DC GODFREY NGUPULA “HAKUNA MVUTANO HALISI KATI YA MEMBE NA DKT BASHIRU

Tabora Mkuu wa wilaya ya Nzega na mjumbe wa kamati ya Siasa ya wilaya hiyo Mheshimiwa Godfrey Ngupula amesema kuwa kwa siku kadhaa sasa kila kona ni habari ya mvutano kati ya Membe na Dkt. Bashiru. Na haswa mvutano huu unavyoongezwa chumvi na pilipili katika magazeti na mitandao ya kijamii. Nilikuwepo Nzega wakati Dr. Bashiru anatoa ufafanuzi wa kilichotokea,namnukuu “Mimi kwanza nilipoyatamka yale Geita katika maongezi yangu wala sikuwa namaanisha kumuita Membe, utaratibu wa kuitana kichama naujua na unajulikana. “ikitaka kumuita basi nitafanya hivyo kwa barua au kwa simu lakini,…

Soma Zaidi >>

KASUSURA AELEZEA SAKATA LA KUWAONDOA WAMACHINGA WA SOKO LA KIMATAIFA LA MWANJELWA.

  Na.Rashid Msita,Mbeya. Mkurugenzi wa jiji la mbeya James Kasusura achanganua sakata la wamachinga wa soko la mwanjelwa. Aiwa ofisini kwake hii leo Disemba 4,2018 Mkurugenzi wa jiji la mbeya James Kasusura ameongea na waandishi wa habari juu ya sakata la mgomo wa kuondoka wamachinga wenye vibanda wanaofanya biashara zao nje ya soko la Mwanjelwa. Amesema huu mchakato wa soko la Mwanjelwa umeanza muda mrefu kama mnavofahamu soko la mwanjelwa ni soko kubwa, soko la kimataifa ambalo limejengwa kwa gharama kubwa na serikali kupitia mkopo toka bank ya Crdb kwa…

Soma Zaidi >>

MANISPAA YA UBUNGO KUJENGA OFISI ZA KISASA

Halmashauri ya manispaa ya Ubungo imesaini mkataba wa ujenzi wa ofisi za halmashauri hiyo za kisasa na wakala wa majengo nchini (TBA). Kutoka kushoto ni meneja wa TBA Dar es salaam Edwin Godfrey (katikati) meya wa manispaa ya Ubungo Boniface Jacob na kulia ni mkurugenzi manispaa ya Ubungo Beatrice Kwai wakisaini mkataba wa ujenzi wa ofisi za kisasa za manispaa hiyo. Ujenzi huo wa ofisi za kisasa ambao utagharimu jumla ya shilingi bilioni 6.2 utachukua muda wa mwaka mmoja hadi kukamilika kulingana na mkataba waliosaini leo kati ya manispaa ya…

Soma Zaidi >>

LEGAL SERVICE FACILITY (LSF) YAZINDUA KAMPENI MKOMBOZI KWA WANAWAKE NA MAKUNDI MBALIMBALI

Shirika lisilo la kiserikali la Legal Service Facility (LSF) linalofanya kazi ya kukuza upatikanaji wa haki kwa wote hasa kwa wanawake limezindua kampeni kwa jina la ‘Siyo tatizo tena’ yenye lengo la la kuongeza ufahamu kwa jamii kuhusu upatikanaji wa huduma za kisheria. Mkurugenzi mtendaji wa Legal Service Facility  (LSF) Kees Groenendijk akizungumza na waandishi wa habari juu ya kampeni ya ‘Siyo tatizo tena’ kwenye ofisi zao. Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi zao zilizopo Mikocheni B mkurugenzi mtendaji wa LSF Kees Groenendijk amesema lengo kuu la kampeni ya…

Soma Zaidi >>

WAZIRI DKT.KIGWANGALLA APASUA ANGA, ANADI VIVUTIO VYA UTALII NA UTAMADUNI VYA TANZANIA NCHINI UTURUKI

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla (MB) ameongoza ujumbe maalum wa Tanzania kwenye mkutano wa tatu wa Dunia wa Utalii na Utamaduni, ambao ni mkutano wa juu zaidi wa sera za utalii unaofanyika kila mwaka. Katika mkutano huo wa siku tatu, Desemba 3-5, 2018,umeandaliwa kwa pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa ya likiwemo Shirika linalosimamia Utalii (UNWTO) na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambapo Mawaziri na watunga sera zaidi ya 300 wanakutana jijini Istanbul, Uturuki, kuzungumzia mambo mbali mbali yanayohusu utalii wa utamaduni. Waziri Dkt.…

Soma Zaidi >>

TRUMP AENDELEZA MSIMAMO WAKE DHIDI YA MPAKA WA MEXICO, AIOMBA CONGRESS IMRUHUSU KUJENGA UKUTA.

