MAOFISA WATENDAJI UBUNGO,WATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA.

Na Mwandishi wetu, Dar es salaam. Maofisa watendaji wa mitaa ya Wilaya ya Ubungo, wametoa msaada wa vyakula, mchele kg 135, sukari, mafuta ya kula, uga wa ngano, unga wa mahindi,maharage na baadhi ya vifaa vya darasani katika Kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi (Watoto wetu Tanzania). Maofisa hao wametoa msaada huo wakiwa wanaadhimisha mwaka mmoja toka walipoajiriwa na serikalika kuwa maofisa watendaji wa mitaa katika wilaya hiyo. Wakikabidhi msaada huo mbele ya mwanzilishi na Mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho,Ndugu Evans Tegete,mwenyekiti wa maandalizi ya maadhimisho…

Soma Zaidi >>

MKOA WA KAGERA WAZINDU MKAKATI WA NYUMBA KUMI BORA ZA KIUSALAMA KUKOMESHA MAUAJI UHALIFU MAGENDO NA UHAMIAJI HARAMU.

  Na: Mwandishi wetu Karagwe Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti azindua rasmi mkakati wa kuimarisha usalama katika Mkoa wa Kagera uliopewa jina la “Nyumba Kumi Bora za Kiusalama”. Mkakati huo ukilenga kuimarsha Ulinzi na Usalama wa mkoa kuanzia ngazi ya chini katika jamii kwa kila nyumba kumi kuwa na kiongozi ambaye atakuwa na jukumu la kutambua wanafamilia wanaoishi katika kila nyumba anayoiongoza. Mkuu wa Mkoa Gaguti ambaye ni Mhasisi na Mwanzilishi wa Mkakati huo wa kukomesha uhalifu, ujambazi na vitendo vya uvunjifu wa amani katika…

Soma Zaidi >>

UJIO WA MADAKTARI BINGWA MKOANI KAGERA, WENYE MATATIZO MBALIMBALI WAOMBWA KUJITOKEZA

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UJIO WA MADAKTARI BINGWA NA KLINIKI TEMBEZI KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA KAGERA KUANZIA TAREHE O5 HADI 11 NOVEMBA, 2018 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti anapenda kuwataarifu Wananchi wa Mkoa wa Kagera na nje ya Mkoa kuwa Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wameandaa Kliniki tembezi ya Madaktari Bingwa wa fani mbalimbali itakayofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa (Government) kuanzia tarehe 05 – 11 Novemba, 2018. Ikiwa…

Soma Zaidi >>

PBZ YAKABIDHI MSAADA WA MCHELE KWA AJILI YA KAMBI ZA WANAFUNZI UNGUJA

Afisa Muandamizi wa Masoko Benki ya Watu wa Zanzibar Limited Ndg. Mohammed Ismail Khamis amekabidhi msaada wa mchele kilo Elfu mbili (Tani 2) Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa kwa ajili ya Kambi ya Wanafunzi wa Skuli za Wilaya ya Kusini Unguja wanaojiandaa kwa Mitihani yao ya Taifa ya Kidatu cha Nne, inayotarajiwa kuaza wiki ijayo Tanzania kote, makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kusini Unguja Makunduchi. Mkuu wa Wilaya Kusini Unguja Mhe Idrisa Kitwana Mustafa akitowa shukrani kwa Uongozi wa PBZ,kwa msaada…

Soma Zaidi >>

MAMA SAMIA KUZINDUA KAMPENI YA KUZUIA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI YA ‘JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA’

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu anatarajiwa kuzindua kampeni ya Kitaifa ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga ijulikanayo kama ‘Jioneze, tuwavushe salama’ itakayofanyika Novemba 6, 2018, Jijini Dodoma. Tukio hilo la uzinduz huo linatarajiwa pia kuwahusisha wakuu wote wakiwemo wa Mikoa hapa nchini ambao watakuwa chachu ya kusaidia kampeni hiyo hapa nchini na kasha kushuka ngazi ya Wilaya mpaka chini. Jiongeze tuwavushe salama, ni kampeni inayotarajiwa kupunguza vifo vitonavayo na uzazi na watoto wachanga. Ambapo pia itasaidia uelewa mkubwa kwa wananchi…

Soma Zaidi >>

MAHUNDI ATOA NENO KWA MKANDARASI MRADI WA MAJI CHUNYA.

