RAIS MAGUFULI AWASIMAMISHA KAZI VIONGOZI WA POLISI KYERWA.

  Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa kamanda wa polisi mkoa wa Kagera,Augustino Ollomi,kamanda wa polisi wilaya ya Kyerwa,Justine Joseph,mkuu wa upelelezi wa wilaya ya Kyerwa Evarist Kivuyo na mkuu wa kituo cha polisi Kyerwa,Robert Marwa. Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu imesema viongozi hao wa polisi wamesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za kuhusika katika magendo ya zao la kahawa katika wilaya ya Kyerwa pamoja na tuhuma nyingine. Aidha Mh.Rais Magufuli amemuagiza katibu mkuu wa wizara ya…

Soma Zaidi >>

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AWATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MIKOPO NA UWEZESHWAJI KIUCHUMI.

  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde amewataka vijana kuunda vikundi,SACCOS na Makampuni ili kuchangamkia fursa za uwezeshwaji kiuchumi kupitia mfuko wa maendeleo wa Vijana na mifuko mbalimbali ya uwezeshaji wananchi kiuchumi. Mavunde ameyasema hayo leo katika Viwanja vya Tangamano,Jijini Tanga wakati akizindua maadhimisho ya wiki ya Vijana katika kuelekea kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru tarehe 14.10.2018 katika uwanja wa Mkwakwani,Tanga. “Tunajua moja ya changamoto kubwa inayowakabili Vijana ni ukosefu wa mitaji, Serikali imedhamiria kuwafikia Vijana wengi zaidi kwa kuwapatia…

Soma Zaidi >>

NYAMAGANA YAJIPANGA KUTATUA UKOSEFU WA VYUMBA 1200 VYA MADARASA IFIKAPO MWAKA 2019.

Mwanza. Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula amewaambia wananchi wa Kata ya Mabatini kupitia mkutano wa hadhara viwanja vya Kabengwe, Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kupitia Halmashauri ya Jiji la Mwanza imeweka mkakati wa kukabiliana na changamoto za upungufu wa vyumba vya Madarasa 1200 inayoikabili sekta ya elimu katika shule za sekondari na Msingi Wilayani Nyamagana. “Tumenunua kifyatulio cha Tofari chenye uwezo wa kufyatua Tofari 6000 kwa Saa, tutaagiza Saruji na Nondo kutoka kiwandani tukitazamia ifikapo 2019 tutakamilisha ujenzi wa Vyumba vya madarasa 1200” Mhe Mabula amesema. Mhe. Mabula…

Soma Zaidi >>

WAZIRI AZINDUA MBIO ZA BAISKELI, ACHANGISHE Mil 280 KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU

NA MWANDISHI WETU NAIBU Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Joseph Kakunda amezindua mpango wa mashindano ya mbio za baiskeli na kufanikisha kukusanya Sh milioni 280 kati ya Sh milioni 340 zinazotarajiwa kukusanywa kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu nchini. Mashindano hayo yaliyopewa jina la ‘Imara Pamoja Cycle Challenge’, yameandaliwa na Kampuni ya Uchimbaji wa Madini nchini -Acacia kwa kushirikiana na Tasisi binafsi kutoka nchini Canada – CanEducate. Akizungumza katika uzinduzi wa uchangiaji wa mashindano hayo juzi jijini Dar es Salaam, Kakunda…

Soma Zaidi >>

TAKUKURU YAWAFIKISHA ZAIDI YA WATUHUMIWA 11 KINONDONI KWA MAKOSA YA UHUJUMU UCHUMI.

  Na Augustine Richard Darmpya.com Dar Es Salaam Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) imewafikisha watuhumiwa zaidi ya 11 wanaokabiliwa na makosa mbalimbali, zaidi ya 4oo katika mkoa wa kipolisi Kinondoni. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam Naibu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Kinondoni ndugu Bernard Hazinamwisho amesema “Tumeamua kuzungumza na waandishi wa habari leo ili kuufukishia habari Umma wa Watanzania juu ya utekelezaji wa majukumu yanayofanywa na ofisi yao. Pia wajue madhara ya vitendo vya rushwa na matokeo yake ili waweze kujirekebisha kitabia…

Soma Zaidi >>

MHE.MABULA AKABIDHI VITABU VYENYE THAMANI YA SH.MILIONI 12.

  Nyamagana, Mwanza. Mbunge jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula amekabidhi vitabu 442 vya Sayansi, michepuo wa Art pamoja na uchumi katika shule ya sekondari Mahina iliyopo Kata ya Mahina. Vitabu hivyo vyenye thamani ya shilingi 12,000,000.00 ni msaada kutoka taasis ya SOS “”Serve Our Soul kwa dhima ya kuboresha sekta ya elimu wilayani humo kwa kutekeleza kwa vitendo Sera ya elimu mwanafunzi mmoja kitabu kimoja. “Ninawashukuru SOS kuwa wadau wa maendeleo Nyamagana,shule ya Mahina mtumie msaada huu wa Vitabu kama ulivyokusudiwa, tuondokane na dhana ya kusifika kutokupenda kusoma” amesema…

Soma Zaidi >>

MHE. MABULA KUKARABATI SHULE YA MSINGI MANDELA MTAA WA KIKWETE IGOMA.

  Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanislaus Mabula kupitia ziara yake ya Mtaa kwa Mtaa aliyoifanya jana ametembelea Mtaa wa Kikwete Kata ya Igoma kwa dhima ya kusikiliza na kutatua kero mbali mbali za wananchi. Mhe. Mabula katika ziara yake ya Mtaa kwa Mtaa ameambatana na Diwani Viti Maalum Halmashauri ya Jiji la Mwanza ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Kikwete Mhe. Anifa, Diwani Kata ya Mhandu Mhe. Sima C Sima, Mtendaji Kata na watendaji wa serikali za mitaa pamoja na viongozi mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi. Mhe.…

Soma Zaidi >>