SERIKALI YAJIPANGA KUKABILIANA NA UCHAFUZI WA MIFUKO YA PLASTIKI

  Dar es Salaam Imeelezwa kuwa endapo hatua za haraka zisipochukuliwa katika kukabiliana na matumizi ya mifuko ya plastiki ifikapo mwaka 2050 taka hizo zitakuwa nyingi baharini kuliko samaki. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamo wa Rais Muungano na Mazingira, Balozi Joseph Sokoine katika mkutano wa wadau mbalimbali katika kupata uelewa juu ya fursa zilizopo katika viwanda mbadala. Amesema kuwa, uchaguzi wa mazingira ni mkubwa sana, kwani matumizi yameogezeka ambapo kwa mwaka nchi ya Tanzania hutumia mifuko billioni 8 hadi 10…

Soma Zaidi >>

CAF YAWEKA HADHARANI VIPENGELE 9 VYA ‘CAF AWARDS 2018’

Shirikisho la Soka Barani Afrika ( CAF ) limeweka hadharani vipengele 9 vya tuzo za ‘CAF Awards 2018’ vitakavyowaniwa mwaka huu Kwa Mashindano Mbalimbali yaliyofanyik. vipengele vilivyotajwa 1. African Player of the Year (Mchezaji Bora Afrika wa Mwaka) 2. Women’s Player of the Year (Mchezaji Bora wa mwaka kwa Wanawake Afrika) 3. Youth Player of the Year (Mchezaji Bora Kijana wa Mwaka Afrika) 4. Men’s Coach of the Year (Kocha Bora wa mwaka Afrika wa Kiume) 5. Women’s Coach of the Year (Kocha Bora wa mwaka Afrika wa kike) 6.…

Soma Zaidi >>

KMC YAMFUNGASHIA VILAGO ABDULHALIM HUMUD

  Na Shabani Rapwi, Dar es salaam Klabu ya Kinondoni Boys ‘KMC FC’ ya jijini Dar es salaam leo Novemba 6 2018 imeachana rasmi na beki wao Abdulhalim Humud baada ya kuomba kuachwa na klabu hiyo kwa makosa ya utovu wa nidhamu. Makosa hayo ni pamoja na kuacha vifaa vya michezo Dar es salaam wakati wa mchezo dhidi ya Coast Union na makosa mengine ya kuwasumbua wake na wapenzi wa wachezaji wenzake ndani ya klabu hiyo. Akizungumza na Waandishi wa habari Meneja wa klabu hiyo Ndugu Walter Harison amesema klabu…

Soma Zaidi >>

MBUNGE STANSLAUS MABULA AWEZESHA TAULO ZA KIKE KWA WASICHANA 1000 SHULE YA SEKONDARI BUHONGWA

  Nyamagana Mwanza Mbunge Jimbo la Nyamagana Mheshimiwa Stanslaus Mabula ametoa taulo za kike kwa Wanafunzi wa kike 1000 shule ya bweni Buhongwa sekondari iliyopo kata ya Buhongwa Wilayani Nyamagana. Ikiwa ni mkakati maalum wa Mbunge kumwezesha mtoto wa Kike kuhudhuria vipindi vyote vya darasani muda Wote hata siku za hedhi, kwa ushirikiano na taasisi tanzu ya First Community Organizations pamoja na Business Professional Women kwa udhamini wa wawekezaji wazawa Lulu Pads. Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Mbunge Jimbo la Nyamagana, Rais wa taasisi ya Business and Profession Women…

Soma Zaidi >>

GAMBOSI KIJIJI KILICHOSIFIKA KWA UCHAWI CHAFANYA MAPINDUZI YA MAENDELEO

  Na Dinna Maningo,Bariadi. Ukifika Kijiji cha Gambosi Kata ya Gambosi maarufu (Gamboshi)kilichopo km 50 Magharibi mwa wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu utakutana na madhari nzuri yenye kuvutia iliyo sheheni miti ya kijani ya asili. Pia kuna hewa safi na maeneo mengi yaliyowazi huku maeneo mengine zikionekana  Nyumba za wananchi,mazao ya Pamba Mpunga,Mahindi na Viazi,Njegere,Choroko na Mbaazi. Kijiji hiki kwa miaka mingi Watanzania walio wengi wamekuwa wakiwa na hofu wakiamini kukithiri kwa imani za ushirikina na uchawi jambo ambalo linaelezwa kuwa kwa sasa hakuna uchawi imebaki tu historia au hadhithi…

