MBUNGE NA WANANCHI NGARA WATOFAUTIANA KUHUSU ARDHI WAMTAKA WAZIRI KUINGILIA KATI

Na Mwandishi wetu Mbunge wa jimbo la Ngara mkoani Kagera Alex Gashaza (CCM) amefanya mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Kazingati katika jimbo hilo chini ya vyombo vya ulinzi na usalama, baada ya kuwepo malalamiko ya kwamba anapinga wawekezaji kupata ardhi kijijini humo Mbunge huyo Gashaza amefanya mkutano huo hii leo ikiwa ni siku chache Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ngazi ya Taifa kuagiza uongozi wa wilaya ya Ngara kuacha mara moja mipango ya kugawa ardhi kwa mwekezaji kutoka korea Kusini Wawekezaji wa nchi hiyo wanahitaji ardhi…

Soma Zaidi >>

ZANZIBAR YAJIDHATITI NA UOKOAJI DHIDI YA AJALI ZA MAJI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK. Ali Mohamed Shein, amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejidhatiti kuwaokoa wananchi wake kutokana na ajali zinazotokea baharini kwa kununua vifaa vya kisasa vinavyokwenda na wakati uliopo. Dk. Shein alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kujiimarisha kwa kukipa vifaa vya kisasa vya uzamiaji na uokozi kikosi cha KMKM, ili kukabiliana na ajali zinazotokea baharini sambamba na kuimarisha usalama katika miji ya Unguja na Pemba. Dk Shein aliyasema hayo, katika uzinduzi wa Vituo vya Uokozi vya KMKM kwa…

Soma Zaidi >>

SERIKALI YAWATAKA WACHIMBAJI WADOGO KUWA WAZALENDO  KWA KULIPA KODI NA TOZO ZINAZOTAKIWA.

Hayo yamesemwa leo January 02, 2019 na Naibu Waziri wa Madini Mheshimiwa Doto Mashaka Biteko alipokuwa akifungua mafunzo ya uchimbaji wenye tija kwa wachimbaji wadogo wilaya ya Bukombe mkoani Geita. Akihutubia wachimbaji hao, Mheahimiwa Biteko ameendelea kuweka wazi nia ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr. John Pombe Magufuli ya kuhakikisha wachimbaji wadogo wanasaidiwa na kifikia uchimbaji wa kati ambapo jumla ya fedha taslimu shilingi Bilioni nane na milioni mia tano zimetengwa kwa ajili ya utafiti wa Madini wenye lengo la kuboresha uchimbaji wa wachimbaji wadogo. Fedha…

Soma Zaidi >>

MRADI WA UJENZI VYOO BORA KUTOKA MWAUWASA WAZINUFAISHA SHULE,ZAHANATI NA SOKO NYAMAGANA

Wilaya ya Nyamagana ni miongoni mwa wilaya mbili Mkoani Mwanza zinazonufaika na Mradi wa usafi wa Mazingira unaotekelezwa na shirika la Maji safi na maji taka MWAUWASA Mwanza Urban water Supply and Sanitation Authority, Kwa ujenzi wa Vyoo bora na Vya Kisasa katika shule 14, Zahanati moja ya Mkolani pamoja na Soko la Igogo. Akiongea katika ziara maalum MWAUWASA Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo la Nyamagana kukagua mradi wa usafi wa mazingira shule ya Msingi Mlimani, amesikitishwa na hali chafu ya mazingira ya vyoo vipya na kuwataka watendaji wa serikali…

Soma Zaidi >>

DUDU BAYA KUKICHAFUA WASAFI?

Godfrey Tumaini anayefahamika kwa jina la kisanii kama Dudu Baya (Konki Masta) ni miungoni mwa wasanii maarufu na wakongwe zaidi katika muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva),pia ni msanii miungoni mwa waanzilishi na wajenzi wa muziki huu ambapo alivuma sana miaka ya 2000 na ngoma zake kali kama nakupenda tu,Mpenzi,nimeondoka na nyimbo zingine kadha wa kadha ambazo zilimuweka na zinaendelea kumuweka kwenye ramani ya muziki mpaka sasa.Lakini nje ya muziki Dudu Baya amejiweka wazi kwamba ni mpinga ushoga namba moja akifikia hatua ya kutaja watu kadhaa ambao alisema wanajihusisha na…