  Washington DC, MAREKANI. Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa nchi hiyo itatumia mabilioni ya dola kwa ajili ya kujenga ukuta katika mipaka ya nchi hiyo na Mexico iwapo Wademocrat katika kongresi ya nchi hiyo wataafiki bajeti ya ujenzi huo. Trump alituma ujumbe huo jana Jumatatu katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter akikariri msimamo wake wa kibaguzi wa kupinga wahajiri. “Kivyovyote vile wahajiri hawataruhusiwa kuvuka mipaka na kuingia Marekani kinyume cha sheria; na iwapo italazimika Marekani itafunga mipaka yake yote ya kusini.” Rais Trump aliandika hivyo…

Soma Zaidi >>

UMOJA WA MATAIFA WAUTAKA MUUNGANO UNAOONGOZWA NA SAUDIA KUSITISHA MASHAMBULIZI YEMEN.

  New York, MAREKANI. Wakurugenzi wa taasisi zinazosimamiwa na Umoja wa Mataifa (UN), wametoa taarifa ya pamoja wakitaka kusitishwa mashambulizi ya muungano vamizi huko Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia. Wakurugenzi hao wa taasisi zilizo chini ya UN, wameashiria hatua ya muungano huo vamizi ya kutotoa ushirikiano katika juhudi za kuleta amani na mazungumzo nchini Yemen. Viongozi wamesisitiza kuwa Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amemsisitizia Muhammad bin Salman mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudia kwamba kuna udharura kwa Riyadh kuunga mkono juhudi za kuupatia ufumbuzi mgogoro wa…

Soma Zaidi >>

MIAKA 10 MRADI WA MAJI HAUJAKAMILIKA HALMASHAURI YA ILEMELA LAWAMANI.

    Na Dinna Maningo,Mwanza. Baadhi ya Wenyeviti wa Mitaa kata ya Nyamongolo wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza wameituhumu Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kwa kushindwa kutekeleza ahadi ya ukamilishaji wa mradi wa maji Nyamadoke  iliyoahidi mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge.   Imeelezwa kuwa  Agost,21,2017 Kiongozi wa mbio za Mwenge Amour Hamad wakati akiweka Jiwe la msingi kwenye mradi huo ,Halmashauri iliahidi mbele ya kiongozi  huyo kuwa ifikapo Juni,2018 mradi utakuwa umekamilika na wanachi watapata huduma ya maji lakini hadi sasa hautoi maji huku wananchi wakishindwa kufahamu sababu ya mradi kutokamilika.…

Soma Zaidi >>

HUMAN RIGHTS WATCH WAIAMKIA MAREKANI, WAIKOSOA DHIDI YA VITISHO VYAKE KWA MAHAKAMA YA ICC.

  New York, MAREKANI. Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch (HRW), Kenneth Roth, amekosoa vitisho vya Marekani dhidi ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) na kusisitizia ulazima wa kukabiliana na vitisho hivyo. Bw Roth jana alisema kuwa Marekani inaitishia mahakama hiyo kwa kuhofia uchunguzi utakaofanywa na mahakama ya ICC kuhusu kuteswa raia wa Afghanistan na wanajeshi wa Marekani na jinai za kivita zinazofanywa na Israel dhidi ya raia wa Palestina. Mkuu huyo wa Human Right Watch, ameongeza kuwa mahakama ya ICC haitalegeza msimamo…

Soma Zaidi >>

RADI YAUA MKAZI MMOJA MKOANI LINDI

  Na Mwandae Mchungulike,Lindi Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Salima Ali Kolela (45) amefariki dunia jana desemba 3 baada ya kupigwa na radi akiwa nyumbani kwake katika kijiji cha Mbuli kata ya Kichonda wilayani Liwale mkoa Lindi. Jabili Mpako ambaye mume wa marehemu amesimulia jinsi tukio lilivyotokea amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 10 jioni wakati yeye anatengeza msala mara baada ya mvua kunyesha waliingia ndani aliporudi tena mlangoni mke wake ambaye marehemu alikuwa amembeba mtoto ndipo radi ilipompiga na kumtupa nje na kuanguka na kupoteza fahamu.…

Soma Zaidi >>