MWANASHERIA MKUU KUKATA RUFAA DHIDI YA KUACHILIWA HURU DIANE RWIGARA

Kigali, RWANDA. Mwanasheria Mkuu wa Rwanda, Jean Bosco Mutangana, ametangaza mbele ya waandishi wa habari kwamba atakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama wa Desemba 6 ulio muachilia huru mwanasiasa wa upinzani na mkosoaji mkubwa wa Rais Paul Kagame, Diane Rwigara na mama yake. Watuhumiwa hao wawili walikuwa wanakabiliwa na kifungo cha miaka 22 kwa makosa ya kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi pamoja na kughushi nyaraka. “Upande wa Mashitaka hauridhishwi na uamuzi wa mahakama, kwahiyo tumeamua kukata rufaa katika siku zijazo. Tulisoma kwa makini uamuzi wa Mahakama Kuu…

Soma Zaidi >>

Dar es salaam. Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, imewaandikia barua wakuu wa vyuo vya ualimu, vyuo vya ufundi na maendeleo ya jamii, vyuo vikuu na vishiriki na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kuhusu matumizi sahihi ya rangi ya bendera na wimbo wa Taifa. Katika barua hiyo iliyosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii inaeleza kuwa wizara hiyo imepokea maelekezo kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, kuhusu matumizi sahihi ya vitu hivyo. Maelekezo hayo yamebainisha kuwa kumekuwa na matumizi yasiyo sahihi yanayofanywa na taasisi za Serikali katika matumizi sahihi ya…

Soma Zaidi >>

WAZIRI MKUU WA UINGEREZA THERESA MAY ANUSURIKA KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NAYE

London, UINGEREZA. Waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May, amenusurika kura ya kutokuwa na imani naye kutoka kwa wabunge wa chama chake cha Conservative, baada ya hapo jana Wabunge 200 dhidi ya 117 kupiga kura kumuunga mkono. Wabunge (117) hao ambao ni sawa na theluthi moja hawakumpigia kura Bi May kusalia kuwa kiongozi mkuu wa chama hicho na waziri mkuu, hali inayomaanisha kuwa kiongozi huyo amepoteza uungwaji mkono wa wabunge wengi ndani ya chama chake. Hatua hiyo inaashiria Bi May bado anakabiliwa na changamoto kubwa kutekeleza mpango wake kuhusu mchakato wa…

Soma Zaidi >>

CHADEMA YAIONDOA MAHAKAMANI KESI YA UCHAGUZI

Dar es salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA) kimeiondoa mahakamani kesi ya uchaguzi namba 5/2018 iliyofunguliwa Mahakama kuu kanda ya Tanga ya kupinga uchaguzi wa marudio jimbo la Korogwe vijijini. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na mkuu wa idara ya habari na mawasiliano CHADEMA,Tumaini Makene,imesema wameiondoa kesi hiyo baada ya kufanya uchambuzi wa kina ukihususha ushauri wa kitaalam kutoka kwa mwanasheria wa chama hicho. Katika kesi hiyo iliyokuwa ianze kutajwa Desemba 10, mwaka huu, aliyekuwa mgombea wa CHADEMA,ndugu Aminata Saguti alikuwa akilalamikia mchakato ulivyoendeshwa kwa kukiuka taratibu za…

Soma Zaidi >>

FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO KUTUMIKA KATIKA MIRADI YA AFYA ELIMU NA UTAWALA MKOANI NJOMBE.

Na Emily Kilagalila,Njombe. Mbunge wa jimbo la Njombe kusini kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM,Edward Mwalongo amesema fedha za mfuko wa jimbo kiasi cha shilingi milioni arobaini(40) zinaenda kuchangia miradi ya afya ,elimu na utawala jimboni humo. Akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya mfuko wa jimbo iliyofanywa kwa lengo la kukagua na kupitisha miradi itakayosaidiwa na mfuko huo,Mwalongo amesema kuwa kiasi cha shilingi milioni 40 kitatumika kununulia vifaa vya ujenzi kulingana na mahitaji ya mradi husika na vitagawiwa kwenye Kata 13 za jimbo hilo ili kuweza kuchochea na kuchangia kasi…

