DC MJEMA AAGIZA TAKUKURU KUWACHUKULIA HATUA WAFANYABIASHARA WANAOUZA MAENEO NA VIZIMBA

Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amemuagiza Afisa wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Ilala kufanya uchunguzi kwa wafanyabiashara wanaouza maeneo ya biashara katika Kata ya Kariakoo na vipande vya barabara. Mjema ameyasema hayo leo, katika Kata ya Kariakoo wakati akifunga ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua katika majimbo ya yaliopo wilayani humo, ikiwemo Ukonga, Segerea pamoja na Ilala. Amesema kuwa, katika kata hiyo kero kubwa aliyokutana nayo ni wafanyabiashara hao kutoshirikishwa katika ngazi ya maamuzi ambapo hadi n sasa wameshasikiliza kwa…

Soma Zaidi >>

TFDA KUTATUA CHANGAMOTO ZA UINGIZAJI WA BIDHAA NCHINI

  Dar es Salaam Serikali imesema pamoja na changamoto zilizopo katika mamlaka zinazosimamia masuala ya udhibiti wa uingizwaji wa bidhaa nchini, baadhi ya mawakala wa forodha wamekuwa wakighushi nyaraka na kuingiza bidhaa zisizokuwepo kwenye nyaraka hizo. Aidha , Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFFA) walieleza kuwa mamlaka za udhibiti ikiwemo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Mapato (TRA),Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali zimekuwa zikichangia ucheleweshaji wa utoaji wa mizigo na kusababisha gharama za bidhaa kuwa kubwa.…

Soma Zaidi >>

NAIBU WAZIRI MHE. HASUNGA AHAMASISHA WAKULIMA KWA KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII

    Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga amewashauri wakulima wajenge utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini mara baada ya kumaliza shughuli za mavuno. Aidha, amewahamasisha wakulima hao mara baada ya kuvuna na  kuuza mazao yao watenge muda wa kupumzika kwa kutembelea maeneo tofauti na yale waliyoyazoea badala ya kukaa sehemu moja. Ameitoa rai hiyo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wakati wa mkutano wa kilele cha  maadhimisho ya siku ya  chakula duniani iliyofanyika kitaifa katika mji wa Tunduma wilayani Mombo mkoani Songwe. Amefafanua kuwa hata hapo…

Soma Zaidi >>

NAIBU WAZIRI HASUNGA AHAMASISHA WAKULIMA “KULA MAISHA” KWA KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga amewashauri Wakulima wajenge utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini mara baada ya kumaliza shughuli za mavuno Amesema wasidhani kuwa wao ni watu wa mashambani pekee na hivyo hawastahili “kula maisha.” Pia amewahamasisha Wakulima hao mara baada ya kuvuna na  kuuza mazao yao watenge muda wa kupumzika kwa kutembelea maeneo tofauti na yale waliyoyazoea badala ya kukaa sehemu moja. Ameitoa Rai hiyo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wakati wa Mkutano wa Kilele cha  maadhimisho ya  Siku ya  Chakula Duniani iliyofanyika…

Soma Zaidi >>

WANANCHI WA KIJIJI CHA BUANGA KUKAMILISHA UJENZI WA SHULE JANUARI 2019

    MUSOMA Wananchi wa Kijiji cha Buanga kwa kushirikiana na Viongozi wa Serikali ya Kijiji hicho wamesema wamejipanga kuhakikisha ifikapo mwezi Januari 2019 watakuwa wamekamilisha zoezi la ujenzi wa Shule mpya ya UTAYARI inayojengwa Kijijini humo. Hayo yalisemwa na Viongozi wa Kijiji cha Buanga kwa niaba ya Wananchi wao jana tarehe 17. 10. 2018 wakati wakiendelea na zoezi la ufyatuaji wa matofali kwenye eneo la ujenzi wa Shule ya Utayari Mpya Buanga. Aidha Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Buanga Ndugu Kejile M. Eyembe alisema, “tunashukuru sana kwa mchango…

Soma Zaidi >>

KAMATI KUU YA CHADEMA YAWAWEKA KIKAANGONI KUBENEA NA KOMU, WAJITOKEZA HADHARANI KUKILI MAKOSA.

