BOOMPLAY UNIVERSAL MUSIC GROUP WATANGAZA USHIRIKIANO KATIKA USAMBAZAJI MUZIKI

Universal Music Group inakuwa kampuni ya kwanza kuingia mkataba na jukwaa linaloongoza kwa huduma ya kusikiliza na kupakua muziki barani Afrika. LAGOS NA SANTA MONICA, 5 Novemba 2018 – Boomplay, huduma ya muziki inayoongoza upande wa kusikiliza na kupakua muziki na Universal Music Group (UMG), kampuni inayoongoza katika usambazaji wa muziki ulimwenguni, leo wanatangaza kusainiwa kwa makubaliano ya kibali cha kusambaza muziki katika masoko mengi ndani ya Afrika. UMG ni kampuni ya kwanza ya muziki wa kupitisha leseni yake kwa Boomplay, ambayo inajulikana kwa huduma yake ya kusikiliza muziki barani…

Soma Zaidi >>

MBUNGE JIMBO LA NYAMAGANA ANAWATAKIA KHERI WANAFUNZI PAMOJA NA WATAHINIWA WOTE WA MITIHANI KIDATO CHA NNE

  Nyamagana Mwanza Mbunge Jimbo la Nyamagana mheahimiwa Stanislaus Mabula anawatakia kila la kheri wanafunzi wote wa kidato cha nne pamoja na watahiniwa wengine wa mitihani ya kidato cha nne walioanza kufanya mitihani yao leo tarehe 5.11.2018 hadi tarehe 25.11.2018 katika jimbo la Nyamagana pamoja na nchi nzima. “Ninamuomba Mwenyezi Mungu awakubushe yote mliyosoma na kufundishwa na walimu muda Wote mliokuwa darasani, pamoja na neema ya wepesi katika kujibu maswali yote ili tuwe na ufaharu tulioukusudia.Alisema Mheshimiwa Mabula

Soma Zaidi >>

UN KUIBADILISHA PANGANI

Mkuu wa Wilaya ya Pangani Zainab Abdallah amefanya kikao na UN Resident Coordinator (Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania) Mr.Alvaro Rodriguez. Lengo la kikao hicho Ni kuhusu ushirikiano wa kufanikisha malengo mbalimbali ya kimkakati ndani ya Wilaya ya Pangani ikiwa kipaumbele cha kwanza ni Vijana. Kupitia Umoja wa Mataifa, inalengwa kuifanya Pangani kuwa sehemu ya mpango wa 2030 Youth Strategy na hili limeridhiwa na Mr.Alvaro ikiwa na habari njema kwa wana Pangani. Aidha kikao kimehusisha mpango wa kufanya Pangani kuwa Wilaya ya Mfano katika utekelezaji wa malengo endelevu (SDG)…

Soma Zaidi >>

DC KIZIGO AUNGANA NA WWF KUWATAKA VIONGOZI KUYATANGAZA MAFANIKIO YATOKANAYO NA UHIFADHI MAZINGIRA

Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Bi. Sophia Kizigo amewataka viongozi wa jumuiya ya Jamii hifadhi ya wanyamapori ya Mbarang’andu kutangaza mafanikio ambayo wameyapata kutokana na uhifadhi wa mazingira kwa vijiji wanachama na wananchi wengine kwa ujumla. Bi Kizigo amesema hayo katika ziara iliyofanywa na watumishi wa Shirika la Uhifadhi Mazingira Duniani (WWF), Kampuni ya Kimataifa ya Ushauri wa Miundombinu (GOPA), Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW), Mamlaka ya Uhifadhi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), na Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo katika kukagua Mradi wa Uhifadhi wa ikolojia na Maendeleo wa Pori…

Soma Zaidi >>

MAGUFULI AWAKUNA VIJANA, WAJITOKEZA HADHARANI KUMPONGEZA

Vijana mbalimbali wamejitokeza kumpongeza Rais Magufuli ikiwa ametimiza miaka mitatu ya uongozi tangu achaguliwe October 2015. Kundi la vijana kutoka Mbagala la ‘Jamii mpya ya Magufuli’ likiongozwa na mwanaharakati Ally Makwiro wamejitokeza kupongeza juhudi hizo za maendeleo zinazofanywa na Rais kwa kipindi hiki kifupi alichopo madarakani tofauti na viongozi wengine waliowahi kuwa madarakani. Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mwanaharakati Ally Makwiro amewataka viongozi wengine kumuunga mkono Rais Magufuli ili kujenga taifa lenye maendeleo kwa wananchi wake. “Viongozi wa ngazi zote serikalini kuanzia mkoa hadi ngazi ya mtaa…

