BEI YA ZAO LA KOROSHO BADO PASUA KICHWA MINADA YAKWAMA

  Na Bakari Chijumba, Mtwara Wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya kusini ya Lindi na Mtwara wamegoma kuuza Korosho zao kwa kile walichodai ni kuporomoka kwa bei ya zao hilo ukilinganisha na misimu iliyopita, kiasi ambacho wamesema hakuna maslahi kulinganisha na gharama zilizotumika katika kuzalisha zao hilo. Katika minada yote mitatu iliyofanyika kwa ajili ya kuanza msimu wa mauzo ya zao hilo wakulima walijikuta wakikataa kuuza korosho zao kwa kile walichodai wanunuzi walikuwa hawajafika bei ambayo ni tegemewa hivyo kupelekea minada yote mitatu kushindwa kufanikiwa. Katika Mnada wa…

Soma Zaidi >>

MBUNGE JIMBO LA NYAMAGANA KUWEZESHA KIKOSI CHA PAMBA S.C KWAAJILI YA MICHUANO YA LIGI DARAJA LA KWANZA MWANZA

  Nyamagana Mbunge jimbo la Nyamagana mheshimiwa Stanislaus Mabula leo October 24 amekabidhi Sukari, Mchele pamoja na $ 100 ambayo ni sawa shilingi Laki mbili na elfu ishirini (220,000.00) fedha za kitanzani katika kikosi cha Pamba Sport Clubs :S.C) kilichopo kambi kwaajili ya kuwakilisha wilaya ya Nyamagana katika michuano ya ligi daraja la kwanza mkoani Mwanza inayoendelea hivi sasa. Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya mheshimiwa Mabula, Mwenyekiti wa taasisi ya First Community Ndugu. Amhed Misanga kwa mwenyekiti wa Pamba Sport Clubs (S.C) aliyewakilishwa na mjumbe wa kamati Chomba Hussein…

Soma Zaidi >>

KAMISHENI YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU YAKUTANA NCHINI GAMBIA

Na Edwin Soko Banjul ..Gambia Kamisheni ya Afrika ya haki za binadamu Leo hii imeanza vikao vyake hapa mjini Banjul Gambia. Kamishina wa kamisheni hiyo Dr. Mary Maboreke alifungua rasmi kikao hicho kwa kusisitiza kuwa haki za binadamu lazima ziheshimiwe ili kulinda utu na ubinadamu wa Mwafrika . Ujumbe mzito wa Tanzania ulioongozwa na mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania (THRDC) ukijumuisha mashirika zaidi ya 15 upo mjini Banjul ukihudhuria vikao hivyo. Mkutano wa Leo ulitanguliwa na mkutano wa Afrika was Azaki ambapo ulianza Oktoba 20 had I…

Soma Zaidi >>

MAJALIWA: SERIKALI IMEJIPANGA KUSIMAMIA MAENDELEO ENDELEVU.

  Dar es Salaam Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa amewataka vijana kuchangamkia fursa mbalimbali za miradi zilizopo nchini Tanzania ili waweze kujiajiri wenyewe na kujiongezea kipato, badala ya kuchagua kazi za kufanya. Kauli hiyo ameitoa mapema Jijini Dar es Salaam kwe katika maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa (UN) ambapo Tanzania imeungana na nchi 189 duniani kwenye sherehe hiyo. Amesema kuwa, Serikali inahakikisha kuweka malengo ya maendeleo endelevu ya kidunia ikiwemo upatikanaji wa elimu, Afya pamoja na ajira kupitia fursa mbalimbali zilizopo…

Soma Zaidi >>

SOKO LA KOROSHO LAZIDI KUDORORA NCHINI.

LINDI. Hali ya bei ya zao la korosho nchini imezidi kukuanguka na kupelekea kuwakatisha tamaa wakulima wa zao hilo nchini kwani siku zinavozidi kwenda na bei ya zao hilo inaporomoka. Umefanyika mnada wa tatu wa korosho leo October, 24. wilayani Nachingwea Ukisimamiwa na Chama kikuu cha ushirika Ruangwa,Nachingwea (RUNALI) na kushuhudiwa kudorora kwa mnada huo. Idadi ya wanunuzi imezidi kuporomoka kampuni tano (5) pekee zimejitokeza leo ukilinganisha na kampuni kumi na tano (15) za mnada wa kwanza na kampuni nane (8) za mnada wa pili. Wakulima wamegoma kuuza Korosho zao…

Soma Zaidi >>

MAJALIWA :SERIKALI IMEJIPANGA KUSIMAMIA MAENDELEO ENDELEVU.

