MKE WA MWALIMU MKUU AJIFUNGUA KOKWA ZA PARACHICHI-MKURUGENZI ATOA MWEZI MMOJA .

Musoma, Mara. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Ndg. John Lipesi Kayombo amewataka Diwani wa Kata ya Bugoji, Mwenyekiti wa Kijiji cha Bugoji, Wenyeviti wa kamati za msingi Kanderema ‘A’ na ‘B’ pamoja na wananchi kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja vitendo vya kishirikina vinavyoendelea katika shule hizo vinatokomezwa. Ametoa agizo hilo jana wakati wa kikao cha pamoja kati yake na viongozi wa Kata ya Bugoji, viongozi wa Kijiji cha Bugoji, walimu wa shule za Msingi za Kanderema ‘A’ na Kanderema ‘B’ pamoja na wananchi wa Kijijij cha Bugoji. Kikao…

Soma Zaidi >>

TANZANIA NA KENYA KUUNGANISHWA NA MRADI WAUMEME KUTOKA SINGIDA HADI NAMANGA.

  Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu ametembelea yadi ya kuhifadhia miundombinu ya kujenga mradi wa kusafirisha umeme wa msongo mkubwa wa 400kV kutoka Singida hadi Namanga ambao utaunganisha nchi ya Tanzania na Kenya(KTPIP) Kwa upande wa Tanzania mradi huo utajengwa kwa umbali wa kilometa 414, Kituo kipya cha kupoza umeme mjini Arusha, na kupanua Kituo cha kupoza umeme cha Singida. Vijiji 14 vitapata umeme, 7 kati ya hivyo ni vya mkoa wa Singida, Manyara 2, na Mkoani Arusha 5. Kwa upande wa Kenya mradi huo utajengwa kwa urefu wa…

Soma Zaidi >>

WANANCHI WA LUDEWA KUPATA UMEME WA GRIDI YA TAIFA.

  Ludewa,Njombe. Wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe kwa mara ya kwanza leo wamepata umeme wa grid ya Taifa baada ya kutumia umeme wa mafuta kwa zaidi ya miongo mitano sasa. Meneja wa Mradi wa ujenzi wa njia ya usafirishaji wa umeme Makambako – Madaba – Songea Mhandisi Didas Lyamuya amesema, kwa mara ya kwanza Tanesco imewasha umeme wa Grid ya Taifa katika Halmashauri ya Ludewa wenye uwezo wa kilowatts 2000 ambazo ni sawa na megawatts 2. Amesema,umeme utakaowashwa Ludewa unasafirishwa kwenye njia ya msongo wa 33…

Soma Zaidi >>

MH MABULA KUMALIZA CHANGAMOTO YA MIUNDOMBINU YA BARABARA NA ELIMU.

  Nyamagana Mwanza. Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula ameendelea na ziara yake ya mtaa kwa mtaa katika kata ya Mkolani na mitaa ya Kasese, Mkolani, Nyamazobe pamoja na mtaa wa Mlimani na kusikiliza kero za wananchi katika miundombinu ya barabara pamoja na sekta ya elimu. Aidha Mhe.Mabula amewapongeza wananchi kata za Mkolani Mitaa ya Nyamazobe na Mlimani kuanza ujenzi wa barabara kufikia maeneo ya miinuko kwa jitihada zao wenyewe na kuahidi kuunga mkono jitihada hizo kwa kushirikiana nao katika upasuaji wa mawe ili ujenzi huo wa barabara ukamilike…

Soma Zaidi >>

MEYA MWASHILINDI: MILIONI MIA SABA KUJENGA KITUO CHA AFYA NZOVWE.

  Na, Rashid Msita, Mbeya. Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya ambaye pia ni diwani wa Chadema kata ya Nzovwe Mhe. D.P Mwashilindi amewaomba wananchi wa kata ya Nzovwe kuchangia nguvu zao katika ujenzi wa kituo cha afya. Mwashilindi amezungumza hayo leo wakati wa ziara yake ambapo pia amefanya mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya Nzovwe. Amesema tayari shilingi milioni mia saba, 700,000,000 za miundombinu na vifaa tiba,zipo na ujenzi unatakiwa kukamilika ndani ya siku mia moja na ishirini. Kukamilika kwa kituo hicho kutapelekea upatikanaji wa huduma zote…

