WAZIRI WA UJENZI ATOA AHADI NONO KWA WANANCHI WA TUNDURU.

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amewahakikishia wananchi wa Tunduru ujenzi wa Barabara ya Mchepuo (Tunduru By Pass na uboreshaji wa keep left kilichopo Tunduru mjini ). Mhe. Kamwelwe Alieleza hayo akiwa katika ziara wilayani humo akikagua barabara ya Tunduru Mangaka na Tunduru Kilimansera. Waziri huyo alisema amedhamiria kufanya hivyo kutokana na barabara kuu iliyopita katikati ya mji wa Tunduru kuzidiwa na malori na msongamano wa Magari. Kwa upande wake Mbunge wa Tunduru kaskazini Mhandisi, Ramo Makani alieleza madhara yanayojitokeza Mara kwa Mara kwenye keep left iliyojengwa chini…

Soma Zaidi >>

HAKI ELIMU WAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA KIKE NCHINI.

Mpwapwa Dodoma Shirika la Haki Elimu limeadhimisha siku ya mtoto wa kike nchini kwa kugawa vitabu na taulo za kike kwa wanafunzi. Akizungumza kwenye zoezi la ugawaji wa vitabu Katika Halmashauri ya wilaya Mpwapwa jijini Dodoma ofisa wa Shirika la Haki Elimu Bi.Airene Mkinga amesema kuwa wameamua kugawa vitabu hivyo ambavyo ni vitabu Kiada ili kuweza kuwajengea wanafunzi moyo wa kusoma vitabu ili kuweza kujiongezea ufahamu na maarifa mbalimbali. “Siku hizi moyo wa usomaji vitabu umepungua miongoni mwa watanzania zaidi ya kubaki kusoma Biblia na Quraan kitu kinachotishia kujiongezea maarifa…

Soma Zaidi >>

KUTEKWA KWA MO DEWJI; HIZI NDIZO KAULI ZA MASHABIKI WA SIMBA

  Stori: Brighton Masalu, Dar Mpya Zikiwa zimekatika saa kadhaa tangu kuenea kwa habari za kutekwa kwa mfanyabiashara  maarufu ndani na nje ya nje na muwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohamed Gulam Dewji ‘Mo Dewji’ na kisha kuthibitishwa na vyombo vya usalama, mashabiki wa Klabu hiyo wametoa kauli tofauti juu ya tukio hilo. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Dar Mpya jioni hii katika maeneo tofauti, mashabiki hao walitoa maoni yenye hisia tofauti huku wote wakilaani vikali tukio hilo na kumuomba Mungu atende muujiza kuwezesha kupatikana kwa Mo Dewji akiwa salama.…

Soma Zaidi >>

SERIKALI YAWASHUKIA WALIOSHINDWA KUENDELEZA VIWANDA.

  MTWARA Na,Omary Hussein. Naibu waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Stella Manyanya amewataka wawekezaji walioshindwa kuendeleza maeneo yao kwa muda mrefu, hususani wamiliki wa viwanda vilivyo binafsishwa, kutumia busara kwa kueleza ukweli ili Serikali ichukue hatua ya kuviwezesha viwanda hivyo kufanya kazi. Naibu waziri ameyasema hayo Mkoani Mtwara akiwa katika kiwanda cha kutengeneza Cement cha Dangote, baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku moja, iliyolenga kujiridhisha na hali ya viwanda mkoani humo. “Sisi kama Serikali tusingependa kuona wawekezaji wakishindwa kujiendeleza bila sisi kuwasaidia lakini ni kwawale tu wenye nia ya…

Soma Zaidi >>

KATIBU CHAMA CHA MAPINDUZI NYAMAGANA AKABIDHI MATOFARI 400 SHULE YA MSINGI BUGANDO

    Nyamagana Mwanza Ndugu Salum Kalli Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Nyamagana hivi leo amekabidhi matofari 400 ya Saruji Shule ya msingi Bugando kwaajili ya ujenzi wa madarasa mawili, ikiwa ni msaada kutoka kwa Wanachama wa CCM shina la wakereketwa Magufuli Merelani Soko Kuu Kata ya Pamba. Akikabidhi msaada huu ndugu Kalli amepongeza jitihada za Wafanyabiashara wadogo wadogo kwa jitihada za kuunga mkono Serikali ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Rais wa awamu ya tano Mhe. Dkt John Pombe Magufuli iliyoelekeza elimu bure kuanzia Shule ya awali…

