TAASISI YA AGRI THAMANI FOUNDATION YASAINI MKTABA WA MAKUBALIANO NA OFISI YA MKUU WA MKOA KAGERA KUTOKOMEZA CHANGAMOTO YA LISHE KAGERA.

  Na: Allawi Kaboyo Taasisi mpya ya Agri Thamani Foundation iliyoanzishwa kwa lengo kuu la kuboresha lishe Mkoani Kagera na kuongeza ushirikishwaji wa wanawake na vijana katika kuongeza Mnyororo wa thamani kwenye Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi imetiliana saini na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera katika Mkataba wa Makubaliano ili kuanza utekelezaji wa shughuli zake ifikapo Novemba Mosi, 2018. Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Taasisi ya Agri Thamani Foundation ambaye ni mzawa wa Mkoa wa Kagera Bi Neema Lugangira mara baada ya kutiliana saini kwenye Mkataba wa Makubaliano…

Soma Zaidi >>

NAIBU WAZIRI WA KILIMO AKUTA MAZITO MRADI WA UMWAGILIAJI CHATO.

  Mara tuu baada ya Wizara ya maji kurejesha kitengo cha umwagiliaji Kwa Wizara ya kilimo Siku ya jana tarehe 9 ,Octoba, 2018 jijini Dodoma na kuwa chini ya Wizara ya kilimo. Leo tarehe 10/10/2018 Mhe Naibu Waziri wa Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa ametembelea vijiji vya Nyisanzi na Bwawani Kata Ya Kigongo Wilaya ya Chato Mkoa Wa Geita kukagua mradi wa umwagiliaji. Mradi huu ulianzishwa Mwaka 2013 ambao haukukamilika chini ya Mkandarasi NYAKIRANG’ANYI CONSULTANT LTD toka Musoma ambaye aliushughulikia Kwa mwaka mmoja na hakuendelea. Mhe. Naibu Waziri alishuhudia kukwama kwa…

Soma Zaidi >>

CCM TEMEKE YAWAONYA WAENDESHA BODABODA.

  Brighton Masalu, Dar Mpya Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Temeke, Mhe.Almishi Hassal amewataka waendesha bodaboda kuhakikisha wanajisajili kwenye vikundi vinavyotambulika kama njia ya kujihakikishia usalama wao ikiwa ni pamoja na kuijali kazi yao kama zilivyo zingine. Mwenyekiti huyo ameyasema hayo mapema leo alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi vyeti kwa madereva wa chama cha waendesha bodaboda wilayani humo (CMPD) waliohitimu mafunzo ya wiki mbili ya usalama wa barabarani katika chuo cha ufundi cha Temeke jijini Dar es Salaam. Aidha, katika hafla hiyo, waendesha bodaboda hao…

Soma Zaidi >>

KASSIM MAJALIWA AWATAKA WATENDAJI WA VIJIJI KUWACHUKULIA HATUA WANAOKATA MITI BILA VIBALI

Mpwapwa Serikali imesema itahakikisha umeme unawafikia watanzania wote iwe wenye nyumba za bati au nyasi, ambapo amewaagiza watendaji wote wa vijiji kuainisha maeneo yenye misitu na vyanzo vya maji na kuwachukulia hatua kali wote watakaobainika kukata miti bila kibali. Akizungumza leo katika ziara yake wilayani Mpwapwa, Majaliwa amseema wakazi wa maeneo ya vijijini watalipa sh. 27,000 badala ya sh. 380,000 kuunganishiwa huduma ya umeme. “Kama zitahitajika nguzo umeme kufika kwenye makazi yako, Serikali italeta na umeme utafika kwenye vijiji vyote hata kama mlimani ikishindikana kuweka nguzo tutafunga sola (umeme jua),”…

