WAZIRI SELEMAN JAFFO AFUNGUA HUDUMA ZA MADAKTARI BINGWA MPWAMPWA

  Mpwapwa Dodoma Waziri wa TAMISEMI mheshimiwa Seleman Jaffo leo October 25 2018 amefungua huduma za madaktari Bingwa wilayani Mpwapwa jijini Dodoma Akiwa wilayani humo Waziri Jaffo amesema Jukumu la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha kuwa Mtanzania mnyonge anasogezewa huduma za afya alipo, kwa maana ndani ya miaka mitatu tumefanikiwa kuwa na vituo vya afya 307 ili Watanzania wanyonge wapate huduma za afya, Waziri Suleman Jaffo waziri wa TAMISEMI.alipokuwa akifungua huduma za madaktari Bigwa Mpwapwa. ” Kazi ya mganga ni kuweza kuokoa maisha ya binadamu hivyo kazi Hiyo…

Soma Zaidi >>

KAMPUNI YA SPORTSPESA YAMPA SHAVU BONDIA MWAKINYO

  Dar es Salaam Kampuni ya kubashiri michezo ya SportsPesa Tanzania imeingia mkataba wa miaka mitatu na Bondia wa kulipwa Hassan Mwakinyo kuwa balozi wa kampuni hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mkurugenzi wa utawala na utekelezaji wa kampuni hiyo, Tarimba Abbas amesema kampuni hiyo kudhamini michezo imekuwa ni jambo la kawaida ambapo kwa sasa wamedhamini michezo ya ngumi. “Wakati kampuni yetu ikiendelea kukua katika hatua mbalimbali za ukuaji, pia tunataka kukua na Mwakinyo na kuleta mwanga mpya kwenye mchezo huu ngumi hapa nchini ” amesema Tarimba. Amesema kuwa,…

Soma Zaidi >>

MKURUGENZI DCB ATAJA SABABU ZA UKUAJI WA BENKI HIYO

  Dar es Salaam Mkurugenzi wa Fedha Benki ya Biashara ya DCB Zacharia Kapama, amesema benki hiyo imefanikiwa kupata faida ya bilioni I.4 katika kipindi cha robo tatu ya mwaka huu. Aidha amesema kuwa mafanikio hayo yametokana na juhudi katika kuhakikisha wanatoka katika hasara ya bilioni I.6 waliyopata mwaka wa jana. Kauli hiyo, ameitoa leo jijini wakatinakizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa katika kuelekea mafanikio hayo waliweza kuboresha mfumo wa endeshaji biashara ambapo gharama za uendeshaji zilishuka pamoja na kuanzisha huduma mpya ya kidigital. “Tulizindua akaunti ya kidigitali…

Soma Zaidi >>

WALIMU WA ST.MARCUS WAZAWADIWA GARI NA PIKIPIKI KWA MATOKEO MAZURI YA DARASA LA SABA.

  Mbunge wa jimbo la Songwe na mmiliki wa shule za St. Marcus na Southern highland sekondari Mhe. Philip Mulugo leo ametoa zawadi ya gari na pikipiki kwa walimu waliofanya vizuri katika matokeo ya shule ya St. marcus (Mbeya). Mhe. Mulugo ametoa zawadi hizo hii leo katika mahafali ya kidato cha nne ya shule ya Southern highland Sekondari na kuwashukuru walimu kwa kuweza kuifanya shule ya St.Murcus kuongoza mbeya kwa kushika nafasi ya kwanza kwa wilaya na ya pili kimkoa katika matokeo ya darasa la saba. Shule ya St.Murcus imeongoza…

Soma Zaidi >>

JIJI LA DODOMA LAONGEZA UWEZO WA KUJITEGEMEA

    NA DANSON KAIJAGE,DODOMA HALMASHAURI ya jiji la Dodoma imeongeza uwezo wake wa kujitegemea kwa kutumia mapato ya ndani kutoka asilimia 9 za awali hadi kufikia asilimia 34 kwa mujibu wa taarifa ya hesabu za Fedha kwa mwaka ulioishia Juni 2018. Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin Kunambi kwenye mkutano wa wazi wa baraza la madiwani wa robo ya kwanza ya mwaka huu wa fedha. Kunambi amesema kuwa, hadi sasa jumla ya shilingi billioni 14 zimeshakusanywa na Halmashauri ya Jiji ambapo lengo lake ni kuhakikisha inakusanya…

Soma Zaidi >>

WAZIRI TIZEBA: KODI ZA TRA SI RAFIKI KWA WAFANYABIASHARA.