Soma Zaidi >>

DKT.KIGWANGALLA: “RELI YA TAZARA INAONGEZA FURSA ZA UCHUMI KUPITIA UTALII

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema kuwa kupitia reli ya TAZARA inayounganisha nchi za Zambia na Tanzania ni kielelezo cha uchumi na kimkakati ikiwemo shughuli za Utalii Nchini. Waziri Dkt. Kigwangalla amesema hayo kwa nyakati tofauti Jijini Dar es Salaam na Matambwe Mkoani Mkoani Morogoro katika eneo la kiutalii la Selous mwishoni mwa wiki wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 42 ya reli hiyo iliyojengwa na Serikali ya China. Awali akizungumza katika stesheni ya TAZARA Jijini Dar e s Salaam, Dkt. Kigwangalla amesema tukio hilo ni…

Soma Zaidi >>

JKT-TANZANIA” TUNAOMBA TFF WACHUKUE HATUA DHIDI YA MWAMUZI MBARAKA RASHID.”

Na Prakseda Mbulu, Mbeya. Uongozi wa timu ya soka inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara JKT-Tanzania imeitaka shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF,kumchukulia hatua mwamuzi aliyechezesha mchezo wao dhidi ya Simba SC,Mbaraka Rashid,kwani mechi hiyo ilikuwa na kasoro nyingi. Akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa kumbukumbu ya sokoine Jijini Mbeya,Afisa habari wa Club hiyo Jamila Mutabazi amesema kwa ujumla michezo ule uliochezewa katika uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga November 3,2018 haukuwa sawa kwani mwamuzi alionekana wazi kushindwa kutafsiri sheria za mpira wa miguu kutokana na kuyaacha makosa ya…

Soma Zaidi >>

MIAKA MITATU YA RAIS MAGUFULI INAVYOWANUFAISHA WATANZANIA

Na Mwandishi wetu Dar es Salaam Serikali ya Rais Dr John Magufuli, imeeleza mafanikio ya miaka mitatu ya mageuzi ya kimaendeleo katika taifa la Tanzania toka Rais huyo alipoingia madarakani mwaka 2015. Akizungumza na waandishi wa habari mapema hivi leo jijini Dar es Salaam msemaji mkuu wa serikali, Dk Hassan Abbas, amesema kuwa serikali imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo toka Rais Magufuli alipoingia madarakani miaka mitatu iliyopita. Msemaji mkuu wa Serikali Dk Hassan Abbas akizungumza na waandishi wa habari mapema leo juu ya mafanikio ya miaka mitatu ya Rais Magufuli.…

Soma Zaidi >>

KAMPUNI YA RUAHA FARM NI MKOMBOZI WA WAFUGAJI NYUKI IRINGA

KAMPUNI  ya  uchakataji  wa  asili  ya Ruaha farm  mkoani Iringa kupitia asali yake Ruaha  Honey  imeanza  kuwaokoa  kiuchumi  wafugaji wa  nyuki  mkoani Iringa kwa kutoa  mizinga na  kuwaunganisha na  soko la asali . “kampuni  ya Ruaha Farm  imekuja  kivingine  baada ya  kufunga mashine  za  kisasa  za  kuchakata  asali  yenye  ubora pasipo  kutumia vifaa vya  kienyeji kama moshi  na vingine “  Mkurugenzi  mtendaji wa kampuni ya Ruaha  Honey  Fuad Abri  alisema  kuwa  kampuni yake  imeendelea  kuunga mkono jitihada za  serikali  ya  awamu ya  tano  chini ya   Rais Dkt  John Magufuli ya Tanzania  ya  viwanda .  Alisema ubora wa  asali  ya kampuni ya Ruaha Honey  ni tofauti na  asali   nyingine  zinazouzwa  mitaani kwani  sifa  kubwa ya  asali  ya Ruaha honey ni asali halisi toka katika vijiji vinavyozunga hifadhi ya Ruaha national park.  Asali ya ruaha honey ni Asali bora inayozingatia usafi wa vyombo, usafi…

Soma Zaidi >>

MIMBA KATIKA UMRI MDOGO KIKWAZO CHA MAENDELEO

Mpwapwa-Dodoma Mimba katika umri mdogo ni miongoni mwa mwa sababu zinazo vivisha jitihada za kupunguza vifo vya akina mama na watoto hapa nchini . Kwa mujibu wa Muuguzi mkuu wa Hospitali ya wilaya yaMpwapwa Bi Rhobi Maro kuwa Mpwapwa ni miongoni mwa wilaya zinazo kabiliwa na tatitizo la mimba katika umri mdogo na ndoa za utotoni unaoweza kusabisha vifo kwa akina mama na watoto pindi wanapojifungua. Aidha Bi Maro alisema kuwa miongozo mbalimbali ya ya kisera na kimkakati ya serikali ya awamu ya tano imelenga kutokomeza vifo vya akina mama…

Soma Zaidi >>