  Dar Es Salaam Kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA iliyoketi jana tarehe 17/08/2018 chini ya Mwenyekiti wake mheshimiwa Freeman Alkaeli Mbowe imetoka na maadhimio makuu manne ikiwa ni pamoja na kuwavua nyadhifa zao zote ndani ya Chama na kuwakeka chini ya uangalizi mkali ndani ya mwaka mmoja. Akisoma Maadhimio hayo leo tarehe 18/10/2018 alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari Naibu Katibu Mkuu bara mheshimiwa John Myika amesema, “Kuhusu sakata la wabunge Antony Komu na Saed Kubenea Kamati Kuu ya Chama imaamua Kuwapa onyo kali, Waaandike barua…

Soma Zaidi >>

FID Q,MKUBWA NA WANAWE NDANI YA TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA 2019

Staa wa muziki wa Hip Hop Fareed Kubanda maarufu kama “Fid Q” ni miongoni mwa Wasanii ambao watashiriki katika msimu wa 16 wa Tamasha kubwa muziki la Sauti za Busara mwakani, 2019. Kwa mujibu waandaaji wa tamasha hilo lenye kauli mbiu “Where African Music Stars Shine Brightly”, taasisi ya Busara Promotions wameeleza kuwa, orodha hiyo ni wasanii waliokubali na kukidhi vigezo vya kushiriki huku orodha nyingine ikitarajiwa kuongezwa hapo baadae. Katika orodha hiyo iliyotolewa mapema jana Oktoba 17,2018, Mbali na Fid Q ambaye anatokea Tanzania, Wasanii wengine na Nchi zao…

Soma Zaidi >>

MRADI WA MAJI WA BULINGA-BUSUNGU WAANZA KUTEKELEZWA KATIKA WILAYA YA MUSOMA VIJIJINI

    MRADI wa Maji wa Bulinga – Busungu katika Kata ya Bulinga umeanza kutekelezwa ili kuondoa tatizo la uhaba wa maji kwenye vijiji vya Kata hiyo na vya Kata za jirani. Wananchi wa Kata ya Bulinga wamesema, sasa wanashuhudia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020 ikitekelezwa na Serikali kwa vitendo. Wamemshukuru Mbunge wao Prof Muhongo kwa ufuatiliaji wa umakini mkubwa wa miradi ya maendeleo ya Jimbo lao. Wananchi hao wameendelea kusema kwamba ukamilikaji wa Mradi huo utaondoa tatizo la uhaba wa maji na kuongeza muda wa…

Soma Zaidi >>

MADAKTARI WAPEWA MUONGOZO WA KUANDIKA DAWA KWA WAGONJWA

Serikali Kupitia Wizara Ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa muongozo kwa madaktari na wafamasia kote nchini kuandika majina halisi ya dawa badala ya kuandika majina ya kibiashara yanayosababisha usumbufu kwa wagonjwa na baadhi ya watoa huduma. Muongozo huo umetolewa na Naibu Waziri wa afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Tumbi wilayani Kibaha mkaoni Pwani mapema leo. Dkt. Ndugulile amesema majina ya biashara yanayoandikwa na baadhi ya watoa huduma za afya yanasababisha usumbufu mkubwa kwa wagonjwa…

Soma Zaidi >>

SEKTA YA UTALII KUNYANYUA UCHUMI WA ZANZIBAR

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema kwamba maonyesho ya Utalii yanayofanyika Zanzibar ni muhimu kwa Serikali na wananchi kwa kuwa yamelenga kuitangaza Zanzibar na sekta ya utalii ambayo ndio muhimili mkuu wa uchumi. Dk. Shein aliyasema hayo leo huko katika viwanja vya hoteli ya Verde, Mtoni Mjini Zanzibar katika ufunguzi wa maonyesho ya Utalii Zanzibar ya mwaka 2018 ambayo yalihudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Makamo wa Pili wa…

Soma Zaidi >>