MHE. MAHUNDI AKEMEA TABIA ZA USHIRIKINA.

  Mkuu wa wilaya ya Chunya Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi leo amefanya ziara katika kata ya Sangambi Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya. Akiwa katika kijiji cha Shoga amewaambia wananchi wa kijiji hicho, waepuke imani za kishirikina, haswa tabia inayofanywa na baadhi ya waganga ‘Rambaramba’ ambao wamekuwa wakiwatapeli wananchi na kusababisha chuki miongoni mwao. Mhe. Mahundi amewaomba wananchi kutowaamini Rambaramba hao, kwani wanasababisha uvunjifu wa amani na kugombanisha jamii kwa ujumla. “Maendeleo yetu yataletwa na sisi wenyewe, hivyo tusiruhusu mtu yeyote kutufarakanisha kwa kisingizio cha kudhibiti uchawi”. amesema Mhe. Mahundi.…

Soma Zaidi >>

MADIWANI ILALA WAILALAMIKIA TARURA KUCHELEWESHA UJENZI WA BARABARA.

  Na Heri Shaaban Baraza la madiwani wa manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam,wameitupia lawama Wakala wa Barabara TARURA Manispaa ya Ilala kwa kushindwa kujenga barabara kwa wakati zilizopo ndani ya manispaa ya Ilala. Madiwani wa Ilala walitoa malalamiko hayo katika kikao baraza la halmashauri Dar es Salaam leo wakati Diwani wa kata ya Upanga Mashariki Sultan Salim akilalamikia Wakala wa Barabara TARURA katika barabara za Mtaa wa Ismani Makao Makuu Jeshi na Urambo makao Makuu ” Sisi kama madiwani wa manispaa ya Ilala atuwaelewi TARURA utendaji wao katika…

Soma Zaidi >>

Ofisi ya Takwimu yasema Mfumuko Wa Bei Wa Taifa Umepungua Kwa Asilimia 3.2.

  Ofisi ya Taifa ya Takwimu imetoa taarifa ya mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka unaoishia Oktoba, mwaka huu, umepungua hadi asilimia 3.2 kutoka 3.4 kwa mwaka unaoishia Septemba, mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Makazi na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo,amesma kuwa kupungua huko kuna maanisha kwamba kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma imepungua. Aidha Mkurugenzi huyo amesema kuwa hiyo inamanisha kuwa mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka unaoishia Oktoba mwaka huu, imepungua…

Soma Zaidi >>

CHADEMA YALAANI VIKALI KUKAMATWA WAANDISHI WA CPJ, WATOA TAMKO KWA SERIKALI.

  Chama Cha Democrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelaani vikali kukamatwa na kushikiliwa hati za kusafiri za wanaharakati wa Kamati Maalum ya Kuwalinda Wanahabari duniani, (CPJ) waliotembelea Tanzania. Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje CHADEMA, Ndg. John Mrema amesema kama chama wameshangazwa na sababu za kuwakamata wanaharakati hao zinazotolewa na idara ya Uhamiaji hapa nchini ya kwamba hati zao nchini zilikuwa kwa ajili ya matembezi na si kwa ajili ya kukutana na waandishi wa habari. “Sisi kama chama tunajiuliza ni sheria ipi imewakataza watalii…

Soma Zaidi >>

EMMANUEL OKWI WA SIMBA ACHAGULIWA MCHEZAJI BORA WA MWEZI OKTOBA (TPL) 2018/2019

MSHAMBULIAJI wa timu ya Simba ya Dar es Salaam, Emmanuel Okwi amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) msimu wa 2018/2019.  Okwi anayecheza nafasi ya ushambuliaji, alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Yahya Zayd wa Azam na Eliud Ambokile wa Mbeya City alioingia nao fainali katika uchambuzi uliofanywa Dar es Salaam wiki hii na Kamati ya Tuzo ya TPL inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kutokana na mapendekezo kutoka kwa makocha waliopo viwanja mbalimbali ambavyo ligi hiyo inachezwa msimu…

Soma Zaidi >>

KAMPUNI YA VISA WASHIRIKIANA NA HALOTEL KULETA MALIPO YA QR KWA WATUMIAJI WA HALOPESA

  Wateja milioni 1 na wakala 40,000 kupata huduma ya malipo ya Visa kupitia Halopesa. Kampuni ya Teknolojia ya malipo ya kimataifa ya VISA imetangaza ushirikiano wa mkakati na Halotel ili kuwezesha malipo ya Visa kwenye simu kwa kutuma codi ya QR kwa wateja wa Halotel nchini Tanzania. Huduma hiyo itakayotolewa mwanzoni mwa mwaka 2019 na hivyo kuwezesha wateja zaidi ya milioni moja wa HaloPesa kutumia Visa kwenye simu ili waweze kufanya malipo ya biashara kwa salama na kuweka na kutoa fedha kwa mawakala wa Visa.Mteja yoyote wa HaloPesa, ikiwa…

Soma Zaidi >>

MAKAMU WA RAIS, MHE.SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA JENGO LA BILIONI 1.8 CHUO CHA MISITU ARUSHA.

  Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameupongeza Ubalozi wa Ufalme wa Norway nchini kwa kutoa ufadhili katika Taasisi za elimu ya uhifadhi wa misitu na mazingira ili ziweze kutoa elimu bora. Ametoa pongezi hizo leo katika chuo cha Misitu, Olmotonyi jijini Arusha wakati akizindua jengo la mihadhara lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 240 na Bweni la wanafunzi wa kike lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 100 ambayo yamegharimu jumla ya shilingi za kitanzania Bilioni moja mia nane milioni mia saba na nne elfu mia sita(1,800,704,600/=). Ujenzi huo…

Soma Zaidi >>

KIASI CHA SHILINGI BILIONI 12 ZAHITAJIKA KUHAMISHA MAGEREZA IRINGA MJINI

Na Francis Godwin,Iringa KIASI  cha  shilingi  bilioni 12 zinahitajika kwa  ajili ya  kuhamisha  gereza  la Iringa mjini  ili  kupisha  upanuzi wa hospitali ya  rufaa ya  mkoa wa Iringa . Kamishina jenerali  wa  magereza  nchini  Phaustine  Kasike   hayo leo   wakati wa  ziara  yake  mkoani Iringa na  kuwa  tayari  mchakato wa  kuhamisha  gereza  hilo  umeanza  katika eneo la mlolo  nje ya  Manispaa ya  Iringa . Kasike  alisema  kuwa  hivi  sasa  maandalizi ya  ujenzi wa nyumba  za  watumishi  wa magereza  yanafanyika katika  eneo la  Mlolo  na  tayari  baadhi ya  vifaa vya  ujenzi kama …

Soma Zaidi >>

CHADEMA WATUMA SALAMU ZA POLE MSIBA WA MAMA MZAZI WA MZEE SUMAYE.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa taarifa za Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama na Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee Frederick Sumaye kupata msiba wa kufiwa na Mama yake Mzazi, Bi. Elizabeth Gisa Sumaye, aliyefariki Jumatano, Novemba 7, 2018 kijijini kwake Endasaki, Hanang, mkoani Manyara kwa ugonjwa wa moyo na mapafu. Kufuatia msiba huo, CHADEMA kupitia Katibu Mkuu wa Chama, kinatoa salaam za pole na rambirambi kwa Familia ya Mzee Sumaye, ndugu na jamaa kwa kufiwa na Mama na Bibi, akiwa ni moja ya nguzo…

Soma Zaidi >>