Soma Zaidi >>

VYUO VIKUU NCHINI KUZALISHA VIJANA IMARA WATAKAOWEZA KUSHINDANA KATIKA SOKO LA AJIRA

    Serikali imevitaka Vyuo Vikuu nchini, kutengeneza Vijana wenye uwezo mkubwa watakao ingia kwenye soko la ajira kwa nchi za Africa na kote Ulimwenguni bila kikwazo. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Stella Ikupa amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akifungua Mkutano wa Kimataifa Uliokutanisha Vijana ambao biashara zao ziko kwenye hatua za awali na ambao wanatafuta marafiki wa biashara, unafahamika kama Innovation in the Data Age. Ikupa amesema Africa kwa sasa inakadiriwa kuwa na watu bilioni moja nukta…

Soma Zaidi >>

AKAMATWA KWA KUFANYA KAZI NCHINI BILA KIBALI.

  Na,Allawi Kaboyo, Bukoba. Raia wa Ufaransa Philippe Krynen anayefanya kazi katika shirika lisilo la kiserikali la Patage Orphans Support amekamatwa na maafisa kazi mkoani Kagera, kwa tuhuma za kufanya kazi bila kibali. Kukamatwa kwa Raia huyo ni mwendelezo wa zoezi la ukaguzi mahala pa kazi linaloendeshwa na maafisa kazi mkoani Kagera la kuhakikisha watu wote hasa Raia wa kigeni wanakuwa na vibali vya kufanya kazi nchini. Akiongelea zoezi hilo Afisa kazi mkoa wa Kagera Bi Hadija Hersi amezungumza kuwa wakati wakiendelea na ukaguzi wao katika taasisi mbalimbali, walibaini uwepo…

Soma Zaidi >>

WAZIRI MKUU AAGIZA UCHUNGUZI WA FEDHA ZA DAWA MPWAPWA

  Na Stephen Noel @Dar mpya MPWAPWA WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri kuchunguza matumizi ya sh. Milioni 70 zinazotelewa na serikali kwenye wilaya hilo kila mwezi kwa ajili ya kununulia dawa. Majaliwa alitoa agizo hilo juzi jioni wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mpwapwa. Kwenye mkutano huo wananchi wamelalamika kuhusu ukosefu wa dawa ambapo dawa pekee ambazo hupatiwa ni za kutuliza maumivu. “Nilidhani wabunge wanachosema Bungeni sicho nikasema nakuja niyasikie, Kweli wananchi hawaridhiki nimeona. “Sasa mkuu wa wilaya shughulika na hili…

Soma Zaidi >>

RC CHALAMILA ATOLEA UFAFANUZI KAULI YAKE ILIYOPOTOSHWA NA BAADHI VYOMBO VYA HABARI.

  Na,Rashid Msita, Mbeya. Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila atolea ufafanuzi kauli yake iliyopotoshwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini juu ya kile alichozungumza kuwa anashauri Rais aongezewe madaraka kwa kuteua watendaji wa wilaya kama ilivyokuwa kwa wakuu wa mikoa,wilaya wakurugenzi. Mhe. Chalamila amesema kuwa habari hiyo imepotoshwa na alichozungumza yeye ni kuwa suala la msingi ni kwamba wakuu wa Idara za Halmashauri zote nchini wapatikane katika mfumo tunaopatikana watendaji wengine kama sisi. “Yaan kwa sasa ili uwe mkuu wa Idara lazima Baraza la Madiwani likithibitishe…

Soma Zaidi >>

SAKATA LA MO LINAFIKIRISHA NA KUTOA ELIMU YA KIPEKEE

Na Brighton Masalu, Dar Mpya Taarifa za kutekwa na kisha kupotea kusikojulikana kwa mfanyabiashara mkubwa nchini na Afrika, Mohamed Gulam Dewji ‘MO’  zimeshtua na kuzua taharuki kubwa. Mshtuko ulishamiri kutokana na aina ya mazingira ya tukio lenyewe kama lilivyoelezwa na mashuhuda na baadaye kufafanuliwa na Kamanda wa Polisi-Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Lazaro Mambosasa. SACP Mambosasa amekiri mbinu iliyotumika kutekwa kwa mfanyabiashara huyo na muwekezaji wa klabu kongwe ya mpira wa miguu ya Simba  ni mpya kidogo. Mambosasa anasema: “Aina ya utekwaji aliyotekwa mfanyabiashara Mo…

Soma Zaidi >>