ASASI NYINGI ZA KIRAIA ZIPO HATARINI KUTUMIWA KUTAKATISHA FEDHA

NA DANSON KAIJAGE, DODOMA IMEELEZWA kuwa Asasi za kiraia nchini zipo katika hatari ya kutumika kama sehemu ya kupitishia fedha chafu na watu wasiokuwa na nia njema. Hayo yalielezwa jana na Kaimu msajili wa mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali nchini Baraka Leonard,wakati alipokua akijibu baadhi ya maswali ya washiriki wa maonyesho ya wiki ya Azaki yanayofanyika jijini Dodoma. Alisema sekta hiyo ipo katika hatari kubwa ya kutumika kama sehemu ya utakatishaji wa fedha haramu ambazo zimekuwa zikipatika katika njia zisizo sahihi. Alisema kuwa fedha nyingi chafu zimekuwa zikingizwa nchini katika…

Soma Zaidi >>

MWENYEKITI WA CCM (W) TEMEKE NDUGU ALMISH HASSAL LEO AANZA ZIARA YAKE KWA KISHINDO

  Temeke Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke Pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Siasa (W) Temeke wamefanya ziara leo October 22 2018 na katika ziara hiyo waliweza Kuzungumza na Kamati ya Siasa Kata , Kamati za Siasa Matawi Yote , Baraza la Wazee kata , Kamati za Utekelezaji Kata(U.W.T , U.V.C.C.M , WAZAZI) , Kamati za Utekelezaji na Utendaji Kila Tawi , Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Diwani. Lengo la Ziara Hii ikiwemo Kukuza na Kudumisha Mahusiano Baina ya Viongozi na Kusikiliza Kero za ndani ya kata ya…

Soma Zaidi >>

KIWANGO CHA MAAMBUKIZI YA MALARIA CHAPUNGUA, SERIKALI YATENGA BILL 3 KUPAMBANA

  Imeelezwa kuwa, kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa maralia nchini Tanzania kimepungua kutoka asilimia 14.4 kwa mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 7 kwa mwaka 2017. Akizungumza kwenye uzinduzi wa matokeo ya utafiti wa viashiria vya malaria nchini kwa mwaka 2017, Mtakwimu Mkuu, Dkt. Albina Chuwa, amesema hiyo ni habari njema ndani ya Serikali ya awamu ya tano na hiyo imetokana na juhudi za Waziri mwenye dhaana ya sekta ya Afya. Amesema kuwa, hali ya uchumi wa taifa kwa mwaka 2017 ambao imeendelea kukuza kwa asilimia 7.1 ukilinganisha na asilimia…

Soma Zaidi >>

HUDUMA YA AKAUNTI YA KIKUNDI YA NBC KUWAKOMBOA WAJASIRIAMALI.

    Na Prakseda Mbulu,Mbeya. Wananchi na wafanyabiashara nchini wametakiwa kujiunga na huduma ya utoaji na uwekaji wa fedha kupitia akaunti ya kikundi iliyozinduliwa leo na benki ya NBC jijini Mbeya. Akizindua huduma hiyo leo katika viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya, katibu tawala wilaya Mbeya,Hassan Mkwawa amesema kwa muda mrefu wajasiriali na wananchi waliopo katika vikundi wamekuwa wakishindwa kupata huduma za kifedha kwa wakati kutokana na kukosekana kwa taasisi za kifedha pamoja na mlolongo mrefu wa upatikanaji wa huduma. “Niwapongeze NBC kwa kuanzisha huduma hii ambayo ni muhimu kwa…

Soma Zaidi >>

MGALU AKAMILISHA ZOEZI LA KUGAWA VIFAA VYA OFISI ZA UWT KATA ZOTE ZA MKOA WA PWANI

  Mbunge wa Viti Maalumu kutoka mkoa wa Pwani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu amekamilisha zoezi la kugawa vifaa vya ofisi kwa ofisi za Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT). Mhe. Subira Mgalu amekamilisha zoezi hilo hii leo na kukamilisha kata zote 133 za Mkoa wa Pwani kwa kuziwezesha Jumuiya hizo za Umoja wa wanawake Tanzania (UWT). ” Zoezi hili la ugawaji wa vifaa vya ofisi kwa Jumuiya yetu ya (UWT) nimelifanya katika Wilaya zote za Bagamoyo, Kibaha Mjini, Kibaha vijijini, Kisarawe, Mkuranga, Rufiji,…

Soma Zaidi >>

MO DEWJI AWASHUKURU WATANZANIA.

