMBA VIJIJI VYA THAILAND.

  Na. Jovine Sosthenes Mvua, upepo mkali na mawimbi vimelikumba eneo la kusini mwa Thailand hususani katika maeneo ya vijiji vilivyo jirani na fukwe ikiwemo maeneo ya utalii yaliyokumbwa na kimbunga kikali cha Papuk. Hakuna taarifa ya vifo lakini tayari mamlaka ya hali ya hewa nchini humo imetoa tahadhari huku ikishuhudiwa mamia ya watalii wakiondoka katika maeneo waliyokuwepo. Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini humo imesema kimbunga kingine kikubwa kinatarajiwa kupiga jioni ya leo na kitakua kina kasi ya kilomita 80 kwa saa. Kimbunga hicho kinatarajiwa kupiga zaidi eneo la Nakhon…

Soma Zaidi >>

BITEKO AKERWA NA AJALI MAENEO YA WACHIMBAJI WA MADINI MKOANI MARA.

  Na. Augustine Richard. Naibu Waziri wa Madini, Doto Mashaka Biteko leo Januari 4, 2019 amewataka wachimbaji wadogo katika eneo la uchimbaji mji wa Buhemba wilayani Butiama mkoani Mara kuzingatia uchimbaji salama ili kuepusha ajali zinazotokea mara kwa mara katika maeneo ya migodi. Biteko ameyasema hayo wakati wa mafunzo kwa wachimbaji wadogo yaliyofanyika wilayani Butiama mkoani Mara yenye lengo la kuwafundisha wachimbaji wadogo masuala ya uchimbaji salama, uchenjuaji, afya,umhimu wa kulipa kodi na tozo mbalimbali na mazingira ya uchimbaji katika mkoa wa Mara. “Akifa mtanzania mmoja huyo Mtanzania ni muhimu…

Soma Zaidi >>

WANAFUNZI 463 WAKOSA NAFASI KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA WILAYANI NJOMBE,UHABA WA MADARASA WACHANGIA

Na Amiri kilagalila-Njombe Halmashauri ya wilaya ya Njombe imefanikiwa kutafuta muarobaini wa wanafunzi zaidi ya 400 waliokosa nafasi ya kujiunga kidato cha kwanza kutokana na ukosefu wa vyumba vya madarasa kwa kuchukua hatua za haraka katika ujenzi wa vyumba vilivyokuwa pungufu katika halmashauri hiyo. Kwa mujibu wa afisa elimu taaluma sekondari Christopher haule katika halmashauri hiyo amesema licha ya wanafunzi 1953 kufaulu vyema mtihani wa darasa la saba lakini wanafunzi 1230 ambapo wavulana wakiwa 710 na wasichana 983 pekee huku wanafunzi 463 wakikosa nafasi kutokana na upunfungufu wa vyumba tisa…

Soma Zaidi >>

WAWILI WAONGEZEKA KATIKA SHAURI LA JINAI LINALOHUSISHA UPOKAJI NA UBAKAJI SERENGETI

Na,Naomi Milton Serengeti Watu wawili wamefikishwa mbele ya mahakama ya wilaya ya Serengeti kujibu mashtaka yanayowakabili katika shauri la jinai namba 325/2018 ambalo lilikuwa na mshitakiwa mmoja hivyo wameongezwa wawili na kufanya idadi ya washitakiwa katika shauri hilo kufikia watatu Mwendesha mashtaka wa Jamhuri Faru Mayengela mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya Ismael Ngaile alitoa maombi ya kuongeza washitakiwa wawili baada ya mshitakiwa wa kwanza kusomewa mashtaka Disemba 28/2018 Akisoma upya hati ya mashtaka Faru aliwataja washitakiwa hao kuwa ni Mwita Marwa(24) Chacha Mwita(34) na Moshi Mayenga(42) wakazi wa…

Soma Zaidi >>

MENO 10 YA TEMBO NA BUNDUKI YA AINA YA SMG YAWAPELEKA WAWILI JELA MIAKA 25.

