DKT BASHIRU ATAKA WASALITI WALIOADHIBIWA CCM KUTUBU,AMPONGEZA ZITTO KABWE AFICHUA SIRI YA KOROSHO….

  NA FRANCIS GODWIN,IRINGA KATIBU mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) Dkt Bashiru Ally ametoa wito kwa viongozi na wanachama  ambao walikuwa wanatumikia adhabu zao na baadhi yao kufukuzwa nafasi za uongozi na uanachama kutokana na kuendekeza makundi wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2015 kuomba msahama kwa chama . “Nataka kutumia dhahara hii leo ya kikao hiki kuwataka wale wote ambao walisimamishwa nafasi zao na kuvuliwa uanachamaa ndani ya chama chetu kuandika barua za kuomba msamaha tutawasamehe maana chama hiki ni chetu sote tunatambua kutokana na Yule waliyemtegemea kuondolewa kugombea…

Soma Zaidi >>

MASWALI NA MAJIBU YA NAIBU WAZIRI MHE. ANGELINE MABULA KWENYE KUNDI LA TANZANIA YETU LA WHATSAPP

  Na Dinna Maningo. Baadhi ya Watanzania wamekuwa wakijiuliza maswali mengi juu ya maswala mbalimbali yanayofanywa na Serikali pamoja na changamoto kadhaa ndani ya jamii lakini maswali yao hukosa majibu kwakuwa hushindwa namna wanavyoweza kufikisha ujumbe kwa mamlaka husika. Pia wengine utamani maswali hayo yangejibiwa na Viongozi wa Serikali wakiwemo Mawaziri wa Wizara mbalimbali lakini kutokana na mazingira ya kuwawezesha kuonana ana kwa ana na viongozi hao wanashindwa kufikisha kero zao ili zitatuliwe. Kwa kutambua umuhimu wa uhuru wa mawazo kundi laTanzania Yetu kupitia mtandao wa Kijamii wa Whassap lililoanzishwa…

Soma Zaidi >>

WAVUVI WAMETAKIWA KUJIUNGA KWENYE VYAMA VYA USHIRIKA.

Tanga. Wataalamu wa Dawati la Sekta Binafsi lililo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, wamewashauri wavuvi kujiunga na vyama vya ushirika ili waweze kupata mikopo itakayoboresha shughuli zao na kuwa zenye tija zaidi. Wataalamu hao wametoa ushauri huo leo wakiwa katika eneo la kushushia samaki baada ya kuvua kwenye eneo la kina kirefu cha Bahari ya Hindi Mkoani Tanga, ambapo wamebainisha wavuvi wengi wanakabiliwa na changamoto ya mitaji midogo, hivyo kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) wanaweza kupata mikopo yenye masharti na riba nafuu. Akizungumza kwa niaba ya…

Soma Zaidi >>

MGOMO WA MADEREVA BUKOBA, ABIRIA WAKOSA UTETEZI.

  Na Allawi Kaboyo Bukoba, Abiria waliopaswa kusafiri leo Novemba 27, 2018 kutoka manispaa ya Bukoba kwenda katika wilaya mbalimbali mkoani Kagera wameshindwa kusafiri, kutokana na madereva kugoma wakipinga kupandishiwa ushuru katika kituo kikuu cha mabasi. Wakizungumzia mgomo huo baadhi ya madereva akiwamo Paskates Paschale walisema kuwa hawakubaliani na hatua hiyo maana hakuna kilichoboreshwa katika kituo hicho ambacho hakina vyoo, hakina nyumba ya kupumzikia abiria na kimejaa vumbi, hali inayowasababishia adha kubwa hasa pindi mvua zinaponyesha. “Angalia stand inavyofanana, walichokifanya wamebeba vifusi vya udongo wametujazia eti wametengeneza, mvua ikinyesha hapaingiliki,…

Soma Zaidi >>

DKT.NDUGULILE ATAKA ONGEZEKO LA MAPATO LIENDE SAMBAMBA NA UBORA WA HUDUMA, TANGA

Uongozi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Bombo kuboresha huduma za matibabu zitakazopatikana na kwa muda mfupi ili kupunguza adha ya wagonjwa kukaa muda mrefu. Ushauri huo umekuja wakati ziara ya Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine wakati wa ziara yake hospitaliji hapo. Dkt.Ndugulile alibaini uwepo wa ida di kubwa ya wagonjwa wanaosubiri huduma huku ka si ya madaktari wanaotoa huduma hiyo kwa wagonjwa ukiwa ni Mdogo Hal i inayopelekea usumbufu Mkubwa wanaofika hospitaliji hapo kusubiri kwa muda mrefu. “Ninaona f ursa ya hospitali hii kukusanya…

Soma Zaidi >>

RAIS MAGUFULI AFUNGUA RASMI MAKTABA MPYA NA YA KISASA UDSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 27 Novemba, 2018 amefungua maktaba mpya, kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam iliyojengwa katika Kampasi Mlimani (Mwl. Julius K. Nyerere) Jijini Dar es Salaam. Maktaba hiyo kubwa Afrika Mashariki na Kati imejengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 93.6 ikiwa ni msaada kutoka Serikali ya China na inakuwa maktaba kubwa kuliko maktaba zote ambazo China imezijenga barani Afrika. Katika taarifa yake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. William…

Soma Zaidi >>