NILIWAHI KUJIITA MAGUFULI

Na Jyross Curtis Naibu wa Waziri wa Mambo ya Nje, Dr. Ndumbaro mapema leo hii akiwa Ikulu Jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuapishwa amefichua siri nzito ambayo aliokuwa ameificha kwa muda mrefu. Mara baada ya kuapishwa, amesema siku moja baada ya Dr. John Magufuli kupitishwa na CCM katika kuwania kiti cha Uraisi mwaka 2015, na yeye mbele ya watumishi wenzake aliamua kujiita ‘Magufuli’ “Siku ya pili yake tulikuwa na mkutano wa wanataaluma na wakati wa kujitambulisha, nilisimama na kujitambulisha kwamba naitwa Damas Ndumbaro Magufuli ” asema Dr. Ndumbaro.…

Soma Zaidi >>

MAMLAKA YA WANYAMAPORI WATAKIWA KUPIMA MAENEO YA HIFADHI.

  Ruvuma. Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mndeme amewaagiza mamlaka ya wanyapori,WWF,TFS na mamlaka zingine zinazosimamia maliasili na wanyapori Mkoani humo kupima maeneo ya hifadhi na kuyalinda ili yasivamiwe na majangili. Aidha amewataka wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kuwafichua wale wote wanaofanya vitendo vya kijangili katika maeneo ya hifadhi mkoani humo. Amewaasa wananchi wanaokaa karibu na hifadhi kuacha vitendo vya kula nyama ya Tembo kwa sababu ndio kichocheo cha ujangili katika maeneo ya hifadhi. Bi Mndeme,ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya Tembo Duniani yaliyofanyika ndani ya…

Soma Zaidi >>

DAS MPOGOLO ENDELEENI KUMUOMBEA RAIS MAGUFULI

Kitonga,Dar es Salaam Katibu Tawala wilaya ya Dodoma (DAS) Edward Mpogolo ameiomba Jumuiya ya Waislamu wa Ahamadiyya, kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Magufuli aendelee kufanya vizuri katika kuiongoza nchi na kuwatumikia wananchi. Kauli hiyo ameitoa mapema leo wakati alipokua katika mkutano huo wa mwaka wa 49 wa Jumuiya hiyo wakati akimuwakilisha mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema. “Endeleeni kumuombea Rais John Magufuli aendelee kufanya vizuri katika kuwatumikia wananchini, kwani dua zenu Allah atazisikia na atamshushia Malaika wa kumlinda ili asikwame” amesema DAS  Mpogolo Amesema…

Soma Zaidi >>

MBUNGE JIMBO LA NYAMAGANA KUWEZESHA KITUO CHA VIJANA SOS.

  Nyamagana,Mwanza. Mbunge Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula,akiwa ziarani katika taasisi ya SOS kwenye kituo chao cha Vijana Youth Center ameahidi kutatua changamoto zinazokabili kituo hicho ikiwemo uhaba wa viti na meza pamoja na ukamilishaji wa jengo la upasuaji. Mhe.Mabula Kwa upekee ameahidi kutoa ushirikiano kwa taasis hiyo ili kuwezesha kituo hicho kuwa cha mfano kwa kuwapatia washiriki na vikundi vyao mitaji kupitia mfuko wa jimbo pamoja na kusimamia fedha za halmashauri za mikopo bila riba kuwafikia ili kituo hicho kiweze kuhudumia mahitaji ya wilaya nzima. Akiwa kituoni hapo Mh.Mabula…

Soma Zaidi >>

WATENDAJI WIZARA YA MAMBO YA NJE WATAKIWA KUTEKELEZA ILANI YA UCHAGUZI.

  Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka watendaji na wakurugenzi wa wizara ya Mambo ya Nje kufanya kazi kwa uadilifu na kutekeleza ilani ya uchaguzi. Rais Magufuli amesema hayo leo Ikulu jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kumuapisha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa,Dkt. Damas Ndumbaro ambapo amesema ni wakati sasa kwa watendaji hao kushirikiana na kuhakikisha hawafanyi kazi kwa mazoea kwani wizara hiyo ni muhimu kwa nchi. “Lengo letu ni kuipeleka nchi yetu mbele,sitapenda kuona ama kusikia…

Soma Zaidi >>

WAZIRI WA NISHATI ATEMBELEA NA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA MIUNDOMBINU KATIKA MRADI WA STIEGLERS GORGE.

