RC CHALAMILA AITAKA MIFUKO YA UWEZESHAJI KUFANYA KAZI KWA UWAZI NA KUEPUKA RUSHWA.

Na Prakseda Mbulu,Mbeya. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, amewataka watumishi katika mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kuepuka rushwa wakati wa utoaji huduma ili kuhakikisha wananchi wananufaika na mifuko hiyo. Mh.Chalamila amezungumza hayo leo octoba 23,2018 wakati akifunga maonesho ya mifuko ya uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii yaliyofanyika katika viwanja vya Ruanda Nzovwe Mbeya kwa nyanda za juu kusini. Chalamila amesema uwepo wa rushwa katika utoaji wa huduma kwenye mifuko hiyo ni vitendo ambacho vimekuwa vikiwanyima haki na kuwabebesha mizigo wananchi na kuwafanya wanalipa fedha nyingi ambazo…

Soma Zaidi >>

WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA GARI KUWAKA MOTO MKOANI KAGERA.

Na Allawi Kaboyo. Bukoba. Watu watatu ambao majina yao hayajatambuliwa wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa baada ya gari linalomilikiwa na wakala wa barabara nchini (Tanroads) kugongana na gari jingine na kusababisha gari hilo kuwaka moto katika kijiji cha Mushasha wilayani Missenyi mkoani Kagera barabara kuu iendayo nchini Uganda. Akizungumzia tukio hilo, mkuu wa wilaya ya Missenyi kanali Denice Mwila amesema kuwa tukio limetokea Oktoba 23 saa nane mchana, kwa kuyahusisha magari mawili likiwamo lenye namba za usajili STL 4842 linalomilikiwa na Tanroads likiendeshwa na dereva aitwaye Greyson Sospeter (40).…

Soma Zaidi >>

WAZIRI MKUU MAJALIWA KUINUA SOKO LA BIDHAA ZA NDANI ,AMPONGEZA RC MTAKA KWA UFANISI WA VIWANDA

  Dinna Maningo,Bariadi. Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa  amewataka Watanzania kununua bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi kwakuwa zinaaminika na zimetengenenezwa kwa ubora uliothibitishwa. Waziri Majaliwa aliyasema hayo wakati  akifungua maonyesho ya Viwanda vidogo (SIDO) yanayofanyika kitaifa  mtaa wa Nyakabindi kata ya Nyakabindi wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu yenye kauli mbiu ya  Pamoja tujenge Viwanda Kukuza Uchumi wa kati. Majaliwa alisema kuwa hakuna sababu ya kuagiza bidhaa nje ya nchi ili hali zinapatikana nchini hususani mkoani Simiyu ambako kuna viwanda vya kuzalisha Sabuni ,Chaki na vinginevyo…

Soma Zaidi >>

HALMASHAURI ZAELEKEZA KUTENGA ASILIMIA MBILI YA MAPATO YA NDANI KWENDA KWA WATU WENYE ULEMAVU.

    NA DANSON KAIJAGE,DODOMA NAIBU Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu ,Sera,Bunge,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu Stellah Ikupa, amezitaka halmashauri nchini kuhakikisha asilimia mbili ya mapato yake ya ndani iliyotengwa kwa ajili ya watu wenye ulemavu zinatolewa. Ikupa alitoa kauli hiyo jana kwenye tamasha la watu wenye ulemavu linalofanyika jijini Dodoma sambamba na wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) lililoandaliwa na The Foundation for Civil Societ (FSC). Sambamba na hilo pia amewataka wahusika wakiwemo maafisa maendeleo ya jamii kulielimishana kundi hilo kuhusiana mikopo hiyo inayotolewa na halmashauri ili iwanufaishe…

Soma Zaidi >>

RAIS MAGUFULI NA KIKWETE WAKUTANA IKULU LEO.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es salaam. Taarifa kutoka Ikulu zinasema kuwa Kikwete na Rais Magufuli wamekutana kwa utaratibu wa kawaida wa kusalimiana na kutakiana heri katika majukumu. Akizungumza baada ya kufanya mazungumzo na Rais Magufuli, Kikwete amesema kuwa, “Nimekuja kusalimiana na kumtakia kila la kheri anafanya kazi nzuri, aendelee tu kuchapa kazi na sisi tupo kwa namna yoyote ya kumpa nguvu tupo tayari kumsaidia“, amesema Rais mstaafu…

Soma Zaidi >>

DADA WA KAZI AMJERUHI SEHEMU ZA SIRI MTOTO WA MIEZI 9, ASINGIZIA MIZIMU.

