KUNA HAJA YA MITIHANI YA TAIFA KUTOFAUTIANA KATI YA SHULE ZA MJINI NA VIJIJINI..

NA MWL.MGALA R.B 0715079380,0675967150 mgalaramadhan@gmail.com Leo nimeona kwa kifupi sana kuwashirikisha sehemu ya tafiti zangu binafsi juu ya Elimu yetu,nikianza na Elimu ya msingi ikiwa ni utafiti nilio ufanya siku 180 kabla ya mtihani wa taifa wa kuhitimu elimu ya msingi uliofanyika tar 5&6 sep 2018. Katika utafiti wangu niligundua changamoto zilizopo katika sekta ya elimu zinafananafanana na zile zinazozikabili sekta zingine,Changamoto yeboyebo kama uhaba wa watumishi,Nyumba za walimu,Maslahi Zimetawala katika maeneo mengi ingawa juhudi za Serekali katika kuzitafutia ufumbuzi ni kubwa. Ukiachiliambali changamoto hizo,Elimu katika sehemu za vijijini imegubikwa…

Soma Zaidi >>

WAKALA WA (DART) AWAOMBA RADHI WATUMIAJI WA MABASI HAYO.

Taarifa Kwa Umma. Wakala wa mabasi yaendayo haraka (DART) amewaomba radhi watumiaji wa mabasi yanayotoa huduma katika mfumo wa DART kwa kuchelewa kuanza kufika kwenye vituo siku ya Jumatano,Oktoba 10, 2018 asubuhi na hivyo kusababisha msongamano mkubwa wa abiria hususan katika kituo kikuu Cha Kimara. Baada yakufanya uchunguzi wa chanzo Cha tatizo hilo, imebainika kuwa kuchelewa kwa mabasi kutoa huduma ulitokana na baadhi ya madereva wa kampuni ya mtoa huduma (UDART) kufanya hujuma ya kuzuia mabasi yaliyokuwa yameegeshwa katika karakana ya Jangwani kwa kuziba geti la kutokea kwa kuegesha mabasi…

Soma Zaidi >>

HALMASHAURI YA TARIME YAENDELEA KUWA BORA KWA UTEKELEZAJI MAJUKUMU KWA WANANCHI.

  Tarime, MARA. Halmashauri ya wilaya ya Tarime vijijini yaendelea kuwa bora katika kutekeleza majukumu ya wananchi mkoani mara Akiyasema mafanikio hayo mbele ya mkutano wa baraza la madiwani lililoketi leo Oktoba 12, 2018, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, (……………) ameyataja mafanikio hayo kwa mwaka wa fedha 2017/2018 kuwa ni kuendelea kuwa na hati safi tangu kuundwa kwa halmashauri hiyo. Mafanikio mengine ni halmashauri (Tarime Vijijini) hiyo kuwa bora kati ya halmashauri 154 nchi nzima, ambapo halmashauri 36 tu ndio zimekusanya mapato vizuri na Tarime vijijini ikiwemo. Aidha, halmashauri imefanikiwa kujenga…

Soma Zaidi >>

DC MMANDA AWATAKA WATENDAJI WA HALMASHAURI, KUANZIA VIJIJI HADI MITAA KUJITAFAKARI.

  Mtwara Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda amewataka watendaji wa Halmashari zote tatu za wilaya hiyo kuanzia ngazi za vijiji na mitaa kila mmoja kujitafakari kwa nafasi yake katika suala la kusimamia ukusanyaji mapato katika maeneo yao akisisitiza kila mtumishi awajibike kwa nafasi yake. Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani Halmashauri ya Mji Nanyamba, amesema kuna tabia imejengeka kwa watumishi wa umma hususani watendaji kuona maeneo yenye upungufu wa mapato lawama zinaelekezwa kwa mkurugenzi wa halmashauri na kusema hoja hiyo haina nafasi kwenye wilaya ya Mtwara. “Ambae…

Soma Zaidi >>

MKUU WA WILAYA”WALIMU JIEPUSHENI NA VITENDO VYA UTOVU WA NIDHAMU”

BUKOBA NA Allawi Kaboyo, Walimu katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wameaswa kutokujihusisha na vitendo vya utovu wa nidhamu ambavyo vinachangia kushusha heshima kwa taaluma yao. Akizungumza katika kongamano la siku ya mwalimu duniani lililofanyika manispaa hiyo, Mkuu wa wila ya Bukoba DEODATUS KINAWIRO amewakumbusha kutimiza wajibu wao kabla ya kudai haki zao. Kinawiro amesema kuwa walimu kama watumishi wengine wa umma wanatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi zao, na kuwataka kuwa na subira wanapotaka kutoa adhabu kwa wanafunzi ili wasitoe adhabu zinazoweza kusababisha madhara. Amesema kuwa ni…

