DKT.ABBASI AMUUNGANISHA DKT. MWINUKA WA TANESCO ‘LIVE’ REDIONI KUFAFANUA MIKAKATI YA TANESCO

Dodoma. Wakati serikali ya awamu ya tano ikifanya mageuzi kuelekea Tanzania ya viwanda,mkurugenzi mtendaji wa shirika la umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, amesema kuwa shirika hilo limepanga kuzalisha megawati zaidivya 5,000 ili kuwa chachu ya Tanzania ya viwanda. Dkt. Mwinuka ameeleza mikakati hiyo jioni hii baada ya kupigiwa simu na .semaji mkuu wa serikali, Dkt. Hassan Abbasi, aliyekuwa akifanyiwa mahojiano katika kipindi maalum cha moja kwa moja (Live) na redio RASI FM ya jijini Dodoma, ambapo mtendaji huyo wa Tanesco akijibu hoja zilizoibuliwa alisema katika miaka mitatu Tanesco imetekeleza…

Soma Zaidi >>

TADB YANYANYUA HALI YA KIPATO CHA MKULIMA MDOGO NCHINI.

    Na mwandishi wetu, Karagwe Kagera Benki ya maendeleo ya kilimo nchini (TADB) imesema imejipanga kunyanyua hali kipato cha wakulima wadogo wadogo nchini kupitia ushirika wao kwa kuwapatia mikopo ya gharama nafuu ili waweze kumudu gharama za uzalishaji. Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila, wakati alipotembelea na kufanya mazungumzo na uongozi wa Chama cha Ushirika Karagwe (KDCU) mkoani Kagera ili kujionea namna mkopo uliotolewa na TADB zilivyosaidia katika ununuzi wa zao la kahawa kwa msimu ulioishia mwezi Oktoba mwaka huu. Bibi Kurwijila…

Soma Zaidi >>

TAASISI YA TULIA TRUST YATOA MSAADA WA VITABU CHUO CHA UUGUZI NA UKUNGA MAKANDANA.

  Mbeya. Taasisi ya Tulia Trust inayoongozwa na Naibu spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson hii leo imetoa msaada wa vitabu vyenye thamani zaidi ya shilingi milioni 10 kwenye chuo cha Uuguzi na Ukunga cha Makandana Tukuyu wilayani Rungwe mkoani Mbeya. Akikabidhi msaada huo meneja wa Tulia Trust Jacquecline Boaz, amesema msaada huo umetolewa baada ya kupokea maombi kutoka kwa uongozi wa chuo kutokana na uhaba wa vitabu vya kufundishia hususani vya sayansi ambavyo ni aghali na vingi hapatikani nchini. Awali baadhi ya wanachuo akiwemo,Rais…

Soma Zaidi >>

MKURUGENZI MSD APIGIWA SIMU ‘LIVE’ KUJIBU HOJA JUU YA USAMBAZAJI DAWA DODOMA

Dodoma. Serikali imesema kuwa kwa sasa hali ya upatikana wa dawa imeimarika na dawa muhimu zinapatikana kwa zaidi ya asilimia 90 katika hospitali, zahanati na vituo vya afya nchini. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Bw. Laurean Bwanakunu alipopigiwa simu na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, moja kwa moja kutoka studio za radio Nyemo FM ya jijini Dodoma, ikiwa ni muendelezo wa kuhakikisha wananchi wanapata majibu sahihi na ya haraka kutoka kwa watendaji wa serikali. Akijibu hoja hizo, Bwanakunu ameeleza kuwa upatikanaji huo wa…

Soma Zaidi >>

NAIBU WAZIRI WA MAJI AKIRI KUSUASUA KWA MIRADI YA MAJI

Na Mwandae Mchungulike,Lindi. Naibu waziri wa maji na umwagiliaji Mheshimiwa Juma Aweso amesema moja ya mpango mkakati wa upatikanaji wa maji ni kuanzishwa wakala wa maji vijijini. Akizungumza mkoani Lindi leo asubuhi kupitia kituo cha radio Mashujaa Fm,Mh.Aweso amesema moja ya kazi ya wizara yake ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji. Wizara ya maji na umwagiliaji lazima kuanzishwa kwa wakala wa maji vijijini mpango huu utasaidia endapo utasimamiwa vizuri. Aidha Aweso amekiri kususua kwa mradi wa maji wa Ng’apa uliopo mkoani Lindi kwa kusema kuwa mradi huo ulikosewa kwenye…

Soma Zaidi >>

HALMASHAURI YA RUANGWA YAMWAGA MIKOPO KWA WALEMAVU NA WANAWAKE.

Na Bakari Chijumba,Lindi. Vijana,wanawake na walemavu wilayani Ruangwa mkoani Lindi, wamewezeshwa na halmshauri kwa kupatiwa mikopo ya vikundi ili waweze kujikwamua kiuchumi. Kupitia mikutano ya hadhara iliyofanyika kwenye vijiji vitano, 04 Disemba 2018, wakati wa ziara ya mkuu wilaya kwenye kata ya Nandagala wilayani humo, wanufaika wa mikopo hiyo wameushukuru uongozi wa halmashauri na kuutaka uendeleze utaratibu huo wa kutoa mikopo kwa vikundi vingi zaidi. Saidi Omari mkazi wa kijiji cha Mmawa, amemshukuru na kumpongeza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Ruangwa, Andrew Chezue, kwa mikopo hiyo anayowapatia kupitia idara ya…

Soma Zaidi >>

DC RUANGWA ATANGAZA KIAMA KWA WANAWAKE WANAOCHEZA NUSU UCHI KWENYE SHEREHE

Na Bakari Chijumba,Lindi. Mkuu wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi,Hashim Mgandilwa, ametoa onyo kwa wanawake wote ambao wanacheza michezo isiyo na maadili kwenye jamii, ikiwemo kukaa nusu uchi katika sherehe mbalimbali zinazofanyika wilayani humo na kusema atawashughulikia ipasavyo. Mgandilwa, ametoa onyo hilo tarehe 04 Disemba 2018, alipokuwa anazungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara, wakati wa muendelezo wa ziara zake katika kata ya Nandagala, kwenye vijiji vitano vya Mmawa, Namahema A Namahema B, Nandagala A na Nandagala B “Nipeni taarifa ya mtu yoyote anaefanya hizo tabia za kukaa na kucheza…

Soma Zaidi >>

NAPE: CCM IMEVAMIWA NA WASAKA TONGE

Na Bakari Chijumba,Mtwara Wakati sakata la Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dr.Bashiru Ally na kada wa Chama hicho, Bernard Membe likiendelea kuchukua nafasi kubwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, mbunge wa Mtama Nape Nnauye ameibuka na kusema CCM imevamiwa na wasaka Tonge wenye maslahi na matumbo yao kuliko chama. Nape Nnauye ambaye ni mbuge wa Mtama, ametoa kauli hiyo baada ya kuenea kwa taarifa kuhusu madai ya kuanzishwa kwa chama kipya kitakachoitwa USAWA, ambapo Bernard Membe na Nape Nnauye wametajwa kuwa miongoni mwa watakaotimkia kwenye chama hicho kipya. Taarifa…

Soma Zaidi >>