Na Dinna Maningo,Bariadi. Waziri wa Kilimo Charles Tizeba amesema kuwa  mbinu zinazotumiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kumtoza Kodi Mfanyabiashara baada ya miezi mitatu anapokuwa kaanzisha biashara yake si rafiki kwakuwa kwa muda huo anakuwa hajapata faida. Tizeba aliyasema hao wakati alipotembelea na kukagua mabanda ya maonyesho ya  Wajasiliamali yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi kata ya Nyakabindi mkoani Simiyu ambapo kilele chake ni Octoba,28,2018. Waziri Tizeba akimuhoji Meneja wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi Gabriel Mwangosi namna wanavyotoza kodi, alisema kuwa kitendo hicho si haki kwakuwa biashara yake inakuwa haijafahamika  kwa…

Soma Zaidi >>

MARUFUKU KULIMA MAHINDI,MTAMA NA UWELE NDANI YA JIJI

    NA DANSON KAIJAGE, DODOMA MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amepiga marufuku kulima kilimo cha mazao ya mahindi,mtama na uwele katika kata 20 ambazo zipo ndani ya Jiji. Ametoa kauli hiyo jana alipokuwa akiwasilisha mada mbalimbali katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya Dodoma kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo  Vijijini jijini hapa. Kunambi alisema kuwa kata 20 ambazo zipo ndani ya Jiji la Dodoma hazitakiwi kuendesha kilimo cha mazao marefu na badala yake mazao ambayo yanatakiwa kulimwa ni mazao ambayo ni…

Soma Zaidi >>

BENJAMIN MKAPA AAHIRISHA MAZUNGUMZO YA AMANI YA BURUNDI

    Arusha. Shughuli za ufunguzi wa mazungumzo ya amani nchini Burundi zilizokuwa zifanyike siku ya Jumatano jana jijini Arusha zililazimika kusogezwa mbele ingawaje mwezeshaji wa mazungumzo hayo Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa hakueleza sababu. Hata hivyo taarifa za ndani zimedai kuwa Mkapa ametuma ujumbe wake kwa serikali ya Rais Pierre Nkurunziza kuitaka, itume wawakilishi katika mazungumzo hayo. Awali,serikali ya Burundi iliomba kusogezwa mbele kwa mazungumzo hayo ikidai kuwa nchi hiyo iko kwenye maombolezo ya mwezi mzima wa Oktoba. Wajumbe wa upinzani waishio nje ya Burundi wanaojumuika katika…

Soma Zaidi >>

HOFU YAONGEZEKA DRC KUFUATIA IDADI YA VIFO VINAVYOTOKANA NA EBOLA KUFIKIA 159

  Kinshasa, DRC. Idadi ya watu waliopoteza maisha Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, inaendelea kuongezeka. Hadi siku ya Jumanne juzi, idadi ya watu waliopoteza maisha kufuatia ugonjwa wa Ebola ilikuwa imefikia 159, kulingana na ripoti ya tarehe 23 Oktoba 2018 ya shirika la Afya duniani (WHO) . Wiki mbili zilizopita, WHO ilionya kuwa, kuna hatari ya maambukizi hayo kuendelea kuenea iwapo visa vya maambukizi havitapungua. Mapema wiki hii Umoja wa Ulaya ulisema unatoa Euro Milioni 7.2 kusaidia mapambano dhidi…

Soma Zaidi >>

RAIS TRUMP AAHIDI KUWASHUGHULIKIA WALIOTUPA VIFAA VYA MILIPUKO KWA MARAIS WA ZAMANI

    New York, MAREKANI. Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema usalama wa taifa lake ni jambo alilolipa kipaumbele cha kwanza, matamshi anayotoa saa chache baada ya maofisa usalama kubaini vifaa vya mlipuko vilivyotumwa kwa marais wa zamani na watu mashuhuri. Jumla ya vifurushi vitano vinavyodaiwa kuwa ni mlipuko vilitumwa kwa aliyekuwa mgombea wa chama cha Democratic, Hilary Clinton, Rais wa zamani Barack Obama na ofisi za shirika la habari la CNN. Rais Trump sasa anataka wahusika kusakwa ambapo ametoa wito wa umoja na kuachana na siasa za chuki na…

Soma Zaidi >>