KILA MKULIMA WA KOROSHO ATALIPWA PESA ZAKE KUPITIA AKAUNTI YAKE: DC MTWARA.

  Mtwara. Serikali imesema kuwa kila mkulima wa korosho atalipwa pesa zake kupitia akaunti yake ili kuepusha mkulima kudhulumiwa pesa kama ilivyokua huko nyuma. Hayo yamesemwa leo tarehe 1 Oktoba, 2018 na Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mhe. Evod Mmanda wakati akizungumza na wakulima wa zao hilo wilayani humo. “Msimamo wa Serikali ni kila mkulima atakayeuza korosho lazima aingiziwe fedha zake kwenye akaunti yake yeye mwenyewe, hakuna malipo yatakayopitia kwenye akaunti ya mtu mwingine, nasisitiza hapo na mnielewe vizuri maana msimu uliopita bado tunakesi zinaendelea za watu kudhulumiana hatutaki hayo…

Soma Zaidi >>

MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA OLMOLOG WILAYANI LONGIDO YAHITIMISHWA RASMI.

  Mbunge wa jimbo la Longido mhe Dr Steven Kiruswa ameendelea na ziara jimboni, leo ametembelea kata ya Kamwanga na kukagua ujenzi wa kituo kipya cha Polisi kinachoendelea kujengwa, Mbunge huyo ametoa matenki mawili yenye ujazo wa lita 3000 kwa kila moja na amepokea changamoto zilizopo katika nyumba za kuishi askari, na kuwaahidi kuzishughulikia. Wakati huo huo Mkuu wa wilaya ya Longido Mhe Frank Mwaisumbe amefunga mafunzo ya jeshi la akiba kata ya Olmolog,katika ufungaji huo amewapongeza wananchi na kuwaambia ni wakati wao wa kuhakikisha kuna kuwa na usalama eneo…

Soma Zaidi >>

UWT WILAYA YA ILALA WAFANYA USAFI CHANIKA HOSPITALI.

  Na Heri Shaaban,Dare es salaam. Umoja wa Wanawake (UWT) wilaya ya Ilala wamefanya usafi katika hospitali ya Mama na Mtoto (MCH) iliyopo Chanika Wilayani Ilala katika wiki ya maadhimisho ya siku ya Wanawake wa CCM yaliyofanyika leo tarehe 1, Octoba,2018. Katika ufunguzi huo Wanawake wa CCM ambapo UWT Wilaya ya Ilala walishiriki kazi za kijamii kwa kufanya usafi,kutembelea wodi ya Wanawake kugawa vitu mbalimbali katika hodi ya Wanawake. Akizungumza katika siku hiyo ya Wanawake Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ilala Amina Dodi aliwataka Wanawake wa Wilaya hiyo wasiwe nyuma…

Soma Zaidi >>

JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA MBUNGE BWEGE NA VIONGOZI WA CUF KILWA

Kilwa Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha ACT Wazalendo, Ado Sheibu, amesema amepokea taarifa hivi punde kuwa Mbunge wa Kilwa Kusini Seleman Bungara (Maarufu kwenye ulingo wa siasa kwa jina la Bwege) amekamatwa na Polisi huko Jimboni kwake Kilwa. Aidha amesema licha ya Mbunge huyo, pia wamekamatwa madiwani watano wa CUF, Katibu wa Mbunge, Deo Chaurembo, Mkurugenzi wa siasa wa CUF Kilwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilwa. Katika taarifa iliyotolewa na kiongozi huyo, imeeleza kuwa, madai ya Jeshi la polisi ni kwamba, Bwege hakutoa taarifa ya mkutano wake…

Soma Zaidi >>

CCM MKOA WA MWANZA YAENDESHA SEMINA YA USAJILI KUPITIA MFUMO WA DIJITI

Mwanza Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, leo kimeendesha semina ya kutoa mafunzo maalum kwa washiriki wa zoezi la uandikishaji wanachama wa chama hicho na Jumuiya zake tatu katika mfumo dijitali mtandao. Semina hii ya siku tatu imewakutanisha washiriki kutokea wilaya sita zikiwemo Nyamagana, Ukerewe, Magu, Misungwi, Kwimba pamoja na Sengerema. Akizungumza katika semina hiyo, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Nyamagana Salum Kalli amesema uandikaji uanachama kupitia mfumo mpya wa digitali ulianzia wilayani Ilemela ambao utawezesha mkoa wa Mwanza kuwa miongoni mwa mikoa minane nchini kuanza kutoa…

Soma Zaidi >>

WAZEE CHADEMA WAANIKA CHANGAMOTO ZAO!

