MBUNGE JIMBO LA NYAMAGANA AWEZESHA TAULO ZA KIKE KWA WASICHANA SHULE YA SEKONDARI MKUYUNI

  Nyamagana, Mwanza. Mbunge Jimbo la Nyamagana Mheshimiwa Stanslaus Mabula amekabidhi taulo za kike kwa wanafunzi wasichana shule ya sekondari Mkuyuni iliyopo kata ya Mkuyuni Wilayani Nyamagana. Akikabidhi msaada huo mgeni rasmi, Rais wa taasisi ya Business and Profession Women tawi la Tanzania Bi. Betila Masawe Mongella ambaye pia ni mke wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza, amesema taasisi yake ya BPW pamoja na taasisi ya First Community Organizations kwa ushirikiano wa Mbunge jimbo la Nyamagana na kwa udhamini wa wawekezaji wazawa wa Lulu Pads nchini wametoa msaada huo ikiwa…

Soma Zaidi >>

WEMA SEPETU APIGWA RUNGU NA BODI YA FILAMU,AFUNGIWA KUIGIZA

Muigizaji maarufu wa filamu Wema Sepetu amegwa rungu na Bodi ya filamu kwa kufungiwa kujihusisha na masuala ya filamu kwa muda usiojulikana mpaka pale bodi hiyo itakapojiridhisha. Maamuzi hayo yamefanyika leo baada ya Bodi ya filamu kukutana na muigizaji huyo kwenye ofisi zao zilizopo Posta mtaa wa Samora kabla ya kufanya maamuzi hayo ambapo imesema kuwa muigizaji Wema Sepetu amekiuka sheria ya filamu na michezo ya kuigizwa Na. 4 ya mwaka 1976 na kanuni zake Na. 156 za mwaka 2011 ambapo kifungu cha 27 cha kanuni za sheria hiyo kinaeleza…

Soma Zaidi >>

WAZIRI JAFFO AWATAKA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BILA KUJALI MANENEO YA WANASIASA

  WAZIRI wa ofisi ya Rais  Tawala  za mikoa na serikali za Mitaa TAMISEMI Sulemani Jaffo amewataka madaktari bigwa  hapa nchini kuwapa fursa wananchi wa pembezoni kuzipata huduma za kibigwa bila vikwazo vingi. Na amewataka viongozi wa kisiasa kuacha tabia ya kuwadhalilisha madaktari amewataka kuwaonya  kwa kufuata kanuni taratibu za kiutumishi. Waziri Jaffo ameyasema hayo jana wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma alipokuwa akizindua  huduma za clinik tembezi za madakari bigwa zilizo ratibiwa  na uongozi wa wilaya ya Mpwapwa kwa kushirikiana na chama cha madaktari  nchini (MARTI) Aidha waziri Jaffo amesema  lengo…

Soma Zaidi >>

PROGRAM YA ULGSP KUJENGA BARABARA ZA RAMI MANISPAA TABORA.

    Na Andrew Chale, Tabora Halmashauri ya Manispaa ya Tabora imependekeza barabara zitakazojengwa chini ya programu ya ULGSP kwa fedha zinazotarajiwa kupatikana mwaka wa fedha 2018/2019. Akisoma taarifa hiyo jana Oktoba 25,2018, kwenye mkutano maalum wa Baraza la Madiwani, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora Injinia Mohamme Almasi amebainisha kuwa barabara hizo kujengwa kwa kiwango cha uhakika urefu wa KM 5 za rami nene ( Asphalt Concrete) maeneo tofauti ya Manispaa hiyo. Amezitaja barabara hizo kuwa ni : barabara ya Kuya yenye urefu wa kilometa (KM) 1.7 iliyo Kata…

Soma Zaidi >>

BUNGE LASHAURIWA KUTOPITISHA MISWADA YA DHARURA

    NA DANSON KAIJAGE,DODOMA BUNGE limeshauriwa kutokubali kupokea na  kupitisha miswada ya dharura kwani kwa kufanyaya hivyo ni kusababisha kukosa muda wa kujadili miswada hiyo. Hayo yalielezwa jana na mtafiti wa foundation for Civil Society,Lulu Urio alipokuwa akitoa taarifa ya majumuhisho ya wiki ya Azaki iliyofikia kilele  jana jijini Dodoma. Alisema kuwa pamoja na mambo mengine lakini bado yapo mambo ambayo yanatakiwa kuangaliwa kwa umakini zaidi kwa lengo la kujadili mambo ya msingi kwa mstakabali wa nchi. Alisema Azaki zimekuwa  zikijishughulisha na utoaji wa elimu mbalimbali kwa jamii hivyo…

