JAFFO ALIA NA WATENDAJI WEZI KWENYE HALMASHAURI, AAGIZA UCHUNGUZI UFANYIKE HARAKA KUWABAINI

Waziri wa nchi ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo amesema Serikali imebaini wizi unaofanywa na baadhi ya watendaji wa halmashauri kwa kuchezea mifumo ya kielektroniki ya ukusanyaji fedha na mapato na kuagiza wakuu wa mikoa kuanza kufanya uchunguzi juu ya wahusika wa ubadhilifu huo ili wachukuliwe hatua za kisheria. Waziri Mhe.Jaffo amebainisha hayo wakati akifunga mkutano wa 34 wa Jumuiya ya tawala za mitaa Tanzania bara ALAT ambapo anasema hali hiyo, imeendelea kuikosesha mapato Serikali na kuathiri shughuli za maendeleo huku akionya wahusika…

Soma Zaidi >>

RC MTAKA AIPONGEZA GEITA KUFANYA  MAONESHO YA KIPEKEE YA DHAHABU NCHINI

Simiyu. Mkuu wa Mkoa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewapongeza viongozi wa Mkoa wa Geita wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhandisi. Robert  Gabriel kwa ubunifu waliofanya wa kufanya Maonesho ya Kipekee ya dhahabu hapa nchini. Mtaka ameyasema hayo mara baada ya kuzungumza na viongozi wa Mkoa wa Geita na kutembelea mabanda ya maonesho katika Maonesho ya Dhahabu yanayofanyika  Uwanja wa CCM Kalangalala Mjini Geita kuanzia Septemba 24, 2018. Amesema Watanzania wengi wamekuwa wakienda kushiriki maonesho ya dhahabu katika mataifa mbalimbali barani Afrika na nje ya bara la Afrika lakini kupitia maonesho haya Watanzania wameanza…

Soma Zaidi >>

DR. BASHIRU ATETA NA MWAKILISHI WA HESHIMA WA TANZANIA – HONG KONG

Dar es salaam Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dr. Bashiru Ally, leo amekutana na kufanya mazungumzo na mwakilishi wa heshima wa Tanzania huko Hong Kong na Macao nchini China Bi Annie Suk Ching Wu, ambapo wamejadili mambo mbalimbali kuhusu ufunguzi wa fursa mpya za kuwasaidia watanzania. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ofisi ndogo Lumumba Dar es Salaam, wameweza kujadili jinsinya kujisimamia kiuchumi, kufungua miradi ya ujasiria mali, fursa za masomo barani Asia, pamoja na nafasi za ajira na hususan katika kundi la vijana na wanawake. Aidha Dkt, Bashiru…

Soma Zaidi >>

RC CHALAMILA AMTAKA WAZIRI WA MAJI KUTUMA WAATALAM WA MAJI MATWIGA.

  Na Prakseda Mbulu.Mbeya. Mkuu wa mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amemuomba waziri wa maji na umwagiliaji Prof.Makame Mbarawa kutuma wataalamu wa maji katika mradi wa maji kata ya matwiga unaoonekana kuwa na kasoro nyingi na viashiria vya rushwa. Mradi wa maji katika bwawa la matwiga umeanza kubomoka,kujaa mchanga ndani ya bwawa pamoja na kukauka maji kitu ambacho amesema hawezi kuupokea mradi huo. RC Chalamila ametoa kauli hiyo september 27, 2018 katika kata ya matwiga wilayani Chunya alipotembelea kukagua mradi huo ambapo amesema ni vema wakapelekwa wataalam kutoka wizara ya…

Soma Zaidi >>

WAZIRI KIGWANGALLA AFANYA MAZUNGUMZO NA MJUKUU WA MALKIA WA UINGEREZA,PRINCE WILLIAM.

  Dar es salaam. WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amekutana na kuzungumza na Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku tatu. Prince William ambaye aliwasili nchini Septemba 26, 2018 kwa ziara maalum ambapo awali alikutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ikulu ya Magogoni Jijini Dar es Salaam, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na baadae kupokelewa ofisini kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, amesema kuwa amefurahia uwepo wake hapa nchini hali iliyopelekea kukaa kwa…

Soma Zaidi >>

SERIKALI YA TANZANIA YAPATA TUZO YA KIMATAIFA YA KUPAMBANA MA MAGONJWA YASIYO AMBUKIZA(NCDs).

