WAJUMBE WAPYA KAMISHENI YA UTUMISHI WA UMMA WAAPISHWA.

Zanzibar, Mjini. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti Wa Serikali Ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, jana amewaapisha wajumbe wapya wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar. Hafla hiyo iliyofanyika Ikulu mjini Zanzibar ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Washauri wa Rais, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mzee Ali Haji. Wajumbe walioapishwa katika hafla hiyo ni Dk. Mohamed Seif Khatib, Mbaraka Mohammed Abdulwakil na Sheikh Hassan Othman Ngwali. Wengineo ni Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh…

Soma Zaidi >>

SAKATA LA KOCHA WA YANGA KUTIMKIA NCHINI UFARANSA LAWACHANGANYA VIONGOZI

NI MKANGANYIKO ndani ya timu ya Yanga ndivyo naweza kusema baada ya hatua ya   Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera kuondoka nchini kwenda Ufaransa. Mkanganyiko huo umeibuka baada ya viongozi wa Yanga kujichanganya.kuhusu kiini cha kocha huyo mwenye mbinu kwenda nchini Ufaransa,utofauti huo uliibuka baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga, Hussein Nyika kusema kocha anakwenda Ufaransa kwa ajili ya kesi yake na mkewe. “Ni kesi, tena hili suala lilikuwepo na atarudi baada ya kesi,” alisema. Nyika amesema kesi hiyo imechukua miaka minne ndio na Zahera raia wa DR…

Soma Zaidi >>

MSANII DIAMOND AKIMSHA TENA,NI KWA WATOA HUDUMA KWENYE NDEGE ZA MAGUFULI,ATCL WANG’AKA

MSANII Bongo Fleva Diamond Platnumz ni kama akimsha tena ndivyo naweza kusema baada ya kulirushia lawama  Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL)  kwa kusema linatoa huduma mbovu . Diamond wakati akiyasema hayo leo huku Mkoani Mwanza, suala hio limewaibua ATCL na kuonesha masikitiko yake kutokana na tuhuma zilizotolewa na mteja na mteja wao ambaye pia ni msanii maarufu wa Bongo Fleva, Akizungumza na wanahabri leo, Msemaji wa ATCL, Josephat Kagirwa amesema tuhuma zilizotolewa na Diamond kuwa limeuza tiketi yake baada ya kubaini kuwa alichelewa kufika uwanjani siyo za kweli, na…

Soma Zaidi >>

AMUNIKE ATUA KAGERA KUSAKA VIPAJI

Na Allawi Kaboyo Bukoba. Mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho la mpira nchini (TFF) Ammy Ninje, amewataka vijana waliochaguliwa kujiunga na kambi itakayowezesha upatikanaji wa wachezaji wa kuongeza nguvu katika timu ya taifa ya wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 17, kujiendeleza kielimu. Ninje ametoa rai hiyo baada ya kukamilika kwa zoezi la kuwachagua wachezaji 14 watakaokwenda kujumuika na wachezaji wengine wenye umri wa chini ya miaka 17, katika kambi itakayowekwa mkoani Arusha mwezi Aprili mwakani. Amesema kuwa maisha ya mpira ni mafupi sana na kuwa wasiposoma sasa na kutegemea…

Soma Zaidi >>

JESHI LAAMUA KULINDA VISIMA VYA MAFUTA KWA MANUFAA YA WALIBYA

Tripoli, LIBYA. Afisa mmoja wa Libya aitwaye El Manzar al Kharrtosh, ametangaza kuwa wanajeshi wametumwa katika eneo linalojulikana kama Hilali ya Mafuta huko kaskazini mwa nchi, ambalo lina visima vikubwa zaidi vya mafuta na bandari kubwa za mafuta za nchi hiyo ili kudhamini usalama wa eneo hilo. Afisa huyo anayehusika na masuala ya habari katika kikosi cha 73 cha wanajeshi watembeao kwa miguu chini ya kamanda mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Libya, amesema kuwa brigedi ya 165 ya wanajeshi watembeao kwa miguu imetumwa katika eneo la Hilali ya Mafuta…