Soma Zaidi >>

VIONGOZI WAONYWA KUTOG’ANG’ANIA MADARAKA

    NA DANSON KAIJAGE,DODOMA VIONGOZI wametakiwa kujenga tabia ya kuwashirikisha wananchi shughuli wanazozifanya kwa lengo kuwafanya kuwa na imani na viongozi hao. Mbali na hilo viongozi wametakiwa kutambua kuwa ili uweze kuongoza vizuri ni lazima kuzingatia misingi ya sheria,Kanuni na taratibu za kazi na kutambua kuwa uongozi ni dhamana tu. Hayo yalielezwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mstaafu Ludovick Utto alipokua akitoa mada katika wiki ya Azaki iliyofanyika jijini Dodoma. “Mtu ambaye anakwea kwenye mti lazima atashuka chini tu, kwa hiyo hata kwa upande…

Soma Zaidi >>

BREAKING NEWS: MFANYABIASHARA MWINGINE WA KIHINDI ATEKWA TABORA

    TABORA: Mfanyabiashara mwingine mwenye asili ya Kihindi aliyefahamika kwa jina la Kishori ametekwa na watu wasiojulikana usiku wa Oktoba 25, 2018 na kisha kuondoka nae sehemu isiyojulikana. Kwa mujibu wa mashuhuda ambao wameongea na mwandishi wa mtandao wa Dar Mpya mapema leo mjini hapa, wameeleza kuwa, tukio hilo limetokea eneo la katikati ya mji wa Tabora karibu na Golden Eagle hotel eneo ambalo ni jirani na ofisi na makazi yake. Shuhuda hao wameongeza kuwa, wakati tukio hilo limetokea lilikuwa ni la ghafla na walimchukua na kisha kukimbia na…

Soma Zaidi >>

MBUNGE MATIKO ASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI TAGOTA.

    Mbunge wa Tarime mjini kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)Esther Matiko ameshiriki ujenzi wa shule mpya ya sekondari Tagota kwa kujenga darasa moja ili kuondoa kero kwa watoto kufuata elimu umbali mrefu. Hii ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa katika kampeni zake mwaka 2015 ndani ya kata ya Kenyamanyori juu ya kuanzishwa kwa shule mpya ambapo wananchi waliadhimia kuanza ujenzi mara moja. Akiwa katika ziara yake yoctober 20,2018 Mh.Matiko alipita na kujiridhisha endapo wananchi wanaendelea na ujenzi baada ya kusitishwa hapo awali ambapo mbunge huyo alifanya…

Soma Zaidi >>

RC KATAVI ALITAKA JESHI LA POLISI KUONDOA MSONGAMANO WA MAHABUSU KATIKA GEREZA LA MPANDA

    Katavi Mkuu wa mkoa wa Katavi mheshimiwa Amos Makala jana October 25, 2018 amefanya kikao na jeshi la Polisi mkoani humo na kulita Jeshi la Polisi kuimalisha juhudi katika kitengo cha upelelezi ili kuondoa msongamano wa Mahabusu katika Gereza la Mpanda. Mkuu huyo wa mkoa alisema “Gereza la Mpanda Lina uwezo wa mahabusu 100 lakini hivi sasa Gereza hilo Lina mahabusu 440. Kesi ndogondogo kama kesi za kuiba Kuku au uzururaji kwanini zichukue muda mrefu kupelelezwa?” Akihitimisha majadiliano hayo pia Mkuu wa mkoa alizungumzia juu ya kuibuka kwa…

Soma Zaidi >>

RC SINGIDA: TUNAHITAJI AFYA NJEMA KATIKA SAFARI YETU YA TANZANIA YA VIWANDA.

    Na Dinna Maningo,Bariadi. Inaelezwa kuwa Watanzania wanahitaji afya njema  ili waweze kushiriki katika uchumi wa Viwanda nakwamba Dawa za tiba asili zimekuwa zikisaidia kuimarusha afya za watu. Hayo yameelezwa na Mkuu wa mkoa wa Singida Rehema Nchimbi wakati alipotembelea maonyesho ya viwanda vidogo (SIDO) yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu. Nchimbi wakati akikagua maonyesho ya bidhaa za wajasiliamali wa dawa za tiba asili aliwahoji wajasiliamali kutaka kufahamu ni kwa namna gani dawa za tiba asili zinavyosaidia afya za Watanzania katika kuelekea uchumi wa…

Soma Zaidi >>