Soma Zaidi >>

WALIMU,WATENDAJI WA VIJIJI NA KATA WATAKIWA KURIPOTI MATUKIO YA UKATILI

Na: Cleo Tarime. TARIME. Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari wilayani Tarime Mkoani Mara pamoja na watendaji wa vijiji, na kata wametakiwa kuendelea kutoa taarifa juu ya matukio ya ukatili wa kijinsia  kwa watoto wote ukiwemo Ukeketaji na Ndoa za Utotoni ili kupunguza Ukatili unaofanyika katika jamii Kauli hiyo imetolewa na Katibu tawala Wilaya ya Tarime John Marwa katika Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani ambapo Wilayani Tarime maadhimisho hayo yamaeadhimishwa katika kata ya Mwema. Marwa amesema kuwa suala licha ya matukio ya ukatili kuwepo katika jamii…

Soma Zaidi >>

UBORESHAJI WA BARABARA KATA YA MWANGATA WAPONGEZWA.

Na Francis Godwin,Iringa   WANANCHI  wa kata ya  Mwangata katika Manispaa ya  Iringa wamepongeza  ukarabati  wa  miundo mbinu ya  barabara  unaoendelea  kufanyika  katika kata  hiyo kuwa  utasaidia kutatua  kero  ya  usafiri  iliyosababishwa na  ubovu  wa  miundo mbinu hiyo.   Wakizungumza  jana   kwa niaba ya  wanzao John  Ndelwa na  Alex  Tumaini walisema  kuwa  ukarabati  wa  barabara  unaoendelea  kufanyika katika  mitaa ya  kata ya  Mwangata  ni ukombozi mkubwa  kwao na  kuwa  kukamilika kwa ukarabati huo  kutasaidia wananchi  wa kata hiyo  kuepukana na  changamoto  za  usafiri .   Walisema bararaba  za  mitaa katika…

Soma Zaidi >>

Kongamano la pili la sekta ya Sanaa na Ubunifu Afrika Mashariki lafanyika Dar

Kongamano la Pili  la Sekta ya Sanaa na Ubunifu ya Afrika Mashariki kuhusu Uwekezaji  (2nd Mashariki Creative Economy Impact Investment Conference) lenye kauli  mbiu ‘Haki Ubunifu ni mali, Nikopeshe’ llilokuwa la siku mbili Oktoba 11-12, 2018 limemalizika  huku wadau na Wabunifu mbalimbali kutoka Tanzania na Nchi za Afrika Mashariki  wakipata kujadili changamoto katika sekta hiyo. Awali akifungua kongamano hilo Oktoba 11,2018 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya uwekezaji Bwana Aritiside Mbwasi  ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji,  Mhe. Charles Mwijage  amesema Sekta ya ubunifu ina umuhimu…

Soma Zaidi >>

CDF KWA KUSHIRIKIANA NA UBALOZI WA USWIDI YATOA MAFUNZO KWA WASICHANA ZAIDI 140

Dar es Salaam Shirika la Jukwaa la utu wa mtoto (CDF ) kwa kushirikiana na chuo cha kikuu kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) chini ya ufadhili wa shirika la FORWARD UK na ubalozi wa Uswidi Tanzania wameandaa kongamano la sauti ya msichana. Katika kongamano hilo limewakutanisha wasichana takribani 141 kutoka mikoa ya Mara,Dodoma na Dar es Salaam ambapo lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha wanawake hao na viongozi katika kujadili mipaka mbalimbali ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili. Akizungumza na waandishi wa Mkurugenzi mtendaji wa Shirika…

Soma Zaidi >>

PROFESA NDALICHAKO KUWA MGENI RASMI MAONYESHO YA TAE 2018.

  Waziri wa Elimu Sayansi Tekenolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako,anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maonyesho ya ya elimu kwa shule za msingi,sekondari na vyuo vikuu yatakayofanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba 16-18 mwaka huu,katika viwanja vya Leaders jijini Dar esSalaam. Muandaaji mkuu wa maonyesho hayo ya Elimu,Deogratius Shija,ambaye pia ni msanii wa filamu nchini,amesema Lengo la maonyesho hayo ni kuwawezesha wazazi walezi kupata taarifa ya shule na vyuo mbalimbali, kwa ajili ya muhula wa mwaka 2019 kwa ajili ya watoto wao. “Katika maonyesho haya sisi Tanzania Academic…

Soma Zaidi >>