Na Brighton Masalu,Dar es salaam. Baraza la wazee wa chaama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) limeainisha baadhi ya changamoto zinazowakabili wazee nchini, ikiwa ni pamoja na huduma za afya. Wakizungumza na waandishi wa habari mapema leo katika ofisi za makao makuu ya ofisi hizo Kinondoni jijini Dar es salaam,mwenyekiti wa baraza hilo, Hashim Juma Issa na katibu mkuu, Rodrick Lutembeka wamesema,wameamua kutumia siku hii ya wazee duniani, kuwasilisha maoni hayo kwa kile walichosema uzee ni hazina hivyo wasikilizwe na kulindwa. Aidha wameishauri serikali iweke utaratibu wa kuwalipa mafao wazee wote…

Soma Zaidi >>

MHE. MABULA AKABIDHI VITABU VYA SH.12 MILIONI SHULE YA SEKONDARI MKUYUNI

Nyamagana,Mwanza. Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanislaus Mabula kwa ushirikiano wa ufadhili wa taasisi ya SOS amekabidhi vitabu 452 vya Sayansi pamoja na masomo yenye michepuo ya Art na uchumi katika shule ya sekondari Mkuyuni vyenye thamani ya shilingi 12,000,000. Vitabu hivyo ni msaada kutoka taasisi hiyo ili kuimarisha sekta ya elimu wilayani Nyamagana. “Nawapongeza wadau wa maendeleo SOS kutoa vitabu 452 shule ya sekondari Mkuyuni msaada unaowezesha utekelezaji wa Sera ya elimu ya mwanafunzi mmoja Kitabu kimoja”amesema Mhe Mabula. Hafla hiyo imefanyika katika ziara maalum ya Mbunge Jimbo la…

Soma Zaidi >>

NAIBU WAZIRI WA NISHATI AWASHA UMEME VIJIJI VYA TONGA NA MAKOMBE PWANI

Chalinze,Pwani. Naibu Waziri wa Nishati,Mhe Subira Mgalu Septemba 30,2018 amewasha rasmi umeme katika vijiji vya Tonga na Makombe kata ya Chalinze, mkoani Pwani ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi ya REA na utekelezaji wake hapa nchini. Tukio hilo limeshuhudiwa na viongozi wandamizi kutoka REA, TANESCO, wakandarasi na wanachi. Akiwa kwenye ziara hiyo,Naibu Waziri wa Nishati,Mhe Subira Mgalu ametumia fursa hiyo kuwaasa wananchi kutumia kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) kwani hakihitaji mtandao wa umeme katika nyumba (wiring) na kinaharakisha huduma na gharama yake ni nafuu. “Wakati wa kuwasha…

Soma Zaidi >>

MADALALI WA KOROSHO KWA WAKULIMA WAPIGWA MARUFUKU MTWARA

Na Omary Hussein,Mtwara. Serikali wilayani Mtwara imewatahadharisha madalali wenye tabia za kuwalaghai wakulima na kununua Korosho kabla ya msimu kuanza kwa kuwataka kutafuta kazi nyingine za kufanya kwani katika msimu huu wa mwaka 2018-2019 kumewekwa utarabitu madhubuti kuhakikisha watakao ruhusiwa kuuza Korosho ni wakulima wenye mashamba yanayo tambulika katika wilaya hiyo. Kauli hiyo ya serikali imetolewa na mkuu wa wilaya ya Mtwara Mhe. Evod Mmanda wakati akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mtimwilimbwi Halmashauri ya mji Nanyamba waliojitokeza katika ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi. Akiwa…

Soma Zaidi >>