Soma Zaidi >>

UKOSEFU WA VITABU VYA MAPATO CHANZO CHA KUKWAMISHA MAENDELEO MPWAMPWA.

Na Stephen Noel –Mpwapwa Ukosefu wa vitabu vya kukusanyia mapato kwa ajili ya Uendelezaji wa shughuli za maendeleo Katika Halmashauri ya wilaya Mpwapwa ni kikwazo cha kukwamisha miradi mingi ya maendeleo kusuasua. Kauli Hiyo imetolewa kwa Pamoja na madiwani wa Halmashauri ya Mpwapwa hii Leo Katika Kikao cha Baraza la Madiwani mjini hapa   Akiongea Katika Kikao Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye ni makamu wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Diwani Kata ya Mpwapwa mjini Mhe, George Fuime amesema kuwa Mpwapwa yenye Kata 33 Kata zote hazina vitabu vya kukusanyia michango…

Soma Zaidi >>

WABUNGE WA CUF, CHADEMA WASUSIA VIAPO VYA WABUNGE WAPYA WA CCM

Wabunge wa Chadema na wa CUF upande wa katibu mkuu Maalim Seif wamesusia kushuhudia kiapo cha wabunge wanne wa CCM wakati wabunge hao walipokuwa wanaapishwa. Mkutano wa Bunge umeanza leo asubuhi Jumanne Novemba 6, 2018 na kuongozwa na Spika Job Ndugai. Mara baada ya kumaliza dua na wimbo wa Taifa, uliwadia wasaa wa kiapo kwa wabunge wanne waliokuwa upinzani ambao walijiuzulu na kuhamia CCM ambako waliibuka washindi. Wakati wa shughuli hiyo ya kiapo, wabunge hao wa Chadema na CUF upande wa Maalim Seif hawakuwapo bungeni. Aliyekuwa wa kwanza kuapishwa ni…

Soma Zaidi >>

ALIKIBA ATOA DONGO BAADA YA MWALIKO WA DIAMOND WASAFI FESTIVAL.

Jana Novemba 5, Diamond Platnumz alitangaza kuwa anatamani sana kumuona msanii mwenzake pia akiwa kama kaka yake kwenye muziki Alikiba awepo kwenye tamasha lake la Wasafi Festival ..video yake inapatikana DarMpyaTv Lakini baada ya Diamond kuongea hayo watu walianza kuzungumza mitandaoni na kuanza kusema Alikiba hawezi kukubali huku wengine wakisema Alikiba akubali tu, na hadi kufikia wengine kusema Alikiba atatoa jibu lake baya au la kizarau sana. Sasa bila shaka taarifa hizo zimemfikia Alikiba ambapo muimbaji huyo ameposti picha ya mchekeshaji Mr. Bean ikiwa na maneno yanayosomeka; ‘Thank you for…

Soma Zaidi >>

UVCCM DAR ES SALAAM YACHIMBUA FURSA ZA VIJANA KWA MKURUGENZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM.

  Dar es Salaam, Tanzania. Viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Ndg. Musa Kilakala jana walifanya ziara katika ofisi ya Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam. Ziara hiyo iliyokuwa na lengo kubwa la kutaka kujua juu ya mikopo inayotolewa kwa vijana na kufahamu fursa mbalimbali za vijana zinazopatikana katika ofisi hiyo ilifanyika jana Jumatatu 5, Novemba 2018. Sambamba na hilo walijadiliana na Mkurugenzi wa jiji juu ya namna bora ya kutatua changamoto zinazowakabili vijana wanaoendesha…

Soma Zaidi >>