Pwani. Waziri wa Nishati Dkt. Medard. Kalemani Septemba 28, 2018 ametembelea na kukagua utekelezaji wa miundombinu wezeshi wa mradi wa maporomoko ya Mto Rufiji (Stieglers Gorge). Katika ziara hiyo Mhe. Kalemani ameagiza Taasisi zote zinazotekeleza ujenzi wa miundombinu hiyo kumaliza kazi hizo kufikia Oktoba 10 mwaka huu. Katika ziara yake hiyo Mhe. Waziri wa Nishati aliambatana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Japhet Hasunga, baadhi ya Wabunge kutoka Mkoa wa Pwani, Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na TANESCO. Mradi wa umeme wa Rufiji unatarajiwa kuzalisha jumla ya Megawati…

Soma Zaidi >>

RC RUVUMA KESHO KUFANYA ZIARA WILAYANI TUNDURU.

  Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme kesho atafungua msimu mpya wa korosho mkoani humo akiongozana na wakuu wa wilaya zote za mkoa wa huo katika ukumbi wa clasta wilayani Tunduru Aidha October 1 ataelekea Lukumbule tarafa ya lukumbule ,aidha akiwa anaelekea huko atapitia katika kata ya mtina kijiji cha mtina atawasalimia wananchi na kupata taarifa fupi ya mwenendo wa mradi wa maji wa mtina. Baada ya kupata taarifa fupi, ataelekea kata ya lukumbule ambako atatembelea mradi wa umeme unaojengwa na kampuni ya power corner ambao mpaka sasa unahudumia…

Soma Zaidi >>

UTOAJI HATI MILIKI ZA ARDHI TANZANIA WAONGEZEKA KWA KASI

Dodoma Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amesema kasi ya utoaji hati za umiliki wa ardhi na makazi imeongezeka kwa kasi ambapo hadi kufikia septemba mwaka huu 2018 jumla ya hati 25,463 zimeandaliwa. Akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa uwasilishwaji matokeo ya utafiti kuhusu haki na usalama na umiliki wa rasilimali ardhi na makazi jijini Dodoma,Mabula amesema jumla ya hati 17,680 zilikuwa zimewasilishwa ofisi za kanda kwa ajili ya usajili na hati 9,739 zimeshakamilika. Hata hivyo, naibu waziri huyo amesema pamoja na jitihada zinazofanywa na…

Soma Zaidi >>

WALIMU NA VIONGOZI WA KIJIJI WATAKIWA KUPUNGUZA UTORO MASHULENI

Longido Mbunge wa Jimbo la Longido Mhe Dr Steven Kiruswa ameendelea na ziara leo ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea katika jimbo hilo. Katika ziara hiyo, amekagua ujenzi wa tenki kubwa la maji unaondelea katika kata ya Gilai-Meirungoi na kuona namna ujenzi unavyoendelea. Mbunge alitembelea ujenzi wa shule mpya ya msingi ya kijiji cha Meirugoi kata ya Glai-Meirugoi unaondelea na kushirikiana na Mafundi kupanga mawe. Aidha amewahimiza viongozi wa kijiji cha Magadini pamoja na walimu wa shule ya msingi Magadini kutengeneza mkakati bora ili kupunguza utoro shuleni, na pia…

Soma Zaidi >>

MBUNGE JIMBO LA NYAMAGANA ATEMBELEA MIRADI 9 YA SOS

Nyamagana Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanislaus Mabula ameipongeza taasis ya SOS kuwa wadau muhimu wa maendeleo Wilayani humo katika nyanja za ujasiriamali , elimu, jamii, jinsia, watoto na vijana. Aidha miradi aliyotembelea katika Kata nne za Halmashauri ya Jiji la Mwanza, ni pamoja na mradi mkubwa wa malezi kwa watoto katika Kijiji Cha Malezi, shule ya awali ya SOS Kindergarten, Mradi wa Kituo cha vijana, mradi mkubwa wa ujenzi wa madarasa ya kisasa na ukarabati wa shule ya msingi na sekondari Igelegele.   Hata hivyo, Mabula ameshiriki zoezi la…

Soma Zaidi >>