UWT WILAYA YA UBUNGO YAAHIDI KUREJESHA JIMBO 2020.

Dar es salaam. Umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Ubungo, wameahidi kuwa uchaguzi wa mwaka 2020 Chama cha Mapinduzi (CCM) kitashika dola katika jimbo la Ubungo na kurejesha kata zilizopotea ambazo kwa sasa zinakaliwa na wapinzani. Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa umoja wa Wanawake mkoa wa Dar es Salaam, Doroth Kilave, wakati wa maadhimisho ya wiki ya wanawake wa chama hicho. “Wanawake wa UWT ni jeshi kubwa kwa umoja wetu tutahakikisha tunalinda dola, chama kinashinda chaguzi zake katika jimbo la Ubungo na majimbo mengine yaliopo…

Soma Zaidi >>

DIWANI KATA YA MWANGATA AKUTANA NA WATUMISHI WA UMMA

NA FRANCIS GODWIN ,IRINGA Diwani wa kata ya Mwangata jimbo la Iringa mjini kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Edward Nguvu Chengula amekutana na watumishi wa umma kata ya Mwangata kupata mipango kazi yao. Diwani Chengula amekutana Leo na watumishi hao katika ofisi ya kata ya Mwangata ikiwa ni mwendelezo wa vikao vyake vya ndani na watumishi wa umma kwa ngazi mbali mbali. Akizungumzia kikao hicho amesema kuwa toka achaguliwe kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni amekuwa akikutana na watumishi hao ili kupokea changamoto zao na mikakati ya kiutendaji kazi ili…

Soma Zaidi >>

NAIBU WAZIRI KANDEGE ATOA AGIZO ZITO KIGAMBONI

Kigamboni Na Brighton Masalu, Dar Mpya Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Josephat Kandege ametoa agizo kurekebishwa ramani ya ujenzi wa jengo la wodi ya wazazi katika kituo cha afya cha Kigamboni tofauti na ilivyokuwa awali. Agizo hilo, amelitoa leo alipokua katika ziara ya kukagua miradi ya mendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa ofisi za halmashauri hiyo, ambapo katika ziara hiyo aliambatana viongozi mbalimbali ikiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ngw’ilabuzu Ludigija “Haiwezekani ujenzi wa jengo la wazazi…

Soma Zaidi >>

MBUNGE MABULA ATEMBELEA MRADI WA SOS, SH. MILL. 255 KWA AJILI YA UJENZI WA MADARASA 7.

  Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanislaus Mabula ametembelea mradi mkubwa unaotekelezwa na Taasisi ya SOS kwa ajili ya ujenzi wa vyumba saba vya madarasa shule ya Msingi Igelegele Kata ya Mahina uliogharimu shilingi 255,000,000.00. Amesema kuwa, kufuatia taasisi hiyo kujitolea kujenga mradi wa kujenga vyumba vya madarasa vilivozingatia ubora wa matumizi ya ardhi, amewapongeza kwa kujuhudi walizoonesha katika kuleta maendeleo. “Nawapongeza wadau wa maendeleo SOS kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa vizuri, vyenye ubora na vinavyozingatia matumizi bora ya ardhi na kufanya shule ya msingi Igelegele kuwa shule ya…

Soma Zaidi >>

MATOKEO YA DARASA LA SABA YAFUTWA, NI KWA WALIOFANYA UDANGANYIFU

Dar es salaam. Baraza la taifa la mitihani NECTA, limefuta matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya msingi kwa shule zote Za msingi zilizopo Halimashauri ya Chemba ikiwa ni pamoja na shule ya Hazina na New Hazina,Fountain Joy,Anny Ndumi za Dar es Salaam na Alliance,New Alliance ,Kisiwani za Mkoani Mwanza pamoja na Kondoa Integrity Za Kondoa baada Ya kubainika shule hizo kuvujisha mtihani huo. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam,katibu mtendaji wa(Nacte),Dkt. Charles Msonde amesema Baraza hilo limefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa watendaji na…

Soma Zaidi >>

SERIKALI YANUNUA MASHINE ZA MIONZI ZENYE THAMANI YA BILIONI 1.74

Dar es Salaam Serikali kupitia wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto imenunua mashine za Mionzi (digital X-ray) zipatazo kumi zenye thamani ya shilingi bilioni 1.74. Hayo yamesemwa leo na waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu wakati akipokea mashine hizo kwenye Bohari ya Dawa(MSD) jijini Dar es Salaam.. Waziri Ummy amesema kuwa serikali inaendelea kutoa kipaumbele katika kuboresha huduma za afya nchini ikiwa ni lengo la kuhakikisha huduma za afya zinawafikia watanzainia wote karibu na maeneo wanayoishi. “Maendeleo ya Taifa letu la Tanzania yataletwa na wananchi wenye…

Soma Zaidi >>

NAIBU WAZIRI WA ELIMU ASHANGAZWA MILANGO YA VYUO KUNUNULIWA KENYA.

  Namtumbo. Naibu Waziri wa Elimu William Ole Nasha jana, ametembelea wilaya ya Namtumbo na kukagua mradi wa ujenzi wa chuo cha VETA ambapo pia alipokea taarifa ya elimu kutoka kwa mkuu wa wilaya hiyo, Sophia Kizigo. Aidha pamoja na kupongeza jitihada na hatua ya mradi huo ilipofikia, lakini alishangazwa kukuta kuwa milango yote iliyowekwa katika majengo ya chuo hicho ilinunuliwa nchini Kenya badala ya Tanzania. Kwa upande Injinia, wa mradi huo alijitetea kwamba Tanzania hakuna kiwanda kinachotengeneza milango hasa milango ya aina hiyo. Hata hivuo, Naibu waziri aliwashauri kwamba…

Soma Zaidi >>

WIZARA YA ELIMU YAWATAKA WANANCHI KUPUUZA HABARI ZINAZOSAMBAZWA MITANDAONI KUHUSU (KKK)

Dar es salaam Wizara ya Elimu,sayansi na Teknolojia imewaomba wananchi kupuuza taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikionesha kushuka kwa viwango vya kujua kusoma na kwa wanafunzi wa darasa la pili. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa October 1 mwaka huu na wizara hiyo, imesema kuwa upimaji wa (KKK) kusoma, kuandika na kuhesabu uliofanywa mwaka 2017 na Baraza la mitihani la Tanzania imeonesha mafanikio makubwa katika stadi za kusoma,kuandika na kuhesabu. Aidha, imesema takwimu za upimaji zilizosambazwa mitandaoni, ziliwasilishwa kwenye kikao cha tathmini ya mwaka kwa sekta kwa ajili ya maridhiano…

Soma Zaidi >>