KATIBU MKUU WA CCM AONGOZA UJUMBE ZIARA YA KIMKAKATI NCHINI CHINA

Ujumbe wa Viongozi wa CCM umeondoka leo kuelekea nchini China kwa ziara ya kimkakati inayolenga kuongeza mahusiano kati ya CCM na Chama Cha Kikomunisti cha Watu wa China (CPC), Kamaradi Bashiru Ally Katibu Mkuu wa CCM anaongoza ujumbe huo. Akizungumza kabla ya kuanza safari Kamaradi Bashiru ameelezea safari hiyo kwamba ni ya kimkakati na inalenga kuimarisha mahusiano kati ya CCM na CPC. Aidha amesisitiza safari hiyo pamoja na mambo mengine ujumbe wa viongozi hao utakwenda kubadilisha uelewa, uzoefu na kujifunza mikakati ya kujitegemea kirasilimali ili kuendesha Chama, namna bora na…

Soma Zaidi >>

WAZIRI MWAKYEMBE AWAPIGIA DEBE WABUNIFU WA AFRIKA MASHARIKI

Na Andrew Chale, Dar Waziri wa Habari, Sanaa, Utamduni na Michezo Mhe. Dkt Harson Mwakyembe ameziomba sekta za uwezeshaji na mashirika kujitokeza kwa wingi kusaidia juhudi za Wabunifu wa kazi za Sanaa ili kukuza sekta hiyo kwa Nchi za Afrika Mashariki. Dkt. Mwakyembe ameyasema hayo  Oktoba 12, 2018 wakati wa kufunga rasmi Kongamano la Pili  la Sekta ya Sanaa na Ubunifu ya Afrika Mashariki kuhusu Uwekezaji  (2nd Mashariki Creative Economy Impact Investment Conference) lenye kauli mbiu ‘Haki Ubunifu ni mali, Nikopeshe’ Akitoa neno la kufunga kongamano hilo, Dkt. Mwakyembe amebainisha…

Soma Zaidi >>

MBUNGE RORYA AWAHAIDI MILIONI 2 WANAWAKE,UJENZI WA CHOO BUKWE SEC

Mbunge wa Jimbo la Rorya Lameck Airo amewahaidi kuwapa Milioni moja akina mama wanaouza viazi vitamu pembezoni mwa barabara ya Tarime- Mwanza eneo la Kotwo kata ya Bukwe wilayani Rorya ili kutengeneza meza badala ya kuuza viazi vikiwa chini. Pia Mbunge huyo ameahidi kutoa milioni moja kujenga vyoo vya wasichana katika shule ya Sekondari Bukwe ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake. Mbunge huyo aliahidi mbele ya wananchi wa Kata ya Bukwe wakati wa mkutano wa kujadili maendeleo na wizi wa mifugo. Akisoma Risala fupi ya maendeleo na usalama,Mtendaji wa Kijiji…

Soma Zaidi >>

BIBI KIZEE ADAI KUTOTENDEWA HAKI, POLISI YAMTAKA KUFUNGUA KESI UPYA.

      Na Mwandishi wetu Rorya. Mkuu wa Polisi katika wilaya ya Kipolisi Rorya Ramadhan Sagire amemtaka Annastazia Opiyo mweye umri wa miaka (82) mkazi wa Kijiji cha Buganjo kata ya Bukwe wilayani Rorya mkoani Mara kufungua upya kesi yake. Bibi huyo alidai kutotendewa haki na Mahakama ya Wilaya ya Tarime baada ya kesi yake dhidi ya Odhiambo Matiku anaidaiwa kumpiga na kumjeruhi na kisha kumuuwa Kijana wake John Gawi. Mjane huyo alieleza hayo mbele ya Mbunge wa Jimbo la Rorya Lameck Airo na Maafisa wa Polisi wakati wa…

Soma Zaidi >>

SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUENDELEA KUMUENZI BABA WA TAIFA