Dar es salaam Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa amewataka vijana kuchangamkia fursa mbalimbali za miradi zilizopo nchini Tanzania ili waweze kujiajiri wenyewe na kujiongezea kipato, badala ya kuchagua kazi za kufanya. Kauli hiyo ameitoa mapema leo Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa (UN) ambapo Tanzania imeungana na nchi 189 duniani kwenye sherehe hiyo. Amesema kuwa, Serikali inahakikisha kuweka malengo ya maendeleo endelevu ya kidunia ikiwemo upatikanaji wa elimu, Afya pamoja na ajira kupitia fursa mbalimbali zilizopo nchini kupitia…

Soma Zaidi >>

IDADI YA WACHANGIAJI WA MFUKO WA BIMA YA AFYA (NHIF) WAONGEZEKA

Idadi ya wanachama wachangiaji wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya imeongezeka kutoka wanachama 164,708 waliokuwa wameandikishwa  mwaka 2001/2002 hadi wanachama 873,012 mwezi Septemba 2018. Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiwasilisha  taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mfuko huo kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Bungeni jijini Dodoma. “Ongezeko hili limetokana na kanuni na misingi  inayotumika katika kuendesha utaratibu wa mfuko huu ikiwa ni pamoja na uchangiaji wenye usawa kwa kuzingatia…

Soma Zaidi >>

NENO LA KWANZA KUTOKA KWA MO KWA WANA SIMBA

Ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu mfanyabiashara maarufu hapa nchini na mmiliki wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji kupatikana kwa mara ya kwanza ametoa neno la matumaini mazuri ndani ya klabu hiyo. Kupitia akaunti yake ya twita Mo Dewji amewathibitishia mashabiki na wapenzi wa klabu ya Simba kuwa hatua za awali za ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mazoezi zimeanza hivyo Wanamsimbazi hao wategemee kuwa na uwanja wao wa mazoezi siku za usoni. >>Tumefika hatua nzuri ya maendeleo ya uwanja wetu wa mazoezi wa #SIMBA. Nafurahi kuona maono yangu yanakamilika…

Soma Zaidi >>

CUF YAMPA MAKAVU JULIUS MTATIRO NA JINSI ALIVYOTAKA KUISAMBARATISHA CUF

Na mwandishi wetu   Chama cha Wananchi (CUF) kimemtolea uvivu na kumpa makavu yake aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Bara wa chama hicho Julius Mtatiro kwa kutolea ufafanuzi baadhi ya hoja zake alizozitaja kwenye mazungumzo yake aliyofanya na wanahabari Unguja. Kupitia taarifa iliyotolewa kwa wanahabari na Abdul Kambaya, Mkurugenzi wa Habari Uenezi na Mahusiano na Umma CUF, chama hicho kimesema Mtatiro anatafuta njia ya kupata uongozi wa serikali chini ya CCM kwani ndiyo hoja yake ya msingi aliyoitoa wakati anakihama chama hicho, hivyo kuongea hoja zake zisizo na msingi na kuuponda…

Soma Zaidi >>

SERIKALI YAWEKA JUHUDI ZA KUDHIBITI MATUMIZI MABAYA YA MTANDAO

Dar es Salaam Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi na mawasiliano,Dkt, Atashasta Nditiye amesema Serikali imeweka jitihada za kuboresha na kudhibiti matumizi mabaya ya huduma ya mawasiliano kupitia mtandao. Kauli hiyo ameitoa mapema leo jijini Dar es Salaam, wakati akifungua mkutano wa pili wa mwaka wa wataalam wa Tehama ambao umelenga kujadili masuala ya habari mawasiliano na teknolojia, katika kukuza uchumi endelevu. Amesema kuwa,mkutano huo umelenga kujadili masuala manne ikiwemo kuwatambua wanatehema kwa elimu na vigezo vyao, kutengeneza chombo cha kueka heshima katika kudhibiti matumizi mabaya ya mtandao pamoja na…

Soma Zaidi >>