MAVUNDE AKABIDHI GARI LA HUDUMA ZA MAZISHI,WANANCHI DODOMA MJINI WAMPONGEZA

Dodoma. Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Mheshimiwa Anthony Mavunde leo ametekeleza ahadi yake ya kuwapatia wananchi wa jimbo hilo gari la kuhudumia shughuli za mazishi ambalo litatumiwa na wananchi wote bila gharama yoyote. Gari hilo maalum la huduma za mazishi limekabidhiwa leo kwa wananchi wa Dodoma chini ya uratibu wa ofisi ya mbunge na ofisi ya mkuu wa wilaya Dodoma mjini ambapo mbunge Mavunde amewashukuru wamiliki wa vituo vya G.88 NJOMBE FILLING STATION(NFS)na GAPCOkwa kujitolea mafuta lita 150 kwa mwezi kama sehemu ya mchango wa uendeshaji wa gari hilo.…

Soma Zaidi >>

BUNGE SPORTS CLUB YAFANYA MAKUBWA BUJUMBURA.

  Bujumbura,Burundi. Bunge Sports Club yatikisa Bujumbura, soka yawaduwaza EALA mabao 2-0, mpira wavu ( wanawake ) wamewazabua EALA seti 3-0, wakati netball Bunge Queens yawasambaratisha Kenya magoli 52-29 Timu za Bunge Sports Club za soka, mpira wa wavu ( wanawake ) na Netball zimekuwa gumzo katika jiji la Bujumbura baada ya kushinda michezo yote mitatu iliyoshiriki leo disemba 6, 2018. Katika michezo ya tisa ya Mabunge ya Afrika Mashariki, walikuwa ni Bunge Queens walioanza kusafisha njia ya Ushindi baada ya kuwapoteza kabisa Kenya kwa kuwalaza magoli 52-29 kwenye mchezo…

Soma Zaidi >>

WAZIRI WA NISHATI DKT. KALEMANI AMETOA AGIZO HILI KWA TANESCO MTWARA.

  Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ameuagiza uongozi wa juu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuteua na kupeleka meneja atakayesimamia halmashauri ya Nanyamba wilayani Mtwara, ili pamoja na mambo mengine aharakishe zoezi la uunganishaji umeme kwa wananchi. Ametoa agizo hilo jana, Disemba 5 akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme pamoja na kuzungumza na wananchi wa Mtaa wa Kilimanjaro, waziri Kalemani alisema ukosefu wa ofisi ya TANESCO katika eneo hilo ni mojawapo ya sababu zinazochelewesha zoezi la kuwaunganishia umeme wananchi. “Najua hapa hakuna Ofisi…

Soma Zaidi >>

CHAMA KIKUU CHA UPINZANI AFRIKA KUSINI ‘DA’ KUPINGA MAREKEBISHO YA KATIBA MAHAKAMANI.

  Pretoria, AFRIKA KUSINI. Chama kikuu cha upinzani nchini Afrika Kusini cha Democratic Alliance (DA), kimetangaza kuwa kitaenda mahakamani kusimamisha pendekezo la kufanyika marekebisho ya ardhi baada ya Bunge kupasisha ripoti inayoidhinisha kufanyika marekebisho ya katiba yatakayoruhusu kutwaliwa ardhi zinazomilikiwa na wazungu waliowachache bila ya kulipwa fidia. Chama cha Democratic Alliance (DA) na baadhi ya makundi ya kutetea haki za binadamu yamekosoa vikali mpango huo wa serikali ya Pretoria yakisisitiza kuwa, utahatarisha haki ya kumiliki na kuwatia woga wawekezaji wa kigeni. Umiliki wa ardhi na mashamba ni suala nyeti sana…

Soma Zaidi >>

HAMAS YAOMBA AFRIKA KUSINI KUINGILIA KATI KUSAIDIA MAPAMBANO YA UKOMBOZI WA WAPALESTINA.

  Pretoria, AFRIKA KUSINI. Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imeiomba Afrika Kusini izidishe uungaji mkono na misaada yake kwa taifa la Palestina katika mapambano yake ya ukombozi dhidi ya utawala haramu wa Israel. Wito huo umetolewa na ujumbe wa Hamas ulioko nchini Afrika Kusini kwa shabaha ya kupata uungaji mkono zaidi wa Pretoria kwa mapambano ya ukombozi ya Palestina. Katika mazungumzo yake na Spika wa Bunge la Afrika Kusini mjini Pretoria, ujumbe wa Hamas unaoongozwa na Mahmoud al Zahhar umepongeza hatua zinazochukuliwa na bunge la nchi hiyo,…

Soma Zaidi >>

JENERALI JESHI LA MAREKANI AKIRI KUSHINDWA KUIDHIBITI TALIBAN HUKO AFGHANSTAN.

