SERIKALI YAOMBWA KUWEKA JICHO LA PEKEE KUNUSURU ZAO LA NGOZI

Umoja wa Wataalam Wasaidizi Tanzania (TAVEPA), umeiomba Serikali kuweka mkakati wa makusudi wa kunusuru zao la ngozi kwa kuwa sasa hivi hakuna soko la uhakika la zao hilo. Mwenyekiti wa (TAVEPA) Bw. Salim Msellem, alisema hayo leo (03.12.2018) Jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 14 wa wataalam wasaidizi wa afya ya mifugo nchini. “Ngozi nyingi hutupwa, kitu ambacho kinaletea hasara taifa kwa kukosa fedha za kigeni, pia kudhoofisha uchumi wa mfanyabiashara mmoja mmoja wa ngozi hapa nchini,” alisema Bw. Msellem. Alisema pia lazima kuwe na mkakati wa dhati…

Soma Zaidi >>

ACT WAZALENDO WAIBUA MAPYA SAKATA LA KIKOKOTOO KIPYA CHA MAFAO.

  Sakata la kikokotoo kipya cha mafao limeendelea kuchukua sura mpya baada ya Chama cha ACT Wazalendo kuitaka serikali kurudisha kikokotoo cha zamani. Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Yeremia Maganja alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya chama hicho Kijitonyama na kuitaka serikali kutumia kanuni ya kikokotoo cha mafao ya zamani ili wastaafu waweze kujikimu kimaisha na kupata mikopo kupitia akiba ya mafao yao. “Kuyapunguza mafao yao ya mkupuo mpaka asilimia 25 ni kuwaondolea haki hii ya kuweza kuwa na mikopo ya…

Soma Zaidi >>

ACT WAZALENDO WAIBUA MAPYA SAKATA LA KIKOKOTOO KIPYA CHA MAFAO

Sakata la kikokotoo kipya cha mafao limeendelea kuchukua sura mpya baada ya Chama cha ACT Wazalendo kuitaka serikali kurudisha kikokotoo cha zamani. Hayo yamesemwa leo wakati mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Yeremia Maganja alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya chama hicho Kijitonyama na kuitaka serikali kutumia kanuni ya kikokotoo cha mafao ya zamani ili wastaafu waweze kujikimu kimaisha na kupata mikopo kupitia akiba ya mafao yao. “Kuyapunguza mafao yao ya mkupuo mpaka asilimia 25 ni kuwaondolea haki hii ya kuweza kuwa na mikopo ya nyumba,…

Soma Zaidi >>

BENKI YA DUNIA YAAHIDI BILIONI 200 KATIKA SUALA LA MABADILIKO TABIA NCHI.

  Kutoka Poland. Benki ya Dunia (WB) imeahidi kiasi cha Dola bilioni mia mbili, kusaidia uwekezaji kwenye suala la mabadiliko ya hali ya hewa kwa mwaka 2021-2025, na kuongeza kiasi hiki kwa mara mbili ya fedha zake za sasa za ufadhili wa miaka mitano. Nchi zilizoendelea zimeahidi kutoa dola bilioni 100 kwa mwaka ifikapo mwaka 2020 ili kufadhili sera za hali ya hewa katika nchi zinazoendelea. Lakini hata kama kiwango kimeongezwa,kwa mujibu wa OECD (Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo), nchi za Kusini zinaomba ahadi zilizo wazi kutoka Kaskazini.…

Soma Zaidi >>

BURUNDI YAKOSOA MSIMAMO WA UMOJA WA AFRIKA KUFUATIA WARANTI YA KUMKAMATA BUYOYA.

  Bujumbura, BURUNDI. Serikali ya Burundi imeshutumu Umoja wa Afrika (AU) kwa msimamo wake, kufuatia waranti wa kumkamata Rais wa zamani wa Burundi, Pierre Buyoya, baada ya kumshtumu kwamba alihusika kwa mauaji ya aliyekuwa Rais wa kwanza kutoka Kabila la Wahutu, Melchior Ndadaye, aliyechaguliwa kidemokrasia mwaka 1993. AU imeionya Burundi dhidi ya hatua zinazoweza kuhujumu mchakato wa amani baada ya kutolewa waranti wa kimataifa wa kumkamata rais wa zamani Pierre Buyoya na maafisa wengine 16. Hivi karibuni Bw Buyoya alipinga vikali madai kuwa alihusika kwenye kifo cha Bw Ndadaye. Buyoya…

Soma Zaidi >>

WAZIRI MHAGAMA AAGIZA UONGOZI WA NSSF KUWA NA UZALENDO KATIKA UTENDAJI.

