WANUFAIKA WA TASAF MPWAPWA WATAHADHARISHWA

Wanufaika wa kaya maskini wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma wametakiwa kutumia fursa za pesa za Tasaf kubadilisha maisha Kama serikali ilivyo kusudia. Hayo yamesemwa na ofisa ufuatiliaji wa Tasaf wilayani Mpwapwa Bwana Hosea Sichone alipokuwa akiongea na wanufaika wa mradi huo wa vijiji vya Kingiti na Lukole alipokuwa kwenye ziara ya ukaguzi wa uhawalishaji (utoaji) wa fedha kwa wanufaika hao. Sichone amesema tangu mpango huo uanzishwe kuna baadhi ya Kaya wameonyesha mafanikio mkubwa na yenye kuonekana kwa jamii . Aidha Sichone amesema kuwa pia wapo watu ambao tangu Mango huo uanzishwe…

Soma Zaidi >>

MAVUNDE AANZISHA TUZO ZA TAALUMA “MAVUNDE ACADEMIC AWARD” KWA WANAFUNZI WA JIMBO LA DODOMA MJINI.

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony P. Mavunde ameanzisha tuzo maalum za Taaluma kwa ajili ya mwanafunzi mmoja mmoja watakaofanya vyema katika mitihani ya Taifa ya Elimu ya Msingi na Sekondari. Aidha wanafunzi watakao ibuka mshindi katika tunzo hiyo,ofisi ya Mbunge itawagharamia masomo yao mpaka katika ngazi ya Chuo kikuu. Mavunde ameyasema hayo leo katika Shule ya Dodoma Sekondari wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Vitabu 1500 vyenye thamani ya Tsh 20,000,000 na taa za umeme jua 1000 za kusomea zenye thamani ya Tsh 17,000,000 kwa Shule za…

Soma Zaidi >>

SHIRIKA LA DIGINITY KWANZA LAIOMBA SERIKALI KUWAPA FURSA WAKIMBIZI

Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na masuala ya wakimbizi nchini Tanzania, (Dignity Kwanza ) Janemary Ruhundwa ameiomba Serikali kuwapa fursa wakimbizi wanaoingia nchini bila kuvunja utaratibu uliowekwa. Kauli hiyo ameitoa mapema leo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi kuweza kuripoti masuala mbali yanayohusu wakimbizi. Amesema kuwa, endapo Serikali itaweza kuwapa fursa wakimbizi kwa kuwawezesha kujihudumia wenyewe pamoja na kufanya kazi hii itasaidia Serikali pamoja na kuweza kuongeza pato la taifa kutokana na shughuli…

Soma Zaidi >>

WAZIRI MWALIMU AMEIAGIZA ST. FRANCIS KUPUNGUZA GHARAMA ZA MATIBABU KWA WANANCHI.

Na WAMJW – IFAKARA Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameuagiza uongozi wa Hospitali ya Dini ya St.Francis kupunguza gharama za matibabu kwa wananchi ndani ya mwezi mmoja kabla hajarudi kufanya ukaguzi wa mara ya pili. Ameyasema hayo wakati akiwa katika ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika Hospitali ya St Francis iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Ifakara Mkoa wa Morogoro kufuatia taarifa isiyoridhisha juu ya gharama za matibabu iyoripotiwa siku ya Octoba 3 na Televisheni ya Taifa (TBC). Waziri Ummy…

Soma Zaidi >>

DC HOMERA ATATUA TATIZO LA MAJI TUNDURU.

  Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mhe. Juma Homera amehamasisha wadau wa Mkoa Ruvuma na kuweza kufanikiwa kupunguza kero ya maji wilayani humo kwa kiwango kikubwa. Hayo ameyasema jana alipokua akitoa shukurani zake kwa wananchi na wadau walioshiriki kikamilifu katika jitihada za kuwakomboa wananchi wa wilaya hiyo. “Ahsante (HUC ) wanafunzi wangu wa Mbesa Airport Primary School na walimu hatimaye wamepata maji, ndani ya Mbesa peke yake visima zaidi ya 10 kuchimbwa, tukutane maeneo ya tukio tutatue kero za wananchi tutekeleze ilani ya CCM 2015 / 20, tunduru mpya !…

Soma Zaidi >>

UONGOZI WA CCM WILAYA YA KYELA WAZIMULIKA KERO ZA WAKULIMA WA KAKAO.

  Na Rashid Msita,Mbeya. Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kyela kimeagiza kusitishwa mara moja mfumo wa stakabadhi mazao ghalani kwakuwa chama hicho kimebaini utaratibu huo umeanzishwa bila maandalizi muhimu kufanyika. Hayo yamesemwa hiyo jana na Katibu wa Siasa,Itikadi na Uenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kyela Ndugu Emmanuel Mwamlinge mbele ya waandishi wa habari ” Wananchi na wakulima hawakushirikishwa wala hawakupewa taarifa ya kufutwa ushirika kupitia mikutano ya vijiji na kata (KAMAKA) na hivo maamuzi ya kikao hiko yalikua ni batili” amesema Ndugu Emmanuel Mwamlinge. kamati ya…

Soma Zaidi >>

UKOSEFU WA CHAKULA CHANZO CHA UDUMAVU KWA WATOTO.

  Na Cleo, Shinyanga. Imebainika kuwa  suala la ukosefu wa lishe bora ni chanzo kikubwa cha udumavu kwa watoto ambapo asilimia 43 ya watoto hao wamedumaa kwa kukosa lishe bora huku asilimia 45 ya wanawake kati ya miaka 15 hadi 49 wanaupungufu wa damu kwa sababu ya upungufu wa lishe ndogo jambo ambalo linazidi kusababisha kushuka kwa uchumi wa taifa. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Shirika la TGNP Mtandao  Lilian Liundi hapo jana katika tamasha la jinsia ngazi ya wilaya mwaka 2018 lililoandaliwa na Shirika hilo  nakufanyika katika viwanja vya Sabasaba Kata ya Maganzo Wilayani  Kishapu Mkoani Shinyanga huku…

Soma Zaidi >>