MHE. SUBIRA MGALU ATAJA MAFANIKIO YA MIAKA MITATU, MRADI WA RUFIJI HYDROPOWER KUZALISHA (2100MW).

  Naibu waziri wa Nishati Mheshimiwa Subira Mgalu amesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt.John Pombe Magufuli jumla ya vijiji 3702 na wananchi 177,162 wameunganishwa kupitia miradi ya REA 11, REA 111 awamu ya kwanza, Makambako-Songea, VEI-BTIP na Densification. Mhe. Subira Mgalu amezunguma hayo akiwa wenye kongamano maalum lililoandaliwa na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) kwa ajili ya kumpongeza Rais Magufuli kwa utendaji wake mzuri ndani ya kipindi cha miaka mitatu, kongamano ambalo lilifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa PTA Sabasaba…

Soma Zaidi >>

LOWASSA ATUMIA USAFIRI WA UBER,KUUNGA MKONO JUHUDI ZA VIJANA KUJIAJIRI

Waziri mkuu wa zamani na mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Mhe. Edward Lowassa, leo Jumatatu ametumia usafiri wa Uber kuunga mkono juhudi za vijana kujiajiri. Lowassa amesema kuwa Uber pamoja na taxfy  unaweza kusadia vijana kukabiliana na tatizo la ajira iwapo kutakuwa na mipango endelevu. “Natumia usafiri huu ikiwa ni kuunga mkono vijana kujiajiri” amesema na kuongeza kama kutakuwa na mipango endelevu inaweza kusaidia tatizo hilo la ajira. “Maelfu ya vijana kila mwaka wanamaliza elimu mbalimbali na ajira hakuna usafiri huu unaweza kutumika kama njia ya kusaidia tatizo la…

Soma Zaidi >>

TIMU YA TAIFA YA TANZANIA U-23 KUWAFALIJI WATANZANIA KESHO

  Na Shabani Rapwi, Dar es salaam. Timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania chini ya Miaka 23 kesho Novemba 20 inashuka dimbani kukipiga dhidi ya Burundi U-23 kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya AFCON nchini ya Miaka 23 (QUALIFIERS OF TOTAL U-23 AFRICA CUP OF NATIONS) Saa 1:00 Usiku kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam. Ikumbukwe kwenye mchezo wa awali timu ya Taifa ya Tanzania U-23 ilikubali kichapo cha goli 2-0 nchini Burundi. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Kocha Mkuu Bakari Shime amesema…

Soma Zaidi >>

VYAMA VISIVYO NA WAWAKILISHI BUNGENI VIMEMTAKA MSAJILI WA VYAMA KUWAPATIA MUSWADA WA SHERIA NAMBA 5.

  Dar es Salaam Siku chache mara baada ya kusomwa bungeni kwa muswada wa sheria namba 5 ya mabadiliko ya vyama vya siasa nchini Tanzania ambao umelenga kuboresha mazingira ya vyama vya siasa, leo vyama visivyo na wawakilishi bungeni vimeibuka na kumtaka msajili wa vyama vya siasa nchini kuwapatia muswada huo ili waweze kuujadili na kutoa maoni yao. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha DP, Abdul Mluya amesema kuwa, ameshangazwa sana na taarifa zinazotolewa na wanasisa kwenye mitando ya kijmii wakidai…

Soma Zaidi >>

JUMLA YA WANANCHI 534 WALIOUZA KOROSHO WAMELIPWA.

  Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma Mheshimiwa Juma Homera amesema mpaka sasa Serikali imelipa wananchi 534 ambao wameuza korosho kwa msimu wa 2018/2019. Aidha amesema jumla ya fedha zilizolipwa na Serikali mpaka sasa ni Tsh 550,740,300/= kwa vyama viwili ambavyo ni Chamana Amcos, na Mtetesi Amcos na Amcos nyingine 6 ambapo utaratibu wa uhakiki unaendelea ili waweze kulipwa. “Mpaka sasa vyama viwili vilivyolipwa ni kwa jumla ya Kg 1,668,9100 na zote zimeshachukuliwa na magari 6 ya jeshi yenye uwezo wa kubeba tani 30 na zaidi na kuelekea mkoani…

Soma Zaidi >>

SERIKALI YATOA TAMKO BAADA YA TAIFA STARS KUFUNGWA, AMUNIKE AOMBA RADHI MASHABIKI.

  Serikali kupitia kwa Waziri mwenye dhamana ya michezo Mhe. Harrison Mwakyembe imewataka watanzania kukubaliana na matokeo ya mchezo wa jana wa kuwania kufuzu kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika AFCON yatakayofanyika nchini Cameroon ambapo timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ilipoteza mchezo wake mhimu dhidi ya mpinzani wake timu ya taifa ya Lesotho kwa kukubali kipigo cha goli moja kwa bila katika mchezo uliofanyika mjini Maseru. Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo Waziri Harrison Mwakyembe amewasifu wachezaji kwa kucheza kwa bidii katika dakika zote…

Soma Zaidi >>