Soma Zaidi >>

MWALIMU NYERERE FOUNDATION YAWAKUTANISHA WADAU MBALIMBALI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI

Dar es Salaam Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation imeandaa kongamano maalum la siku mbili lililowakutanisha viongozi mbalimbali wa vyama siasa nchini lenye lengo la kujadili umuhimu wa amani na utulivu katika kipindi kabla na baada ya uchaguzi Mkuu 2020. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo hii, Mkurugenzi mtendaji wa taatisis hiyo, Joseph Butiku wakati akifungua kongamano hilo, amesema kuwa, kumekua na viashiria vya uvunjifu wa amani nchini katika kipindi cha uchaguzi, hivyo ameamua kuwakutanisha wadau hao ili waweze “Tumeamua kukutana hapa leo baada ya kufanya…

Soma Zaidi >>

IGP SIRRO AFANYA MABADILIKO YA MAKAMANDA WA POLISI.

Mkuu wa jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, amefanya mabadiliko ya baadhi ya makamanda wa Polisi wa vikosi hapa nchini. Katika mabadiliko hayo aliyekuwa Kamanda wa Polisi Viwanja vya ndege, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Matanga R. Mbushi anakwenda kuwa Mkuu wa vikosi Maalum vya Polisi, Kamisheni ya Operesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi, Nafasi ya DCP Matanga inachukuliwa na aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jeremiah Shilla, hivyo anakuwa Kamanda wa Polisi Viwanja vya ndege. Vilevile aliyekuwa Kamanda wa Polisi kikosi Cha…

Soma Zaidi >>

NAIBU WAZIRI WA AFYA APIGA MARUFUKU MAJINA YA KIBIASHARA KUTUMIKA KWENYE DAWA.

Naibu Waziri wa Afya Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile amepiga marufuku majina ya kibiashara kutumika katika Hospitali zote za Serikali na badala yake yatumike majina ya asili ambayo yanatambulisha dawa hizo. Ameyasema hayo mapema leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema,wanapiga marufuku madaktari kuandika dawa kwa majina ya kibiashara na badala yake waandike majina ya asili GenericName. “Tunapiga marukufu na kuwataka watumie majina asili na halisi ya dawa ambayo Madaktari wote wamejifunza kwa muda wote wakiwa masomoni na ndiyo yanayotakiwa kutumika” alisema Dkt. Faustine Ndungulile .…

Soma Zaidi >>

NAIBU WAZIRI MGALU AAGIZA TANESCO KUONGEZA NGUVU KATIKA VIJIJI VYENYE UHITA

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ameliagiza Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuongeza nguvu ya umeme katika vijiji vyenye uhitaji mkubwa nchini kulingana na mahitaji ya kijiji husika. Agizo hilo amelitoa jana Octo 09,2018 alipokua katika ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa usambazaji na kuwasha huduma ya umeme vijijini kupitia mradi wa njia ya kusafirisha umeme mkubwa wa 400kV Backbone (BTIP) katika Wilaya ya Igunga mkoani Tabora pamoja na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa REA III awamu ya kwanza. Mgalu ametoa agizo katika Kijiji cha Mwamashimba chenye…

Soma Zaidi >>

MAJIMBO MATATU KUSINI MASHARIKI MWA MAREKANI KUATHIRIKA KWA KIMBUNGA.

  Takribani watu nusu milioni wanatakiwa kuondoka haraka katika makazi yao eneo la kusini mashariki mwa Marekani ili kupisha kimbunga Michael ambacho kinakaribia kulikumba eneo hilo. Taarifa za watabiri wa hali ya hewa zinasema kimbuka hicho kwa sasa kimekwisha ingia katika hatua ya tatu na kuongezeka kasi yake kwa kadri kinavyopitia ghuba ya Mexico kuelekea jimbo la Florida, Alabama na Georgia. Kimbunga hicho kinasababisha upepo mkali ambao unakwenda kwa kasi ya kilomita 200 kwa saa, ambapo wataalam wanasema kuwa wakazi wa jimbo la Florida leo huenda wakakumbwa na mawimbi maji…

Soma Zaidi >>