Soma Zaidi >>

WALIMU NJOMBE WAMFAGILIA RAIS MAGUFULI

Na Amiri kilagalila Mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kutengua Matumizi ya Kikokotoo Kipya kwa Watumishi baada ya Kustaafu Chama Cha Walimu Mkoa wa Njombe kimempongeza Raisi kwa Utenguzi huo kwa kusema kuwa Rais Ametambua Shida wanazopiotia watumishi Mara baada ya Kustaafu. Akizungumza na mtandao huu Ofisini kwa hii Leo Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Mkoa wa Njombe Mekson Wizengo amesema Kwa kufanya Hivyo Raisi amerejesha imani na amani ya Mioyo ya Watumishi wa nchi hii wakiwemo walimu. “Msimamo wa chama cha…

Soma Zaidi >>

MHE. MABULA AKAGUA MIRADI YA MAJI YENYE THAMANI YA BI 46.81

Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula afanya ziara ya kikazi MWAUWASA “Mwanza Urban Water Supply and Sanitation Authority” Mamlaka ya maji safi na Maji taka Jijini Mwanza kukagua miradi saba ya maji inayotekelezwa katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza yenye thamani ya shilingi 46,810,000,000.00. Mhe. Mabula akiwa MWAUWASA amepokelewa na mwenyeji wake Kaimu Mkurugenzi Mhandisi. Magayane ambaye alipata fursa ya kutoa taarifa ya miradi yote inayotekelezwa na taasis hiyo matharani iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikiwemo Ujenzi wa Tank la maji Nyegezi pamoja na ulazaji wake wa…

Soma Zaidi >>

JAMII YATAKIWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUIBUA MATUKIO YA UKATILI DHIDI YA WATOTO.

Dodoma. Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto,imewataka wazazi,walezi na jamii kwa ujumla kuzingatia ulinzi wa mtoto ili kutekeleza lengo la la kupunguza matukio ya ukatili kwa silimia 50 ifikapo mwaka 2021!2022. Aidha,wizara hiyo imeitaka jamii kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii kwa kuepuka kutuma picha za watoto ambao ni wahanga wa ukatili na kuziweka wazi kinyume cha sheria ya mtoto ya mwaka 2009. Taarifa ya wizara imetolewa leo,baada ya kuwepo kwa taarifa mapema wiki hii juu ya mwalimu mmoja wa shule ya msingi jijini Dodoma,kumfungia mtoto…

Soma Zaidi >>

RAIS AL BASHIR ABANWA VIKALI NA WASUDANI, WAAMUA KUANDAMANA KWA MAMIA MJINI KHARTOUM

Khartoum, SUDAN. Maandamano makubwa yamefanyika mwisho wa mwaka 2018 katika mji mkuu wa Sudan Khartoum yakiitikia wito wa baadhi ya vyama vya upinzani na jumuiya za kiraia kwa ajili ya kulalamikia ughali wa maisha na hali mbaya ya uchumi wa nchi hiyo. Waandamanaji hao walikuwa wakielekea katika Ikulu ya Rais mjini Khartoum wakati walipokabiliwa na vyombo vya usalama vilivyolazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji hao waliokuwa wakipiga kelele dhidi ya serikali ya Rais Omar Hassan al-Bashir. Waandamanaji wengi walikuwa wamebeba mabango na maberamu yenye maandishi yasemayo ‘Irhal’ yaani…

Soma Zaidi >>

DRC:HUDUMA YA INTANETI NA KUTUMA SMS YAKATWA GHAFLA MPAKA MATOKEO YA UCHAGUZI YATAKAPOTANGAZWA.

Kinshasa, DRC. Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imekata huduma ya intaneti na ujumbe wa mfupi wa simu za mkononi (SMS) kote nchini humo kwa siku ya tatu mfululizo hii leo wakati nchi hiyo ikisubiri kwa hamu kubwa matokeo ya kwanza ya uchaguzi wa Rais. Hali hii imetokea kuanzia juzi Desemba 31 kufuatia uchaguzi wa Rais nchini humo, uliofanyika Jumapili iliyopita, huku baadhi ya mikoa ikigubikwa na ghasia na machafuko. Pande mbili za upinzani na muungano wa chama tawala hapo juzi (Desemba 31) zilieleza kuwa, zinaelekea kuibuka na…

Soma Zaidi >>