MKURUGENZI ILALA AWATAKA WENYEVITI,WATENDAJI KUSIMAMIA MIKOPO.

  Na Heri Shaban. Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri awataka Wenyeviti wa Serikali ya Mitaa wa Manispaa ya Ilala na Watendaji wa Mitaa kusimamia mikopo ya serikali iweze kufika kwa walengwa . Mkurugenzi wa Ilala aliyasema hayo Dar es Salaam leo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya utaratibu mpya wa utoaji mikopo kwa wanawake ,Vijana na watu wenye Ulemavu . Shauri alisema mikopo hiyo inatolewa na Serikali aina riba kwa wanawake ,vijana na watu wenye Ulemavu ili iweze kuwafikia wananchi kama ilivyokusudiwa na atakayepitisha majina yake kwa udanganyifu…

Soma Zaidi >>

SHEKIMWERI AVITAKA VIKUNDI VYA SANAA KUENDELEZA UTAMADUNI WA TANZANIA

Na Stephen Noel,Darmpya Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jijini Dodoma, Jabir Shekimweri amevitaka vikundi vyote vya sanaa za kiutamaduni wilayani humo kuweza kuenzi na kuendeleza utamaduni wa makabila yaliopo katika wilaya hiyo. Ameyasema hayo mapema leo, Wilayani Mpwapwa katika jafla ya kukabithi vyeti vya usajili wa vikundi saba vya sanaa za kitamaduni katika ukumbi wa ofisi yake. Shekimweri amesema kufuatia agizo la Waziri wa Habari sanaa na michezo Dkt, Harison Mwakyembe kuzitaka wilaya zote kuvitambua na kuvisajili vikundi vyote vya sanaa wameamu kuvirasimisha kwa lengo la kuweza kufahamika na Baraza…

Soma Zaidi >>

HUU NDIYO MSHAHARA MPYA WA N’ GOLO KANTE.

  Na Shabani Rapwi, Dar es Salaam Kiungo wa klabu ya Chelsea FC, N’golo Kante (27) leo Novemba 23 amesaini kandarasi mpya ya miaka mitano ya kuitumikia klabu hiyo. Kante sasa atakuwa akipokea mshahara wa pauni 290, 000 kwa wiki, sawa na Tsh Milioni 856 za Kitanzania ambapo awali alikuwa akipokea pauni 150,000. Mara baada ya kusaini kandarasi hiyo mpya Kante amefunguka na kusema. “Nina furaha sana kuongeza muda wangu wa kubaki Chelsea, imekuwa miaka miwili mizuri sana na natamani mingine zaidi” alisema “Tangu nimekuja hapa nimeboresha zaidi kiwango changu…

Soma Zaidi >>

UTURUKI YAONESHA NIA YA KUWEKEZA KATIKA KIWANDA CHA NGUO SIMIYU.

  Na Stella Kalinga, Simiyu Wafanyabiashara kutoka nchini Uturuki wameonesha dhamira ya kuwekeza katika ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza nguo mkoani Simiyu ambacho kitakuwa na uwezo wa kuajiri watu zaidi ya 4000. Hayo yamebainishwa katika kikao kati ya Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo ambaye aliambatana na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara wa Uturuki kutoka makampuni saba ya nchi hiyo, katika kikao maalum na viongozi wa mkoa wa Simiyu, wakuu wa taasisi mbalimbali na jumuiya ya wafanyabiashara ya mkoa wa Simiyu, kilichofanyika Novemba…

Soma Zaidi >>

SELEMANI MATOLA AMEKUWA MWIBA KWA KLABU YA SIMBA

Mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kati ya wenyeji Simba Sc dhidi ya Lipuli Fc umetamitika katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam ,huku klabu ya Lipuli fc kutokea mkoani Iringa ikifanikiwa kupata alama 1 kutoka kwa mabingwa watetezi wa ligi Kuu soka Tanzania Bara klabu ya Simba sc. Hii imekuwa sare ya tatu ambayo klabu ya Lipuli fc wameipata kutoka kwa klabu ya Simba Sc tangu wapande daraja msimu uliopita kwamaana ya michezo 3 sare 3. Mchezo wa kwanza ambao ulipigwa msimu uliopita katika dimba uhuru  ulimlizika kwa…