  New York,Marekani. Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto imepata tuzo ya kimataifa ya kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza(NCDs) kama vile Kisukari,Shinikizo la Damu,Magonjwa ya Moyo na Saratani. Tuzo hiyo ya kimataifa,imekabidhiwa jana tarehe 27 Septemba,2018,kwa waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu na kikosi kazi maalumu cha Umoja wa Mataifa mahsusi kwa kupambana na Magonjwa Yasiyo ya kuambukiza (UN Interagency Task Force on the Prevention & Control of NCDs-UNIATF). Hii ni kutokana na juhudi za Wizara ya Afya za kupambana dhidi ya Magonjwa yasiyo…

Soma Zaidi >>

RC HAPI AAGIZA KAIMU MENEJA TANESCO IRINGA AWEKWE MAHABUSU

Na Francis Godwin Darmpya Iringa Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi ameliagiza jeshi la Polisi kumkamata na kumweka mahabusu masaa mawili kaimu Meneja wa Tanesco mkoa wa Iringa kwa kutoshiriki ziara yake. Hapi ametoa agizo hilo leo katika kijiji cha Kingonzile baada ya Diwani wa kata ya Nduli Bashiri Mtove kuwakilisha kilio cha wananchi wa kigonzile juu ya kuomba kusogezewa umeme . Kabla ya kujibu ombi la wananchi ambao walimsimamisha kutoa kilio hicho kupitia diwani wao ,mkuu wa mkoa alilazimika kumwita Meneja wa Tanesco ila hakuwepo na ndipo alipompigia…

Soma Zaidi >>

BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI LATOA MKONO WA POLE

Na Danson Kaijage,Dodoma Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki limetoa kiasi cha sh.milioni 8.5 kama sehemu ya rambirambi kutokana na kuzama kwa kivuko cha Mv.Nyerere na kusabaisha vifo vya watanzania 226 katika wilaya ya Ukerewe sehemu ya Ukara. Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Alhaji Adam Kimbisa Akikabidhi rambirambi hiyo kwa Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, kwa niaba ya Spika wa Bunge Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk.Martin Ngoga, Kimbisa amesema kuwa Bunge hilo limeamua kutoa pole kwa watanzania pamoja na familia zilizopoteza ndugu zao. Amesema kuwa,…

Soma Zaidi >>

ZIARA YA MTAA KWA MTAA YA MBUNGE WA NYAMAGANA INAENDELEA

Nyamagana,Mwanza. Ziara ya mtaa kwa mtaa ya mbunge wa jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula imeendelea ikiwa na dhima ya kusikiliza na kutatua changamoto za kudumu kwa jamii. Mhe Mabula amefanikiwa kutembelea mitaa ya Mwalukila,Sahwa,Igwambiti A na C pamoja na mtaa wa Shibula ambapo amejionea adha waliyoyonayo wananchi juu ya maeneo ya kusitiri watu katika nyumbani zao za milele(MAKABURI). Akiwa ameambatana na wataalamu wa ardhi,mhe Mabula pia ametembelea maeneo yote yaliyorasimishwa katika mfumo rasmi na kuangalua maeneo mbadala yatakayofaa kwaajili ya makaburi ambapo amebaini eneo la wazi zaidi ya mtaa…

Soma Zaidi >>

PIGO LINGINE KWA CHADEMA,MBUNGE WAO ATIMKIA CCM

Serengeti,Mara. Mbunge wa jimbo la Serengeti,Marwa Ryoba Chacha kupitia tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) ametangaza kukihama chama hicho na kujiunga na chama cha mapinduzi(CCM). Akitangaza uamuzi huo usiku wa september 27 katika manispaa ya Musoma Mkoani Mara Mhe. Chacha amesema hajashawishiwa na mtu yoyote kuhama bali ameamua kwa hiyari yake kuhamia CCM ili kuunga mkono juhudi za rais wa awamj wa tano Dkt.John Pombe Magufuli. Amesema wananchi wa Serengeti walimpa imani kubwa ya kuwatumikia hivyo ameona kama hawatendei haki akiwa ndani ya CHADEMA. “Nawaomba wananchi wa Serengeti,mlinipa Imani…

Soma Zaidi >>