IKULU  Dar Es salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kuhakikisha fikra na mipango mizuri aliyoiweka inatekelezwa kwa manufaa ya Watanzania wote. Mhe. Rais Magufuli ametoa kauli hiyo tarehe 14 Oktoba, 2018 wakati akizungumza na Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani Jijini Dar es Salaam alikokwenda kumtembelea muda mfupi baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Jumapili iliyofanyika katika Kanisa la…

Soma Zaidi >>

NDUGU SALUM KALLI AFUNGUA RASMI KONGAMANO LA KUMUENZI BABA WA TAIFA KATA YA MBUGANI

    Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Nyamagana Ndugu Salum Kalli amefungua kongamano la kumuenzi Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Kata ya Mbugani kwa kumbukizi za miaka 19 toka atangulie mbele za haki ambapo maadhimisho haya kitaifa kufanyika Mkoani Tanga. Ndugu Kalli ametumia hadhara hiyo kuasa wana Nyamagana na wana Mbugani kuangalia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika taifa la Tanzania kwa kupima maendeleo yalivyojijenga kuanzia awamu ya kwanza hadi awamu ya tano. Kutumia historia ya mafanikio kwa kumuenzi mwasisi wa taifa hili Baba wa Taifa hayati…

Soma Zaidi >>

CHAMA CHA MAPINDUZI CHAPITA BILA KUPINGWA UCHAGUZI MDOGO UDIWANI KATA YA MABATINI

  Nyamagana Mwanza.   Chama Cha Mapinduzi kata ya Mabatini wilayani Nyamagana hivi leo tarehe 13/10/2018 kupitia Mgombea wake Ndugu Deus Lucas Mbehe kimetangazwa mshindi katika marudio ya uchaguzi mdogo wa Udiwani. Kaimu Mkurugenzi wa uchaguzi akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Mwanza Kiomoni Kiburwa Kibamba amesema Ndugu Deus Lucas Mbehe ndio mgombea pekee kupitia Chama Cha Mapinduzi aliyejitokeza katika kuwania kinyang’aniro hicho hivyo kwa mamlaka aliyopewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa mujibu wa kifungu cha 82(a) cha sheria ya uchaguzi wa Serikali za…

Soma Zaidi >>

MH NDALICHAKO AACHA HISTORIA KONGAMANO LA ELIMU PANGANI.

  Pangani TANGA Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa Joyce Ndalichako amekua mgeni rasmi katika kongamano la Elimu wilaya ya Pangani tarehe.13.10.2018 Mheshimiwa Ndalichako ameanza kwa kutembelea shule mbalimbali,kukutana na kuongea na walimu,na wanafunzi. Kongamano limehudhuriwa na viongozi sekta zote Wilaya ya Pangani ikiwemo wadau wa Elimu toka ndani na nje ya Pangani ikiwemo kamati ya siasa,kamati ya ulinzi na usalama, wajumbe wa bodi na kamati za shule, walimu wote wa Pangani, maafisa Elimu kata, Wafanyabiashara,Wawekezaji, taasisi mbalimbali toka ndani na nje ya Pangani ikiwemo NSSF mkoa, TPA mkoa,vNMB na…

Soma Zaidi >>

MWENYEKITI UVCCM PWANI: NDOTO YA MAFANIKIO HUTIMIZWA KWA BIDII.

  Pwani. Mwenyekiti wa Uvccm mkoa wa Pwani ndugu Charangwa S. Makwiro amewaasa vijana Kujiamini na Kuwa na Bidii pindi wanapotaka kutimiza ndoto zao . Ndugu Charangwa ameyasema hayo october 13,2018 akiwa mgeni rasmi katika mahafali ya saba (7)ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Ngorongo wilayani Rufiji mkoani Pwani. “Ili ufikie mafanikio lazima uwe na ndoto ambapo ukiongeza na Kujiamini pamoja na Bidii lazima utafanikiwa tofauti na hivyo utakua kijana wa kuburuzwa kila kitu unapangiwa kama Bendera kufuata upepo” alisema Charangwa Aidha Bi.charangwa ameendelea kusisitiza wanafunzi wanaobakia…

Soma Zaidi >>