  Kabul, AFGHANSTAN. Kamanda Mkuu wa Jeshi la Marekani, upande wa Mashariki ya Kati, Luteni Jenerali Kenneth McKenzie, amekiri kuwa vita vya Afghanistan vimeishia kwenye mkwamo na kupelekea maafa makubwa ya roho za raia wa nchi hiyo, maafa ambayo hayawezi kuvumilika. Awali Bw Joseph Dunford, ambaye ni Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Marekani naye alikiri kuwa, kundi la Taliban haliwezi kushindwa wa vita vya Afghanstan na kwamba utumiaji nguvu za kijeshi kwa ajili ya kuhitimisha vita nchini humo umegonga mwamba. Baadhi ya maafisa, wabunge, shakhsia wa kisiasa na…

Soma Zaidi >>

BARAZA LA MAULAMAA LA INDONESIA LATOA WITO WA KUFUKUZWA BALOZI WA SAUDIA.

  Jakarta, INDONESIA. Baraza hilo ambayo ni taasisi kubwa zaidi ya Kiislamu nchini Indonesia limemtuhumu Osama bin Muhammad al Shuaib, balozi wa Saudi Arabia nchini humo kuwa anaingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo na kuitaka serikali ya Jakarta imfukuze haraka balozi huyo au iandae mazingira ya kuitwa nyumbani na utawala wa Aal Saud. Inaonekana kuwa wito wa Baraza la Maulamaa la Indonesia la kutaka kufukuzwa nchini humo Balozi wa Saudi Arabia lina uhusiano kwa njia moja au nyingine na mienendo mibaya ya utawala wa Saudi Arabia na waajiri wa…

Soma Zaidi >>

MRITHI WA MFALME SAUDIA ‘BIN SALMAN’ NI MBAYA ZAIDI KULIKO WATENDA JINAI.

  Washington DC, MAREKANI. Gazeti moja la Marekani la Foreign Policy limetoa changamoto kwa siasa za Marekani kuhusu Saudi Arabia na kuandika kuwa, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa nchi hiyo, Muhammad bin Salman ni mbaya zaidi kuliko watenda jinai wote Duniani. Chombo hicho cha habari kimeashiria kuwa, jitihada zote zinazofanywa na baadhi ya maafisa wa serikali ya Marekani akiwemo Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi hiyo, Mike Pompeo, za kutaka kutetea mauaji ya Jamal Khashoggi aliyekuwa mwandishi na mkosoaji wa utawala wa Saudia na kusema, matamshi yaliyotolewa na…

Soma Zaidi >>

UTAFITI WA IEP:UBAGUZI WA RANGI UMEONGEZEKA DUNIANI.

  Sydney, AUSTRALIA Taasisi moja binafsi inayoshughulika na masuala ya Uchumi na Amani (IEP) duniani, imeeleza kuwa, katika ripoti yake mpya ya mwaka huu 2018, vitendo vya ubaguzi wa rangi viliongezeka na takwimu za watu waliouawa kutokana na mashambulio ya kigaidi zimepungua katika mwaka uliopita wa 2017. Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa na taasisi (IEP) hiyo ya Institute for Economic and Peace yenye makao yake mjini Sydney, Australia, vielezo vya kimataifa kuhusu ugaidi katika mwaka 2018 vinaonyesha kuwa, maafa ya roho za watu yaliyotokana na mashambulio ya kigaidi katika…

Soma Zaidi >>

RAIS AL BASHIR KUGOMBEA TENA, KUFUATIA BUNGE LA SUDAN KUUNGA MKONO MAREKEBISHO YA SHERIA ZA UCHAGUZI.

  Kartoum, SUDAN. Kiongozi wa muda mrefu wa Sudan, Omar Hassan al Bashir anakaribia kupata idhini ya kugombea tena kiti cha Urais wa nchi hiyo, baada ya wawakilishi wa Bunge la nchi hiyo kuunga mkono pendekezo la kufanyika marekebisho ya sheria za uchaguzi. Marekebisho hayo yatakayoondoa ukomo wa muda wa urais, hivyo yatamuwezesha Rais Omar al Bashiri kugombea kiti cha rais wa Sudan baada ya kumalizika muda wake wa sasa mwaka 2020. Kwa mujibu wa katiba ya sasa ya Sudan, Al Bashir, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1989 haruhusiwi kugombea…

Soma Zaidi >>