MAREKANI YAITAKA CONGO KUENDESHA UCHAGUZI WA AMANI.

  Marekani imetoa wito wa uchaguzi wa haki na wa amani katika jamhuri ya kidemokrasi ya Congo ambako kampeni rasmi za uchaguzi wa rais zimeanza leo. Wapiga kura zaidi ya milioni 40 wa nchi hiyo ya Afrika kati watamiminuka vituoni Decemba 23, kumchagua mwanasiasa atakayechukua nafasi ya rais Joseph Kabila baada ya kukaa madarakani kwa miaka 18. Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo imepata fursa ya kihistoria ya kuitisha uchaguzi wa kuaminika na wa amani na kukabidhi madaraka kwa njia za kidemokrasi. msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje…

Soma Zaidi >>

WAZIRI HASUNGA AKABIDHIWA RASMI OFISI,TIZEBA ATOA NENO.

  Na Bakari Chijumba. Aliyewahi kuwa Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Dkt. Charles Tizeba ambaye ni Mbunge wa Buchosa Mkoani Mwanza leo Novemba 22, 2018 amemkabidhi rasmi ofisi Waziri wa kilimo Mheshimiwa Japhet Hasunga (Mb). Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa mikutano maarufu kama Kilimo IV Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu mawaziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba na Mhe. Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe, na Wakuu wa idara na Vitengo. Akizungumza katika hafla hiyo fupi Mhe Dkt Tizeba amempongeza Mhe. Hasunga kwa kuteuliwa kuhudumu…

Soma Zaidi >>

WAGANGA WA TIBA ASILI 19912 WAMESAJILIWA NCHINI.

  Na. WAMJW- Dar es salaam. Jumla ya waganga wa tiba asili na tiba mbadala 19912 wamesajiliwa na Baraza la Tiba asili na Tiba mbadala nchini ili kuweza kutoa huduma hizo kwa kufuata sheria na taratibu. Hayo yamesemwa na Msajili wa Baraza la Tiba asili na Tiba mbadala nchini Dkt. Ruth Suza wakati wa semina na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa tiba asili na tiba mbadala nchini. “Pamoja na waganga wa tiba asili na tiba mbadala 19912 kusajiliwa pia tumesajili vituo vya tiba asili na tiba mbadala 19 kutoa…

Soma Zaidi >>

ESTHER BULAYA : SERIKALI INADAIWA DENI LA TRILIONI NANE

  Waziri Kivuli,Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Esther Bulaya amesema serikali inadaiwa deni la trilioni nane na mifuko ya hifadhi za jamii nchini jambo ambalo linatishia uhai wa mifuko hiyo. Bulaya amesema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya msimamo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) juu kupinga sheria mpya ya mafao ya hifadhi ya jamii na kusema serikali imekopa fedha zaidi ya shilingi trilioni nane kwenye mfuko huo na kuziwekeza kwenye miradi isiyo na tija. “Kwa mujibu wa Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali…

Soma Zaidi >>

YANGA WAANZA VYEMA MKOANI

  Mchezo wa ligi Kuu Tanzania Bara umemalizika katika dimba la  Ccm Kambarage mkoani Shinyanga na klabu ya Yanga Sc kutokea Jijini Dar es salaam kushinda 2-1. Mchezo ulianza majira ya 10:00 jioni ,Yanga walikuwa wakwanza kuandika bao kupitia mshambuliaji wao raia wa Kongo H.Makambo  dakika ya 10 ya mchezo kabla ya Salim Aiyee kuisawazishia Mwadui dakika ya 45 baada ya mlinda lango wa Yanga Claus Kindoki kufanya makosa. Mpaka  mapumziko mchezo ulimalizika kwa sare 1-1 Yanga waliingia kipindi cha pili kwa kasi ,huku wakifanya mabadiliko kadhaa alitoka mlinda lango…