Soma Zaidi >>

UFARANSA YAIKABIDHI JAMHURI YA AFRIKA YA KATI SILAHA ZA KIVITA ZAIDI YA 1,400

Bangui, AFRIKA YA KATI. Serikali ya Ufaransa juma hili imekabidhi bunduki zaidi ya elfu 1,400 aina ya AK-47 kwa vyombo vya usalama vya Jamhuri ya Afrika ya Kati vinavyokabiliana na mashambulizi yanayofanywa na makundi yenye silaha. Waziri wa ulinzi wa Ufaransa, Florence Parly, alishuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika kwenye kambi ya jeshi ya M’Polo iliyoko mjini Bangui. Msaada huu wa kijeshi ni sehemu ya ahadi ya Serikali ya Ufaransa iliyoitoa mwezi Novemba jijini Paris, sambamba na euro milioni 24 kama msaada wa kibinadamu. Maelfu ya raia wa Jamhuri ya Afrika ya…

Soma Zaidi >>

IKIWA ZIMEBAKI SIKU 10 KUFANYIKA UCHAGUZI MKUU DRC, GHALA LA TUME YA UCHAGUZI LATEKETEA KWA MOTO

Kinshasa, DRC. Moja ya ghala kubwa katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kinshasa, limeteketea kwa moto, vyanzo rasmi kadhaa vimethibitishia kutokea tukio hili huku Chanzo cha moto huo hakijafahamika bado. Moto huo uliozuka katika ghala hilo usiku wa jana Jumatano kuamkia leo Alhamisi umesababisha hasara kubwa, ambapi vifaa vilivyokuwa katika ghala hilo karibia vyote vimetekea kwa moto. Tukio hilo linatokea ikiwa zimesalia siku kumi kabla ya Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 23. “Moto ulizuka karibu saa nane usiku saa za Kinshasa (sawa na saa saba saa za…

Soma Zaidi >>

JE WAJUA TIMU ILIYOMUUA MVUMBUZI WA DRONI ZA HAMAS MOHAMED ZOUARI

Tunis, TUNISIA. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tunisia imetoa ufafanuzi mpya kuhusu timu ya mauaji ya mhandisi Mohamed Zouari, mwanachama wa Brigedi za Izzuddin Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ambaye pia alikuwa mvumbuzi wa droni za wanamuqawama wa Palestina. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tunisia amewaambia waandishi wa habari kwamba kulitumika fedha nyingi sana katika operesheni ya kumuua kigaidi Bw.Mohamed Zouari. Msemaji huyo amesema kuwa mmoja wa walioshiriki kwenye operesheni hiyo ya kigaidi ni raia wa Austria anayejulikana…

Soma Zaidi >>

MAGAIDI 27 WAUAWA NA VIKOSI VYA ULINZI VYA MISRI HUKO SINAI

Cairo, MISRI. Vikosi vya ulinzi vya jeshi la Misri vimewauwa magaidi wapatao ishirini na saba (27) katika oparesheni maalumu iliyofanyika katika eneo la Sinai la Kaskazini mwa nchi hiyo. Kamanda mkuu ya vikosi vya ulinzi vya Misri jana alitangaza kuwa wanajeshi pamoja na wahandisi wa kijeshi walinasa na kuripua mabomu 344 ambayo magaidi walikuwa wameyatega ili kuwalenga askari jeshi na wale wa usalama wa nchi hiyo, na walifanikiwa kuangamiza maficho 342 ya magaidi huko kaskazini na katikati mwa eneo la Sinai. Idadi kubwa ya miripuko na silaha mbalimbali zilinaswa pia…

Soma Zaidi >>

DC TSERE AWAAPISHA KIAPO CHA KAZI WATENDAJI WOTE WILAYANI LUDEWA MKOANI NJOMBE

Ludewa,Njombe. Mkuu wa wilaya ya Ludewa ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya Mheshimiwa Andrew Tsere disemba 12,2018 amefanya kikao cha kuweka mikakati kwa watendaji wa kata na vijiji vyote pamoja na maafisa tarafa wote katika wilaya hiyo ya Ludewa Katika ukumbi wa vikao wa halmashauri ya wilaya. Mh.Tsere amefanya uamzi huo wa kuwaita maafisa hao wa kata na vijiji kwa lengo la kuhakikisha wananchi wa wilaya ya Ludewa wanapata fursa zao za haki zao kwa utaratibu mzuri kupitia usimamizi wa watendaji pamoja na uwajibikaji mzuri…

Soma Zaidi >>