Soma Zaidi >>

AZAM FC YAZIDI KUNG’ARA LIGI KUU TANZANIA BARA

  Na Shabani Rapwi, Dar es salaam Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) imeendelea siku ya jana kwa michezo miwili kupigwa kwa nyakati tofauti ambapo mchezo wa awali ulikuwa kati ya Yanga SC dhidi ya Mwadui kwenye dimba la Kambarage mkoani Shinyanga. Katika mchezo huo Yanga iliibuka kidedea kwa kuichapa timu ya Mwadui FC magoli 2-1 Yanga huku magoli hayo yalifungwa na Heritie Makambo dakika ya 9 na Mrisho Ngassa dakika ya 55 na goli la Mwadui likifungwa na Salim Aiyee dakika ya 38. Mchezo mwengine ulichezwa majira ya saa 1:00…

Soma Zaidi >>

AZAM FC YASHUSHA NEEMA KWA WACHEZAJI HAWA.

  Na Shabani Rapwi, Dar es Salaam. Klabu ya Azam imekuwa na utaratibu wa kuwapongeza wachezaji wake kwa kutoa Tuzo ya mchezaji bora kwa kila mwezi ndani ya klabu hiyo. Mapema jana kabla ya kuanza kwa mchezo wa dhidi ya Ruvu Shooting, Azam FC ilitoa Tuzo sita kwa wachezaji waliofanya vizuri kwa miezi ya Agosti, Septemba na Oktoba. Tuzo tatu zikienda timu ya wakubwa Azam FC na tatu zikienda kwa timu ya vijana Azam B. Waliopata tuzo ya mchezaji bora kwa timu ya wakubwa Azam FC ni Joseph Maundi mchezaji…

Soma Zaidi >>

SHANTELL-02

Na Pastory Raymond Ilipoishia….. Angesahauje mshtuko alioupata baada ya kujigundua mjamzito baada ya Mghana huyo kumkimbia? Angesahauje jinsi alivyojaribu kuitoa mimba ya Shantell na asiweze? Na Leo anamuona akiwa amemeea kama shina la mgomba. Tunda la mwanaume pekee aliyewahi kumpenda na kuwa naye mpaka sasa akiwa na umri wa miaka Arobaini na kenda. Inaendelea…. Mwanamke huyu wa makamo aliyekuwa mbele yake aliivua miwani yake na hivyo kuyafanya macho yake yaweze kuonekana na kumpa mawazo ya kuwa siku zilizopita mama huyu alikuwa kisu kikali kilichokata mioyo ya wanaume wengi. Shantell alikuwa…

Soma Zaidi >>

WAZIRI LUKUVI ALETA FARAJA ILIYOPOTEA KWA ZAIDI MIAKA THELATHINI KWA WANANCHI WA SINGU NA ENDASAGO BABATI.

  Na Munir Shemweta, Babati Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amerejesha faraja iliyopotea kwa zaidi ya miaka 30 kwa wananchi wa Singu na Endasago wilaya ya Babati mkoa wa Manyara baada ya kusitisha kuondolewa katika mashamba yanayomilikiwa na kampuni za Agric Evolution na Endasago Co Ltd. Aidha, Lukuvi ametoa suluhu ya utata kuhusu fidia kwa wananchi waliojenga unapopita mradi mkubwa wa umeme Kilowatt 400 ambapo wamiliki wa mashamba walitaka walipwe fidia huku wananchi nao wakitaka kulipwa jambo lililokwamisha kuendelea kwa mradi. Uamuzi wa Lukuvi unafuatia…

Soma Zaidi >>