  Na, Naomi Milton Serengeti Jummane Azori(43) mkazi wa Songambele Kigoma na Pala Yoram(29) mkazi wa Uvinza Kigoma wamehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela kila mmoja katika kesi mbili tofauti moja ni kuhujumu uchumi na ya pili ni kupatikana na silaha ambayo ni Bunduki aina ya SMG. Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya Ismael Ngaile katika mahakama ya wilaya ya Serengeti baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa kwa upande wa mashtaka dhidi ya washtakiwa hao. Kabla ya kusomwa kwa hukumu hiyo mwendesha mashtaka wa Jamhuri Emmanuel…

Soma Zaidi >>

WAKILI FATUMA KARUME AWAUMBUA WAKINA MUSIBA NA WENZAKE,

AMEWAUMBUA ndivyo naweza kusema baada ya Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume, kuibuka na kusema hana mpango wowote kwa sasa wa kumiliki kadi ya chama cha siasa nchini badala yake amedai ataendelea kutoa maoni juu ya masuala mbalimbali nchini kupitia taaluma yake ya sheria. Kauli hii ya Wakili Karume inakuja ikiwa ni teyari watu mbali mbali akiwemo Anayejiita Mwanaharakati Mzalendo,Cyprian Musiba kumtuhumu kuwa ni mwanachama wa vyama vya upinzani na anatumiwa kuikwamisha serikali. Wakili huyo anayesifika kwa kutetea haki za binadamu amebainishwa kuwa “sijwahi kumiliki na wala…

Soma Zaidi >>

NECTA IMETANGAZA MATOKEO YA MTIHANI WA TAIFA WA DARASA LA NNE NA KIDATO CHA PILI.

DODOMA. Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) leo Ijumaa Januari 4, 2019 limetangaza matokeo ya mtihani wa Taifa wa darasa la nne na kidato cha pili iliyofanyika Novemba 2018, kueleza kuwa ufaulu umeongezeka ikilinganishwa na matokeo ya 2017. Akizungumza leo mjini Dodoma katibu mtendaji wa baraza hilo, Dk, Charles Msonde amesema kati ya watahiniwa 1,302,461 wa darasa la nne waliofanya mtihani huo sawa na asilimia 95.58, waliofaulu kwa kupata daraja A, B, C, na D ni 1,213,132 sawa na asilimia 93.16. Amesema wanafunzi 89,093 sawa na asilimia 6.84 wamepata alama…

Soma Zaidi >>

MTETEZI HUYU WA HAKI ZA BINADAMU AWACHANA WANAOMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWENYE SAKATA LA WASTAAFU,

NA KAROLI VINSENT WAKATI kukiwa na Maandamano kila mahala  ya kumpongeza Rais John Magufuli kwa hatua yake kuzuia ukokotoaji mpya kwenye mifuko ya jamii, Maandamazo hayo yamepingwa vikali na Aliyekuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)Dkt Hellen Kijo Bisimba,ambapo amesema Rais Magufuli hastahili kupewa pongezi kwa madai kuwa yeye na serikali yake ndio chanzo cha Matatizo hayo kwa wafanyakazi. Akizungumza na DarMpya.com Dkt Bisimba amesema hatua ya Rais Magufuli kutoa zuio kwa vikokotoaji huo ni ya kisiasa. “Ujue hapa kuna siasa mtu anatengeneza tatizo halafu anakuja…

Soma Zaidi >>

MAHAKAMA YAKATAA OMBI LA SERIKALI KUHUSU KESI YA KUPINGA MUSWADA WA VYAMA VYA SIASA

Na Bakari Chijumba, Mtwara. Mahakama Kuu ya Tanzania imeamua shauri la kesi ya kupinga muswada wa vyama vya siasa lisikilizwe kwa muda mfupi kwa kuwa kuna maslahi mapana ya umma, hivyo litasikilizwa tena Januari 11, 2019. Awali mawakili wa Serikali waliomba siku 21 ili isikilizwe lakini mahakama imekataa Ombi hilo la AG kuomba siku 21 ya kupata nafasi ya kushauriana na mamlaka mbalimbali ili Kujibu Hoja za Waleta Maombi. Akizungumza nje ya mahakama hiyo Kwa niaba ya wenzake kiongozi wa ACT, Zitto Kabwe ameishukuru Mahakama kwa kutambua uzito wa kesi…

Soma Zaidi >>

AJIBU KURITHI MIKOBA YA KELVIN YONDANI

  Na. Jovine Sosthenes. Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameamua kumvua kitambaa cha unahodha beki wa timu hiyo, Kelvin Yondani ‘Vidic’ baada ya kutohudhuria mazoezini pasipo kutoa taarifa. Zahera raia wa Congo amemkabidhi kitambaa hicho nyota wake Ibrahim Ajibu kufuatia kitendo cha utovu wa nidhamu kilichofanywa na Yondani. Beki huyo mwenye historia kubwa na Yanga kutokana na kudumu kwenye kikosi hicho kwa muda mrefu, mwanzoni mwa msimu huu alitangazwa rasmi kuwa nahodha wa timu hiyo akirithi mikoba ya Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye pia alikuwa akiitumikia nafasi kama hiyo awapo uwanjani. Taarifa…

Soma Zaidi >>