HASUNGA ATOA USHAURI KWA WASANII WANAOPIGA PICHA ZA UTUPU

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga  amewashauri wasanii wanaopiga picha za utupu waache kupiga picha hizo badala yake watembelee Hifadhi za Taifa ili wakapige picha na simba, twiga chui pamoja na sokwe kwa ili  waweze kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini. Pia amewataka wasanii wenye nia ya kutaka kutengeneza filamu  katika Hifadhi ya Taifa wawasaliane na Uongozi wa Hifadhi za Taifa au wawasiliane na  yeye mwenyewe moja kwa moja. Ametoa rai hiyo wakati  akifunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa…

Soma Zaidi >>

RC HAPI APOKEA TAARIFA YA UCHUNGUZI MRADI WA MAJI PAWAGA-IRINGA

Mkuu wa Mkoa wa Iringa ameagiza kuchukuliwa hatua kwa wahandisi wote waliomdanganya kuhusu taarifa za mradi wa Maji wakati akiwa kwenye ziara yake ya IRINGA MPYA tarafa ya Pawaga, huku mamlaka ya maji IRUWASA ikitakiwa kujitathmini. Hayo yamejiri baada ya kamati ya uchunguzi aliyoiunda mapema mwezi September wakati wa ziara yake kuchunguza mradi huo wa Maji uliozua sintofahamu katika usimamizi wake. Kamati hiyo iliyoundwa na wataalam kutoka vyombo mbalimbali imewasilisha taarifa yake kwa Mkuu huyo wa Mkoa ofisini kwake leo. Pamoja na mambo mengine, mradi huo wenye thamani ya bilioni…

Soma Zaidi >>

MHE. MABULA ASHIRIKI CHAKULA NA WANAFUNZI SHULE YA AWALI SOS.

Nyamagana Mwanza Mbunge Jimbo la Nyamagana Mheshimiwa Stanislaus Mabula leo ametembelea uwekezaji wa shule ya awali “Serve Our Soul Children Home Kindergarten” inayolenga kutoa elimu bora kwa watoto waishio mazingira hatarishi. Mheshimiwa Mabula akiwa shule hapo amepongeza taasisi ya SOS kwa uwekezaji mkubwa wenye dhima yakujenga Misingi imara ya elimu bora na kuondoa athari zinazoweza kutokana na mtoto kuwa katika mazingira magumu na hatarishi pamoja na kuwa na taifa lenye Wananchi tegemezi. Sanjari na hayo Mhe. Mabula ameshiriki chakula cha mchana pamoja na kula cake na Wanafunzi hao. Naye Kaimu…

Soma Zaidi >>

JESHI LA MAGEREZA:TUNAWAPA UJUZI WAFUNGWA ILI WAKITOKA WAACHE UHALIFU

Inaelezwa kuwa ni muhimu wafungwa  kujifunza shughuli za Ujasiliamali wanapokuwa wanatumikia kifungo Gerezani kwakuwa zitawasaidia kujitegemea pindi watakaporejea uraiani. Hayo yalielezwa na Mrakibu wa Jeshi la Magereza kutoka makao makuu ya Jeshi hilo Dar es Salaam  Dedan Biralo,wakati wa Maonyesho ya viwanda vidogo SIDO yanayofanyika Kitaifa viwanja vya Nyakabindi wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu. Akizungumza na Waandishi wa habari waliotembelea banda la maonyesho ya bidhaa za Magareza Biralo alisema kuwa moja ya kazi ya Magereza ni kutoa ujuzi kwa wafungwa ili wakitoka waache uhalifu lakini pia kuwajengea uwezo wa kutengeneza…

Soma Zaidi >>

WACHIMBAJI WA DOGO WAASWA KUTOKWEPA KULIPA KODI.

  Na, Danson Kaijage, DODOMA. Wachimbaki wadogo wa madini nchini wametakiwa kuacha tabia za kukwepa kodi na badala yake wawe mstari wa mbele katika ulipaji kodi kwa faida ya taifa. Hayo yalielezwa jana na rais mstaafu wa chama cha wachimbaji wadogo wa madini nchini (FEMATA) Ndg. John Bina alipokuwa akiwasilisha taarifa katika mkutano mkuu Uchaguzi wa mwaka 2018 iliofanyika jijini hapa. Ndg. Bina amesema kuwa ni jambo la aibu kwa wachimbaji wadogo ambao kwa sasa wanakadiliwa kufikia milioni 6 kukwepa kodi wakati makampuni makubwa yamekuwa yakilipa kodi mbalimbali za uchimbaji.…

Soma Zaidi >>

WAZIRI DKT.KIGWANGALLA: “SASA NAANZA SAFARI MPYA KULITUMIKIA TAIFA”

Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbao la Nzega Vijijini la Mkoani Tabora, Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema kuwa baada ya kupona kutokana na ajali iliyompata bado ataendelea kuchapa kazi kwa bidii kulitumikia Taifa. Pia Waziri huyo amewashukuru viongozi mbalimbali wa dini Nchini kwa dua na maombi yao kwa kipindi chote alichopata ajali hadi sasa kupona na kurejea tena na majukumu yake. Akizungumza katika mkutano wake wa pili uliofanyika katika Kata ya Lusu iliyopo kwenye jimbo lake hilo la Nzega Vijijini, Oktoba 28, 2018, amesema viongozi wa…

Soma Zaidi >>

WAGANGA WAFAWIDHI NCHINI WATAKIWA KUWEKA VIKAO KUJADILI VIFO VYA UZAZI

Waganga  Wafawidhi nchini wametakiwa kukaa vikao kila baada mara kwa mara ili kujadili sababu ya vifo vinavyotokea kwenye hospitali zao ili kuzifanyia kazi changamoto hizo na kurudisha taarifa Wizara ya Afya. Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasilimali watu Wizara ya Afya Dkt. Otilia Gowelle wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Waganga Wafawidhi nchini uliofanyika leo jijini Dodoma “Waganga Wafaidhi mnatakiwa kukaa vikao vya kitabibu kujadili tiba pamoja na kujadili kifo cha kila mgonjwa ili kujua changamoto iliyotokea na kuipatia ufumbuzi na kuandikia taarifa ili kuondokana  na vifo hasa…

Soma Zaidi >>

NAIBU WAZIRI NISHATI : MRADI WA PERI-URBAN KUWEZESHA MIJI ISIYO NA UMEME KUPATA UMEME

Naibu Waziri wa Nishati Mheshimiwa Subira Mgalu hapo jana alitoa taarifa mbele ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan juu ya miradi mbalimbali ya umeme iliyotekelezwa na itakayotekelezwa hapa nchini kupitia Wizara ya Nishati. Mh. Mgalu amekiri kutambua mahitaji ya umeme mkoa wa Pwani na nchi kwa ujumla ni makubwa hasa kwenye miji inayokua hususan Kibaha. Akielezea hatua za Wizara kuhusu kumaliza kabisa tatizo la umeme wilaya ya Kibaha na mkoa wa Pwani kwa ujumla, Mheshimiwa Mgalu alisema “Nilipongia madarakani, kuanzia mwaka 2016 hadi Oktoba 2017 tulikuwa tunatekeleza mradi…

Soma Zaidi >>