  Na, Rashid Msita, Mbeya. Mkuu wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya,Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi, ametembelea mradi wa maji uliopo eneo kitongoji cha Msasani kijiji cha kiwanja Kata ya Mbugani na kuagiza ujenzi ukamilike ndani ya muda uliopangwa. Mhe. Mahundi ametembelea mradi huo wa maji hii leo na kujionea maendeleo ya mradi huo ambao utakuwa suluhisho la kero ya maji ya miaka mingi kwa wakazi wa kata ya Mbugani. Mradi huo ulizinduliwa mwezi Septemba na Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso, na unatarajiwa kuwanufaisha wananchi wa maeneo mbalimbali ya…

Soma Zaidi >>

ACT WAZALENDO WALIAMKIA JESHI LA POLISI KUHUSU DHAMANA YA ZITTO.

ACT WAZALENDO WALIAMKIA JESHI LA POLISI KUHUSU DHAMANA YA ZITTO . Chama cha ACT wazalendo kimetoa tamko kufuatia kukamatwa na polisi kwa kiongozi wa chama hicho Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe. Kauli Hiyo imetolewa hii Leo na katibu wa Itikadi mawasiliano na uenezi wa chama hicho bwana Ado Shaibu alipokuwa akiongea na waandishi wa habari. Bwana Shaibu amesema kuwa Zitto amekamatwa Leo nyumbani kwake Dar-es-salaam kufuatia tuhuma zinazomkabili alizo zitoa siku ya October 28Mwaka huu Katika mkutano Pamoja na waandishi wa habari. Bwana Shaibu amesema siku ya mkutano huo Zitto alizungumzia…

Soma Zaidi >>

SERIKALI YA TANZANIA YAPONGEZA USAID KUPITIA MRADI WA FEED THE FUTURE KWA KUMWAGA PESA

SERIKALI  Tanzania  imepongeza nchi ya   marekani   kupitia  Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) chini ya   mradi   unaofadhiliwa na  Feed the Future Advancing Youth Tanzania  kwa  kusaidia pesa  za ruzuku  zaidi ya  shilingi bilioni 1.2 kwa makundi ya  vijana  wajasilia mali  nchini. Akitoa  pongezi  hizo  jana katika  kijiji  cha  Mgela kata ya  Kiwere  wilaya ya  Iringa mkoani Iringa  wakati  hafla ya  kukabidhi   hundi kwa makundi ya  vijana  wanaojishughulisha na shughuli za  kilimo naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Peter Mavunde alisema  kuwa  USAID  kupitia mradi  huo wa Feed The Future  Advancing Youth Tanzania  imekuwa mkombozi  mkubwa kwa  makundi ya vijana. Hivyo  alisema  kuwa vijana  nchini  wanaowajibu  wa kuchangamkia  fursa  ya  kuwekeza katika  kilimo  na  shughuli  nyingine za  kiuchumi  huku  serikali ya Tanzania  itaendelea  kuwasaidia  vijana  hao  kwa kuraslimisha   shughuli  zao kama  za  ufundi na  nyingine   ili  kuweza  kupewa fedha  za  ruzuku kwa  ajili ya  kukuza  mitaji yao. Mavunde  alisema  kuwa  lazima  vijana  kutoka  vijiweni na  kujikita katika kilimo na  shughuli nyingine za kiuchumi kama  njia ya  kujikwamua  kiuchumi  zaidi. ‘’ Nawataka…

Soma Zaidi >>

Dkt ,KALEMANI ARIDHISHWA NA KIWANDA CHA EVERWELL CABLE

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ameeleza kuridhishwa kwake na uzalishaji wa nyaya za umeme unaofanyika katika kiwanda cha Everwell Cable & Engineering kilichopo mkoani Pwani ambacho kina uwezo wa kuzalisha nyaya za urefu wa kilometa 24,000 kwa mwaka. Alieleza hayo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Pwani na Dar es Salaam ambapo alikagua uzalishaji wa nyaya katika kiwanda hicho pamoja ujenzi wa vituo vya kupoza umeme vya Dege na Kurasini. “ Kwa sasa kuna viwanda vitano vinavyozalisha nyaya za kutosha na za ukubwa mbalimbali hivyo bado nasisitiza agizo la…

Soma Zaidi >>