CHAMA CHA MAPINDUZI KUWACHUKULIA HATUA KALI WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA WASIO SOMA MAPATO NA MATUMIZI.

  Katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Kata ya Mtoni Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es salaam Ndg. Humphrey Polepole Katibu Mwenezi wa CCM amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitawachukulia hatua kali Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wanaotokana na CCM wasio soma mapato na matumizi kwa wananchi kwa mujibu wa Sheria. Akifafanua suala hilo  hii leo Ndg. Polepole ameeleza kuwa kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa wa Mwaka 2019 CCM inahitaji watu watakao kuwa Viongozi wa wananchi kupitia CCM wenye sifa nzuri kwenye mitaa yao. Amekemea suala la urafiki,…

Soma Zaidi >>

WAZIRI DK.MWAKYEMBE AJIVUNIA UKONGWE WA TAMASHA LA SANAA BAGAMOYO

  Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe jana  Oktoba 20,2018 amepongeza juhudi zinazofanywa na uongozi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kwa juhudi zake za kukuza Sanaa Nchini. Dk. Mwakyembe ameyasema hayo  Oktoba 20,2018 wakati wa kungua rasmi  Tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo  huku akitoa wito kwa Wasanii kutumia tamasha hilo kama njia ya kujifunza. Akizungumza katika ufunguzi wa tamasha hilo  ambalo linatarajiwa kumalizika Oktoba 27, mwaka huu, Dk Mwakyembe amesema kupitia warsha zitakazo endeshwa na tamasha hilo zitakuwa chachu kwa…

Soma Zaidi >>

ASAS AJITOLEA KUSOMESHA YATIMA 10.

Na Francis Godwin,Iringa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Salim Asas amejitolea kusaidia kusomesha elimu ya sekondari watoto kumi walio katika shule ya sekondari ya Dairy Bread Life Tanzania kwa kuwalipia ada kiasi cha shilingi milioni ishirini kila mwaka kwa miaka minne. Asas ambae alikuwa ni mgeni rasmi alitoa ahadi hiyo jana wakati wa mahafali ya kidato cha nne katika shule hiyo iliyopo Mgera wilaya ya Iringa ,alisema kuwa amevutiwa na jitihada mbali mbali mbali zinazofanya na meneja mkuu wa shule hiyo mchungaji…

Soma Zaidi >>

WABUNGE SUBIRA MGALU NA ZAYNAB VULLU WAZIWEZESHA (UWT) WILAYA 7 ZA MKOA WA PWANI VITI 700.

  Wabunge wa viti maalumu kutoka mkoa wa Pwani kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Subira Mgalu na Mhe. Zaynab Vullu wamekabidhi viti mia moja (100) kwa Jumuiya ya Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Kibiti mkoani Pwani. Wabunge hao walitoa msaada huo hapo jana wakiwa katika ziara wilayani kibiti ikiwa ni wilaya yao ya saba kutembelea na kati ya nane za mkoa wa Pwani, ambapo tayari wamekwishasaidia kuinua vyanzo vya mapato kwa Jumuiya saba za wilaya za (UWT). Wabunge hao wa viti maalumu (Mhe. Subira Mgalu…

Soma Zaidi >>

KIKUNDI CHA ‘MAAFANDE’ WANOGESHA TAMASHA LA SANAA BAGAMOYO 2018

Kikundi cha shule ya Polisi Tanzania –Moshi ‘Maafande’  cha Ngoma za asili jana Oktoba 20, 2018 wameweza kukonga nyoyo umati uliojitokeza kwenye tamasha ufunguzi wa tamasha la 37 la Utamaduni na Sanaa Bagamoyo. Maafande hao waliweza kuteka jukwaa kwa ngoma za kabila la Wasonge (Wamanyema)  kwa kucheza ngoma ya Babobe. Ngoma hiyo inayochezwa kiustadi mkubwa iliweza kuwa kivutio kwa wananchi waliofika kushuhudia tamasha hilo.  