Soma Zaidi >>

SHIGONGO AIBUKA KWENYE SAKATA LA USHOGA,AKUBALI KUMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI

Dar es salaam. Mkurugenzi wa kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo ameshukia vikali barua ya maazimio 15 ya bunge la Umoja wa Ulaya kwa serikali ya Tanzania ambayo yanaonekana kuwa masharti magumu kwa taifa hasa suala la ushoga. Kupitia chapisho lake mtandaoni Shigongo amesema Umoja wa Ulaya umeweka masharti hayo magumu kwa kuwa Rais Magufuli amekuwa na misimamo thabiti juu ya rasilimali za taifa hasa pale alipozuia kusafirishwa kwa mchanga wa dhahabu (makinikia). >>Mimi nasimama na rais wetu, Dk. John Pombe Magufuli kuyapinga maazimio hayo kwani inaonesha wazi yamekuja kutokana…

Soma Zaidi >>

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YACHUKIZWA NA WAFANYABIASHARA

Zanzibar, Mjini. Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa 11 wa Jumuiya Ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda Na Wakulima Zanzibar (ZNCCIA). Uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip iliyopo Malindi mjini Zanzibar Makamu wa pili wa Rais, Balozi Seif alieleza, Serikali makini husisitiza umuhimu wa jumuiya ya Wafanyabiashara yenye kuleta manufaa na faida kwa kufungua milango ya biashara ndani na nje ya nchi Sambamba na kuongeza wigo wa pato la Taifa, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inachukizwa na kuona watu wachache wanaigeuza sekta ya biashara kuwa kichaka cha wakwepa kodi, wala…

Soma Zaidi >>

MBUNGE ZUNGU AWATAKA WANAWAKE ILALA KUCHANGAMKIA MIKOPO

Na Heri Shaban Dar es salaam Mbunge wa jimbo la Ilala Mussa Zungu,amewataka wanawake wa jimbo la Ilala kuchangamkia mikopo ya serikali isiyo na riba ambayo inatolewa na halmashauri ya manispaa ya Ilala. Zungu aliyasema hayo jijini Dar es Salam jana wakati wa kikao cha kufunga mwaka kinachoelezea maendeleo ya kata ya Upanga mashariki kilichoandaliwa na diwani wa kata hiyo Sultan Salim. “Serikali inatoa mikopo isiyo na riba,kwa watu watano watano na vikundi vilivyosajiliwa kwa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu”alisema Zungu. Aidha Zungu aliwaagiza maofisa maendeleo wa kata zote jimboni…

Soma Zaidi >>

BASTOLA YAMWOKOA MASAU BWIRE

Msemaji mwenye maneno mengi kutoka klabu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire, jana alikumbana na ‘songombingo” watoto wa mjini wanasema kutoka kwa mashabiki wa Yanga na kumlazimu kutoa bastola uwanjani ili kuwazuia mashabiki wa Yanga ambao walikuwa wakimzonga na kumkejeli. Awali Bwire alitamba kuivunja rekodi ya timu ya Yanga yakutofungwa mechi hata moja tangu ligi hiyo kuanza lakini mambo hayakuwa kama alivyopanga baada ya Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-2, ulisababisha mashabiki wengi wa Yanga kuanza kumtania Bwire ambaye alikuwa ameyapokea matokeo kwa masikitiko. Bwire amefunguka kuwa aliamua kufanya maamuzi…

Soma Zaidi >>

KOCHA ZAHERA AWACHANA VIONGOZI WA YANGA

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema amechukiwa na mabosi wake kufanya usajili wa golikipa Ibrahim Hamid ambaye hakuwa pendekezo lake. Zahera ambaye aliiongoza Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu Bara jana, alisema hayo ikiwa ni baada ya mechi hiyo kumalizika. Zahera alieleza kuwa mabosi wake wameamua kumzunguka tofauti na maagizo ambayo aliwapa ili kufanya usajili. Kitendo hicho kimefanya Zahera ashindwe kuvumilia na kuamua kuwachana LIVE viongozi wake bila ya kuonesha hofu ya kufuzwa kazi. Aidha, Zahera amewataka wanachama na…

Soma Zaidi >>