ASKOFU MENGELE:TUNGETENGENEZA KIZAZI CHA AJABU KUTOIMBA WIMBO WA TAIFA MASHULENI.

Na Amiry Kilagalila,Njombe. Askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)jimbo la kusini Isaya Mengele amemshukuru Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli, kwa kutoa marekebisho juu ya matumizi ya wimbo wa taifa pamoja na rangi za bendera ya taifa. Askofu huyo ametoa shukrani hizo mbele ya mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth msafiri wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo cha tumaini mkoani Njombe yaliyofanyika katika katika chuo hicho mkoani Njombe huku akimtaka mkuu huyo wa wilaya kuzipeleka shukrani za kanisa hilo kwa Rais.…

Soma Zaidi >>

NAIBU WAZIRI NISHATI ACHANGIA MIFUKO 50 YA SARUJI KUUNGA MKONO UJENZI KITUO CHA AFYA MSANGANI.

Pwani. Naibu waziri wa nishati ambaye pia ni mbunge wa viti maalumu mkoa wa Pwani Subira Mgalu amechangia mifuko hamsini ya saruji katika ujenzi wa kituo cha afya Msangani ikiwa ni kutimiza ahadi yake. Akiwa kwenye ziara ya ufuatiliaji wa miradi ya kimkakati katika halmashauri ya Kibaha amekabidhi mifuko hiyo ya saruji kwa uongozi wa Msangani ambao ndiyo unaosimamia ujenzi huo mbele ya mbunge wa Kibaha Mjini Silyvestry Koka, Mhe.Mgalu amepongeza wananchi wa maeneo hayo kwa kujitolea kwenye shughuli za kimaendeleo hasa kwa ujenzi wa kituo cha afya ambapo ukikamilika…

Soma Zaidi >>

SAKATA LA MAKATO YA WASTAAFU ,SERIKALI YAIBUKA NA KUTOA NENO.

  Na Karoli, Vinsent. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama amesema serikali imeshapata barua kutoka kwa chama cha Wafanyakazi nchini (TUCTA) inahuyosu malalamiko kuhusu ukokotoaji mpya wa mafao ya kustaafu kupitia mifuko ya hifadhi Jamii. Waziri Mhagama ameyasema hayo jana Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa amefanya ziara kwenye ofisi ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (Osha). Amesema teyari serikali imeshapata Barua kutoka TUCTA na kufikia uamuzi wa kukutana na chama hicho kwa…

Soma Zaidi >>

WANAFUNZI 12,399 WACHAGULIWA  KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2019 SIMIYU.

Simiyu. Jumla ya wanafunzi 12,399 mkoani Simiyu wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2019 katika shule za Serikali za kutwa na bweni kwa awamu ya kwanza. Hayo yalibainishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini Desemba 14, 2019 wakati akitoa taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi wa Kidato cha kwanza kwa mwaka 2019 Mjini Bariadi. Sagini amesema jumla ya wanafunzi waliofaulu Mtihani wa Darasa la Saba ni 24,983 sawa na asilimia70.68 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani, ambapo amebainisha kuwa wanafunzi 12, 584 kati ya 24,983 waliofaulu hawajachaguliwa…

Soma Zaidi >>

SALUM MWALIM:OLENASHA ALIOMBE RADHI TAIFA.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)Zanzibar Salum Mwalimu amemtaka naibu waziri wa elimu William Olenasha kujitokeza na kuliomba taifa radhi kutokana na kauli yake ya kuwa mawaziri hawaendi kwenye majimbo ya wapinzani(wahuni) Mwalimu ameyasema hayo mkoani Njombe wakati akizungumza na viongozi wa chama hicho mjini Njombe. “Juzi nimeona naibu waziri mmoja bila aibu anazungumza mambo ya ajabu eti pale nilikuwa siji mlikuwa mnanialika kwasababu mbunge wenu hapa alikuwa ni CHADEMA,Olenasha atoke aliombe taifa radhi unaibu waziri sio wakwake wala sio wa baba yake ni wa watanzania…

Soma Zaidi >>