Baada ya siku chache kupita tangu Mfanyabishara Mo Dewji kupatikana leo amerudi mtandaoni kwa mara kwanza toka atekwe na watu wasiojulikana. Kupitia akaunti yake ya Twitter bilionea huyo leo ametweet kwa mara ya kwanza na kuwashukuru wote waliomuombea katika kipindi chote kigumu ambacho alikuwa ametekwa. “Nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kuokoa maisha yangu. Pamoja na kupitia kipindi kigumu lakini daima amesimama upande wangu. Marafiki zangu, napenda kuwashukuru wote kwa maombi yenu na kunitakia kheri. Mungu awazidishie kwa wema wenu. Baraka za Mungu ziwe nanyi leo na daima,” alitweet Mo jioni…

Soma Zaidi >>

TAKUKURU WATOA ELIMU KWA WASHIRIKI WA TAMASHA LA SANAA BAGAMOYO

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Nchini (TAKUKURU ) Wilayani Bagamoyo, Pwani imewataka Watanzania kuwajibika baada ya kutambua haki zao ili mapambano dhidi ya rushwa yaweze kufanikiwa kwa kiwango kikubwa. Kauli hiyo imetolewa leo Oktoba 22, 2018 na Afisa wa TAKUKURU  na Mratibu wa uelemishaji Umma Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Jane Mgaya  (Pichani juu) wakati wa Warsha ya uelemishaji kuhusu masuala ya rushwa kwa Wasanii waliofika kwenye tamasha hilo ambapo amesema kuwajibika itaifanya jamii kuwa na maendeleo ya juu tofauti na ilivyo sasa. “Watanzania wengi wamekuwa wakipambana  kutambua haki…

Soma Zaidi >>

MBUNGE WA VWAWA,HASUNGA AGAWA VIFAA VYA MICHEZO VYA MILIONI 17

MBUNGE wa Jimbo la Vwawa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,  Mhe. Japhet Hasunga  amekabidhi seti za jezi pamoja  na mipira yenye zaidi ya  thamani ya sh.milioni 17 katika shule za  Sekondari za kata nne  zilizopo katika jimbo hilo. Mbali ya kugawa vifaa hivyo, Mhe. Japhet Hasunga ametoa zawadi kwa baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya Hesabu, Fizikia pamoja na masomo mengine katika mitihani ya taifa  kwa kidato cha pili na cha nne ikiwa ni utekelezaji wa ahadi alizokuwa ameahidi kwa wanafunzi hao Akikabidhi  vifaa…

Soma Zaidi >>

MBUNGE MAVUNDE AMWAGA NEEMA KWA MAFUNDI CHEREHANI WA DODOMA MJINI

    Dodoma Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde amezindua Umoja wa mafundi Cherehani Dodoma(UMACHEDO) na kuahidi kuwasaidia mafundi hao upatikani wa mashine za kisasa na mafunzo katika kuelekea uanzishwaji wa kiwanda cha ushonaji. Mavunde ambaye pia ameteuliwa kuwa Mlezi wa Umoja huo,ameahidi kuwapeleka kwenye mafunzo maalum wanachama wa UMACHEDO katika kiwanda cha Opensanit Tabata na EPZA Mabibo-Dar es salaam kwa lengo la kuongeza ujuzi katika tasnia ya ushonaji. Aidha Mbunge Mavunde amewaunganisha mafundi hao na mifuko uwezeshwaji wananchi kiuchumi ambapo kwa sasa wameanza kukopeshwa chini ya…

Soma Zaidi >>

ZIARA YA WAZIRI PROF MAKAME MBARAWA KUMALIZA KERO YA MAJI WILAYANI NAMTUMBO

      Waziri wa maji Prof M. Mbarawa Jana October 21  2018 ametembelea wilaya ya Namtumbo na kukagua miradi mbalimbali ya Maji. Akiwa wilayani humo Waziri amefanya ukaguzi wa miradi miwili ya maji kati ya miradi mitano ambayo inatekelezwa wilayani Namtumbo. Naye Mkuu wa wilaya hiyo Bi Sophia Kizigo amesema, “Tulitembelewa na mheshimiwa Prof. M. Mbarawa, Waziri wa Maji katika ziara yake wilayani Namtumbo Waziri ameaikiliza taarifa ya hali ya upatikanaji wa Maji safi na salama katika wilaya ya Namtumbo na kutembelea miradi miwili (2) mikubwa kati ya mitano…

Soma Zaidi >>