  Na mwandishi wetu Dar, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Waziri Mhagama ameuagiza uongozi wa Shiriki la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kubadili mitazamo dhaifu ya kiutendaji na kuanza kufanya kazi kwa kuongozwa na uzalendo ili kuleta tija na kufikia malengo ya Shirika hilo. Ametoa kauli hiyo mapema mwishoni mwa wiki hii (Novemba 29, 2018) alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi inayoratibiwa na shirika hilo ikiwemo ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu Dar es…

Soma Zaidi >>

DC KILOLO ,AAGIZA WADAIWA SUGU MAZOMBE SACCOS LTD KUBANWA ….

  Na Francis Godwin,Kilolo MKUU wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Asia Abdalah ameagiza wadaiwa sugu katika chama cha ushirika cha kuweka na kukopa cha Mazombe Saccos Ltd Ilula kuitwa mbele ya kamati ya ulinzi na usalama wilaya ili kueleza watakavyorejesha mikopo yao kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria. Mkuu huyo wa wilaya ametoa agizo hilo leo mjini Ilula wakati akifungua mkutano wa mwaka wa wanachama wa Mazombe Saccos ltd . Amesema dhamila ya serikali ya awamu ya tano inayoomgozwa na Rais Dkt John Magufuli ni kuendelea kuweka misingi imara…

Soma Zaidi >>

WAZIRI MKUU AFUNGUA MAFUNZO KWA WAKUU WA MIKOA NA MAKATIBU TAWALA

Na Bakari Chijumba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefungua mafunzo kwa wakuu wa mikoa na Makatibu Tawala wa mikoa, ambapo amesema baada ya mafunzo hayo serikali inatarajia watasimamia kikamilifu nidhamu katika utumishi wa umma na wao wenyewe watakuwa kioo katika kuzingatia miiko ya utumishi wa umma. Waziri Mkuu amesema anaamini baada ya mafunzo viongozi hao wa mikoa watazingatia kikamilifu mipaka ya madaraka yao na kwamba hatua watakazozichukua katika uongozi na utendaji wao zitazingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo nchini. Waziri Mkuu amefungua mafunzo hayo yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi leo (Jumatatu,…

Soma Zaidi >>

TIMU YA UHAKIKI WA WAKULIMA WA KOROSHO YAONGEZEKA, BILLION 35 TAYARI ZIMESHALIPWA.

  Na Bakari Chijumba, Mtwara Timu ya wataalamu wa Uhakiki wa wakulima wa Korosho imeongezeka katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma kutoka timu 11 mpaka kufikia timu 20 ili kuongeza uharaka wa uhakiki kwa ajili ya malipo ya wakulima. Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga ameyasema hayo tarehe 3 Disemba 2018, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Bodi ya korosho Tanzania (CBT), Mkoani Mtwara kutoa ufafanuzi juu hali ya ununuzi wa korosho. Katika mkutano huo pia Waziri Hasunga amesema kuwa timu ya wataalamu tayari…

Soma Zaidi >>

VITENDO VYA UKATILI TISHIO WILAYA YA ILALA.

Na Mwandishi wetu Ilala. MKUU wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema ameagiza ukatili wa kingono katika wilaya ya Ilala wanaofanyiwa wamama,watoto wanaobakwa na wababa kuingiliwa kinyume cha maumbile vikomeshwe. Sophia Mjema ametoa agizo hilo mwishoni mwa wiki katika uzinduzi wa kampeni za siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na Watoto. “Kumekuwepo vitendo vya ukatili wa kingono, wamama wanabakwa, watoto wanabakwa na wababa kuingiliwa kinyume cha maumbile. Pia kukosekana kwa uaminifu kwa wanandoa kufanyiwa ngono bila kinga,kushikwa sehemu za Siri bila kinga, kushikwa sehemu za mwili bila makubaliano ukatili wa…

Soma Zaidi >>