Soma Zaidi >>

SIMULIZI: SHANTELL-01

Na Pastory Raymond Ilikuwa ni Jumatatu kama Jumatatu zingine. Pilika pilika zilikuwa nyingi Kama ilivyo katika miji mingi Duniani. Mwanzo wa wiki tena! Wanafunzi wanaonekana nadhifu, Kila mtu mjini anaonekana mwenye shauku ya kutekeleza adhma aliyojiwekea katika wiki mpya. Wakati wengine wakiwa wana adhma zao wengine walikuwa wana uchovu kwa kusakata rumba wikiendi na kunywa vileo mbalimbali. Huku wengine wakiilani kwanini Jumatatu ilifika mapema. Wengine wakifurahi hasa wafanya biashara ndogondogo ambao washitiri wao wengine ni wale waliopo maofisini kwani wikiendi huwa wapo majumbani mwao na hivyo kutokuambulia mia mbili mia…

Soma Zaidi >>

HIKI HAPA KIKOSI CHA YANGA LEO DHIDI YA MWADUI

Na Shabani Rapwi, Dar es Salaam. Klabu ya Yanga SC leo inashuka dimbani kukipiga dhidi ya Mwadui FC ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) kwenye uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga, Saa 10:00 Jioni. Hiki ndicho kikosi kitakacho anzaa leo kikiongozwa na golikipa, Klaus Nkinzi Kindoki 2. Paulo Godfrey Nyanganya 3. Gadiel Michael 4. Andrew Vicent 5. Abdalla Haji 6. Feisal Salum 7. Mrisho Ngassa 8. Maka Edward 9. Heritier Makambo 10. Amiss Tambwe Wachezaji wa akiba Gk. Ramadhani Kabwili Juma Abdul Cleofas Ngobanila Thabani Kamusoko Raphael Daud…

Soma Zaidi >>

MAANDALIZI YA MBEZI FUN RUN YAPAMBA MOTO, CHAMA CHA RIADHA NCHINI (RT) CHATIA NENO

Dar es Salaam. Maandalizi ya mbio za kujifurahisha za Mbezi Fun Run zilizopangwa kufanyika tarehe 1 Desemba, yamekamilka na tayari Chama cha Riadha Nchini (RT) kimetoa baraka zake. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa RT, Willihelmi Gudagudai amesema RT imetoa kibali kwa wandaaji hao baada ya kufuata taratibu zote na kwamba RT ipo tayari kuziingiza mbio hizo kwenye kalenda ya matukio ya RT. “Tumewataka baada ya tamasha lao, wawasiliane na RT ili mbio zao ziingizwe kwenye kalenda ya mwaka ya matukio ya RT.” amesema Gudagudai. Kwa upande wa waandaji hao…

Soma Zaidi >>

DC LONGIDO, ATATUA CHANGAMOTO ZILIZOPO KATIKA UJENZI WA MIRADI YA MAENDELEO.

  Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mheshimiwa Frank James Mwaisumbe leo ameendelea na ziara yake, Tarafa ya Ketumbeine na kufanya mkutano wa hadhara na wananchi kijiji cha Sokoni na kuweza kujadili mambo mbalimbali. Aidha amewaagiza wananchi wa kijiji cha Sokoni kutenga eneo na kuanza uchimbaji msingi zahanati na Serikali itaongeza nguvu baada ya juhudi za wananchi kuonekana. Hata hivyo, amewataka wakala wa barabara za mijini TARURA kuingiza kwenye mtandao wa barabara zao,barabara ya Ketumbeine hadi kijiji cha sokoni, huku akiwataka kutenga maeneo ya Utalii, na pia wapande miti ya mbao…

Soma Zaidi >>

JE YANGA WATAWEZA KUTOBOA MIKOANI?

  Baada ya kucheza takribani michezo 10 kunako dimba la Taifa jiji Dar es salaam na kushinda michezo 8 na kutoka Sare ya bao 2, leo mabingwa wa kistoria wa ligi kuu Tanzania bara, klabu ya Yanga wataanza karata yao ya kwanza nje ya jiji la Dar es salaam mkoani Shinyanga katika dimba la Ccm Kambarage dhidi ya wenyeji Mwadui Fc. Mtanange huo utapigwa majira ya saa 10 jioni kunako dimba la Kambarage,huku Yanga wakiwa na rekodi ya kutopoteza hata mchezo mmoja msimu huu wa TPL wakiwa na alama 26…

Soma Zaidi >>