Soma Zaidi >>

UMEZAJI DAWA NDIYO SULUHISHO KAMILI KATIKA KUDHIBITI MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE

Na WAMJW – SONGEA Pamoja na juhudi zinazofanywa na Serikali na wadau mbalimbali katika kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, mwamko wa wananchi wa mkoa wa Ruvuma kutumia kingatiba bado upo chini hivyo kukwamisha malengo yaliyokusudiwa. Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi. Christina Mndeme alipokuwa akifungua semina ya uraghibishaji na uhamasishaji wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa Wakuu wa wilaya pamoja na wataalam wa Mamlaka za Serikali za mitaa za mkoa wa Ruvuma iliyofanyika katika ukumbi wa mipango Oktoba 13, 2018. Mkuu huyo wa mkoa aliyataja magonjwa…

Soma Zaidi >>

WAZIRI KANGI LUGOLA ANENA MAZITO, AONYA JUU YA UPOTOSHAJI KWAMBA TANZANIA HATUNA AMANI.

    Dar Es Salaam Tanzania Na Augustine Richard Darmpya.com Waziri wa Mambo ya Ndani mhe,Kangi Lugola leo tarehe 13/09/2018 amezungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam na kutolea ufafanuzi juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea yanayohusiana na Wizara hiyo ikiwemo suala la uvunjifu wa amani na hofu kwa Watanzania. Akizungumza na waandishi wa habari Waziri Lugola amesema, “Kumekuwepo na viashilia vya uvunjifu wa usalama nchini lakini kwasababu tunalo jeshi la Polisi ni lazima Wananchi waonyeshe ushirikiano kwa jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa” Aidha tunatoa wito kwa wenye…

Soma Zaidi >>

RC HAPI AOMBWA KUMALIZA MGOGORO WA MPAKA KATI YA MANJI NA MSIGWA

MKUU wa  mkoa wa Iringa Alli  Hapi  ameombwa  kuwawajibisha  watendaji  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa    waliopuuza  agizo la  ofisi ya mkuu  wa  mkoa  iliyotolewa na  aliyekuwa  mkuu  wa mkoa wa Iringa Amina Masenza  kuhusiana na mgogoro wa mpaka kati ya  Manji na  Cosmas Msigwa . Akizungumza na mtandao huu  leo  Jamila Manji  amesema  kuwa    kufuatia  mgogoro  huo  wa  mpaka  uliokuwepo  eneo la  kiwanja   kilichopo  eneo la  stendi  kuu ya  mkoa wa Iringa  ofisi ya  mkuu wa  mkoa wa Iringa chini ya  aliyekuwa  mkuu wa mkoa  Amina Masenza …

Soma Zaidi >>

MCHUNGAJI DR ILOMO AWATAKA KWAYA KUU KUSHIRIKI KONGAMANO LA KUMUENZI NYERERE

  Wakati kesho ni maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha baba wa Taifa mwalimu Julius Nyerere wito watolewa kwa vikundi vya Kwaya kushiriki maadhimisho hayo. Wito huo umetolewa leo na mchungaji Dr Feles Ilomo wakati wa mkutano mkuu wa Kwaya kuu ya Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Iringa mjini. Dr Ilomo ambae ni mwenyekiti wa Kwaya kuu amesema kutokana na umuhimu wa siku hiyo ya kesho ni vema wanakwaya na jamii kushiriki midahalo ya kumuenzi baba wa Taifa. ” Mimi nitakuwa mmoja wapo wa watoa mada…

Soma Zaidi >>

JESHI LA POLISI MKOANI IRINGA LAKAMATA WATUHUMIWA 17 KWA MAKOSA YA WIZI

Iringa Tanzania Jeshi la Polisi mkoani Iringa limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 17 wakituhumiwa kwa makosa ya uvunjaji na wizi pamoja na kupatikana na mali zinazodhaniwa kuwa ni za wizi. Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamanda wa Polisi mikoani Iringa ACP Juma Bwire Makanya amesema katika mkoa huo mali zilizopatikana ni pamoja na TV bapa 14, TV chogo 5, Sabufa 6, Deki 3, Kompyuta mpakato 2, Spika 3, ving’amuzi 3, Draya 1, Redio za kawaida 4, Mitungi ya gesi 2 na Inverter moja na kichwa Cha Cherehani na Kompyuta monita 2.…

Soma Zaidi >>