Polisi nchini Kenya inamtafuta, Janet Auma ambaye ni dada wa kazi kwa tuhuma za kumjeruhi sehemu za siri mtoto wa bosi wake mwenye umri wa miezi 9. Janet Auma anatuhumiwa kumuingiza vidole sehemu za siri mtoto huyo na kumjeruhi vibaya, huku akisema kuwa mizimu ya babu yake ndiyo iliyosababisha kufanya kitendo hicho. Benadeta Mukami Ni mama wa mtoto alipoulizwa amesema kwamba alipata taarifa kutoka kwa mtoto wake wa kiume, ambapo alimpigia simu akiwa kazini na kumwambia kuwa mtoto anatokwa na damu sehemu za siri, na kuagiza amtoe pampers “Walipomtoa nepi,…

Soma Zaidi >>

MAUAJI YA WATOTO WAWILI, DC BUKOBA ALIAGIZA JESHI LA POLISI KUVURUGA KIJIJI KIZIMA

Na Allawi Kaboyo, Bukoba  Watu tisa ambao hawajatajwa majina yao kwa sababu za kiuchunguzi wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Kagera kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya watoto wawili wa familia moja, waliouawa kwa kuchinjwa na watu ambao bado hawajafahamika. Kaimu kamanda wa polisi mkoani Kagera Issack Msengi alisema kuwa tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Mashule kata Kyamulaile wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, baada ya watoto hao kutoonekana nyumbani kwao kabla ya miili yao kuokotwa. Kaimu kamanda huyo aliyataja majina ya watoto waliouawa kuwa ni  Auson Respicius (7)…

Soma Zaidi >>

JUMUIYA WA WAZAZI IRINGA YAKUTANA KUJADILI MAADILI YA VIJANA.

Na Francis Godwin,Iringa JUMUIYA ya wazazi wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa mjini imefanya kongamano la wazi la maadili kwa vijana kwa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt John Magufuli alilotoa katika mkutano mkuu wa jumuiya ya wazazi wakati wa mkutano mkuu wa jumuiya hiyo jijini Dodoma juu ya kuporomoka kwa maadili kwa vijana nchini. Katibu wa wazazi wilaya ya Iringa mjini Martha Ngunga akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika jana katika ukumbi wa siasa ni kilimo mjini hapa alisema kuwa shabaha ya…

Soma Zaidi >>

MATOKEO YA DARASA LA (7) HADHARANI

Baraza la Mitihani Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya Darasa la saba kwa wanafunzi waliofanya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi kwa mwaka 2018 ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 4.96 ukilinganisha na mwaka jana 2017. Akitangaza matokeo hayo Katibu Mtendaji wa Baraza la NECTA Charles Msonde amesema ufaulu umeongezeka kwa asilimia 4.96 tofauti na mwaka jana huku baadhi ya wanafunzi 357 wakifutiwa matokeo yao kutokana na udanganyifu. “Tathmini ya awali kiwango cha ufaulu kimepanda kwa asilimia 4.9% ikilinganishwa na 2017, pia kiwango cha ufaulu wa somo la Kiingereza uko chini sana…

Soma Zaidi >>

WAZIRI JAFFO ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA IGOMA, NYAMAGANA UNAO GHARIMU SHILINGI MILIONI 400

  Nyamagana Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Suleiman Jaffo akiwa ziarani Nyamagana ametembelea ujenzi wa Kituo cha Afya Igoma kilichopo Kata ya Igoma na kuridhishwa na kasi ya uendelezaji wa ujenzi wa majengo ya upasuaji (Theatre), Wodi ya wazazi (Maternity Ward), Maabara (Laboratory), Jengo la Mionzi (Radiology), Jengo la kuhifadhia Maiti (Mortuary) pamoja na jengo la kufulia nguo za Wagonjwa (Laundry) ambavyo vitagharimu shilingi Milion mianne (400,000,000.00). Akiongea kwa niaba ya wananchi Mbunge wa jimbo la Nyamagana Mheshimiwa Stanislaus Mabula, ameishukuru…

Soma Zaidi >>