UNUNUZI WA ZAO LA KOROSHO BADO NI KITENDAWILI

Umefanyika Mnada mwingine wa korosho November 4,chini ya usimamizi wa chama kikuu cha ushirika cha RUNALI katika kijiji cha Mnero Ngongo wilayani Nachingwea mkoani Lindi. Kati ya Zaidi Ya Tani Elfu tisa zilizopigwa mnada,ni Tani 50 tu zimeuzwa na wakulima wa Ruangwa,Nachingwea na Liwale kwa bei ya Tsh.3001 kwa kila Kilo. Kampuni moja ya Korosho Africa pekee imejitokeza kununua, huku mwenyekiti CBT,Mama Anna Abdallah akigusia mpango wa wabanguaji kuruhusiwa minadani ili wanunue korosho kwa bei ya juu ya mnada husika. Bado wakulima wanaendelea kulalamikia kinachoendelea kwani ni wazi siku zinakwenda…

Soma Zaidi >>

SERIKALI KUJA NA VIFURUSHI VYA BIMA YA AFYA ‘JIPIMIE ‘NA’ DUNDULIZA’

Serikali imesema ina mpango wa kuanzisha huduma ya bima ya afya ambayo itamwezesha mwananchi kujichagulia “Kifurushi” kulingana na uwezo wake. Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipokua akiongea na wafanyakazi wa kituo cha afya cha Magugu pamoja na wananchi wa kata ya Magugu iliyopo wilayani Babati katika mkoa wa Manyara, wakati alipotembelea kituo hicho cha afya. Dkt. Ndugulile amesema, kutokana na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi, serikali sasa chini ya Wizara ya Afya, imeamua kutengeneza mkakati mpya…

Soma Zaidi >>