Soma Zaidi >>

OFA YA KUTEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA SAADAN KWA TSH. 91,000

BAGAMOYO: Hifadhi ya Taifa ya Saadani kupitia Tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo limetangaza ofa Watanzania na wasio Watanzania kutembelea hifadhi hiyo kuanzia Oktoba 25, 26 na 27 mwaka huu kujionea vivutio mbalimbali vya Utalii. Akizungumza Mhifadhi Utalii, Hifadhi ya Saadani, Bi. Apaikunda Mungure amesema ofa hiyo ni maalum kwa msimu huu wa tamasha la Sanaa Bagamoyo  ambapo kwa kiasi cha Tsh. 91,000   ni gharama kwa Raia wa Tanzania pamoja na Afrika Mashariki huku wageni kutoka nje ya Afrika Mashariki hao watalipia US$120 tu. “Ofa hii itanda kwa…

Soma Zaidi >>

UBER YAZINDUA ZANA YA USALAMA KWA ABIRIA NA MADEREVA

JOHANNESBURG, Kampuni ya UBER yaongezea usalama na yatoa Zana ya Usalama kwa abiria na madereva katika nchi 8, pamoja na Tanzania; Vipengele vitajumuisha Kituo cha Usalama, Waasiliani Wanaoaminika, kitufe cha usaidizi wa dharura na taarifa kuhusu viwango vya mwendo ambavyo unaweza kuvigeuza kukufaa.  Hivi Uber imetangaza Zana mpya ya Usalama ambayo, kwa wiki chache zifuatazo, itaanza kutumiwa na mamilioni ya abiria, madereva na watoa huduma ya uwasilishaji wanaotumia programu hii katika bara Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika. Zana hii itaanzisha vipengele vipya bunifu ambavyo vinalenga kuimarisha kigezo cha usalama,…

Soma Zaidi >>

KIKWETE KUWANUNULIA KOMBATI JESHI LA AKIBA

JESHI la akiba limekuwa ni msaada mkubwa katika jamii ya tanzania kutokana na vijanawengi wanaojiunga na jeshi hilo punde tu wanapomaliza mafunzo hayo upelekea kuwa ni kichocheo kikubwa katika jamii juu ya  suala zima la ulinzi na usalama sehemu wanazotoka vijana hao. Katika jimbo la chalinze mkoani Pwani wahitimu zaidi 400 wanatarajiwa kumaliza mafunzo ya Jeshi la akiba mwezi ujao na hivyo kujifungulia fursa kwa upataji wa ajira kwavijana hao kupitia kwenye mashirika mbalimbali katika wilaya hiyo ya Bagamoyo. Wakizungumza na mbunge wao vijana walitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni wengi…

Soma Zaidi >>

KAMISHNA MKUU WA TRA NCHINI AWATAKA WANANCHI KUENDELEA KULIPA KODI KWA HIARI.

Dar es Salaam. Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere amewataka wananchi kuendelea kulipa kodi kwa hiari ili nchi iweze kufikia uchumi wa kati na wa Viwanda katika kutekeleza ajenda ya maendeleo endelevu ya 2030. Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati akifungua fainali za mashindano ya Vilabu 11 vya kodi katika shule za Sekondari za mkoa Dar es Salaam na Pwani ambapo alisema mpaka sasa jumla ya Vilabu 226 vimeanzishwa tangu 2008. Amesema kuwa, mamlaka ya mapato  inamini kuwa wananfunzi ni kundi muhimu katika jamii,ambapo…

Soma Zaidi >>

MBUNGE JOSEPH KAKUNDA ATOA USIA MZITO KWA WANANCHI

  UJUMBE WANGU WA LEO JUMAPILI TAREHE 21 OKTOBA 2018 KWA WANASIKONGE NA WATANZANIA KWA UJUMLA Kaini alimuua Habil siyo Kwa sababu Habil alimkosea au alimsaliti au alikuwa na mpango wa kumpiga vita Kaini HAPANA. Kaini alimuua Habil Kwa sababu alishindwa kuhimili nguvu ya kutovumilia tunu ya Baraka aliyokuwa kapewa Habil na Mungu. Wakati mwingine binadamu unaweza kushangaa Kwa nini baadhi ya watu wanakupiga vita bila sababu yoyote ya kidunia! WENGINE hawakufahamu kabisa lakini wameambiwa tu huyu tumpige vita na tumpinge Kwa kila kitu chake na kila akifanyacho! Utashangaa Sana!!…

Soma Zaidi >>