RC:CHALAMILA,ATAKAYEVURUGA AMANI KIPINDI CHA UCHAGUZI WA MARUDIO MBEYA KUKIONA.

  Na Prakseda Mbulu, Mbeya. Mkuu wa mkoa wa Mbeya mh!Albert Chalamila amewataka wananchi kushiriki uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata nne,pasipo vitendo vya uvunjifu wa amani. Amesema hayo 14, september 2018,wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake,ambapo amesema amani aliyoikuta mkoani Mbeya atahakikisha anaiendeleza na hatakubali kikundi cha watu wachache waivuruge. Chalamila amesema hayo baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa kuna baadhi ya vikundi vimeletwa mkoani Mbeya kwaajili ya kuwatisha wananchi ili wasijitokeze kupiga kura kwa kuingiwa na hofu ya usalama wa maisha yao. “Nasikia kuna baadhi ya…

Soma Zaidi >>

PROF NDALICHAKO AKABIDHI GARI IDARA YA ELIMU PANGANI.

Pangani Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Pangani chini ya Mh Zainab Abdallah, kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Pangani Mh Jumaa Aweso wamefanya mazungumzo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Ndalichako na kukubaliana mbalimbali ikiwa ni muendelezo wa ziara ya Sekta kwa Sekta ndani ya jiji la Dodoma. Baada ya Ofisi ya mkuu wa Wilaya kupeleka madai ya Idara ya Elimu kukosa gari,kumelekea ufuatiliaji na ufanisi wa utendaji kazi katika sekta ya elimu, Prof Ndalichako ameahidi kuwapatia gari kwa ajili ya usafiri huo, ambapo amewaagiza wataalam wa…

Soma Zaidi >>

MBUNGE JIMBO LA NYAMAGANA AFADHILI JEZI ZA WAAMUZI LIGI DARAJA LA NNE

Nyamagana Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanislaus Mabula, amekabidhi Jezi na Vitini vya Uwamuzi vyenye thamani ya shilingi 500,000 kwaajili ya waamuzi wanaoshiriki kuendesha michuano ya kombe la ligi daraja la nne wilayani Nyamagana chini ya usimamizi wa NDFA”Nyamagana District Football Association” kwa mwaka 2018. Akizungumza kwa niaba ya Mbunge Jimbo la Nyamagana, Mwenyekiti wa taasis ya First Community, Ahmed Misanga, amesema Jezi na vitini hivyo vya uwamuzi ni mwendelezo wa ahadi ya Mhe. Mabula kufadhili kikamilifu ligi daraja la nne wilayani humu ikiwa ni ahadi moja wapo aliyoitoa wakati…

Soma Zaidi >>

JENISTA MHAGAMA ATOA ONYO KWA BODI YA PSSSF

Danson Kaijage, Dodoma WAZIRI wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama, jana ametangaza hali ya hatari kwa wajumbe wa bodi ya mfuko wa hifadhi ya jamii (PSSSF) ambapo imetumika nguvu nyingi kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa miwili, hivyo hatakubali kuona mfuko huo unakuwa na ubadhilifu wa aina yoyote. Mhagama ametoa tishio hilo, wakati wa hafla ya kuzindua bodi ya wadhanini wa Hifadhi ya mfuko wa Jamii iliyofanyika Jijini Dodoma, pamoja na kuwatambulisha wajumbe wa bodi hiyo, ambapo amesema, ikitokea Mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa Hesabu…

Soma Zaidi >>

MWENGE WA UHURU:MONDULI WAHAMASISHWA UFUGAJI KWA NJIA ZA KISASA.

Mwenge wa uhuru umetembelea Shamba la mifugo la Manyara (Manyara ranchi) lililopo wilayani Monduli mkoani Arusha ambapo kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Ndg:Charles Kabeho amewataka wafungaji kufuga kwa kutumia mbinu za kisasa ambazo hazi athiri mazingira na zenye kuleta tija kwa jamii na taifa kwa ujumla. Kabeho amesisitiza hilo mara baada ya kukagua shamba la mifugo Manyara ranchi lenye ukubwa wa ekari 45000 lililoanzishwa mnamo mwaka 1959 na muekezaji kutoka Ujerumani ambapo kwa sasa shamba hilo lilotolewa na serikali na kumilikishwa kwa wananchi wa vijiji vya Esilalei na…

Soma Zaidi >>

POLEPOLE:CHADEMA ACHENI MATUSI NA KUTUMIA VIONGOZI WA DINI KWENYE KAMPENI

John Marwa@darmpya.com Dares Salaam Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimesikitishwa sana na kitendo cha viongozi wa dini kufanya kampeni za kumnadi mgombea wa CHADEMA, tena kiongozi huyo akatoa lugha chafu dhidi ya mgombea wetu wa CCM. Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu mwenezi wa Chama hicho, Hamphrey Polepole wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwendendo wa kampeni kufutia uchaguzi wa marudio wa majimbo na kata . Amesema kuwa, wao kama chama tawala hawawezi kutumia dini kwenye majukwaa yao maana tunaheshimu sheria inayokataza mambo hayo…

Soma Zaidi >>

SALUFU:VIONGOZI WASIOWAJIBIKA CCM WATUPISHE

Na Francis Godwin,Darmpya Iringa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa chama cha mapinduzi ( CCM) wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Yohanes Salufu amewataka viongozi wa vitongoji na vijiji wa CCM ambao wanashindwa kutekeleza majukumu yao kujitathimini na kuachia nafasi hizo. Ameyasema hayo, leo wakati wa kikao cha viongozi wa CCM juu ya ufuatiliaji wa ilani ya CCM katika kata ya Nyalumbu, ambapo amesema CCM imejipanga kuona inaendelea kuchukua dola na haiwezekani kama viongozi wa CCM ngazi za chini wakawa kikwazo kwa wananchi na chama. Aidha amesema, lazima viongozi hao kufanya…

Soma Zaidi >>

FAHAMU UMUHIMU WA TANGAWIZI KATIKA MWILI WA BINADAMU.

  Tangawizi ni nini? Tangawizi ni kiungo ambacho kinatokana na mizizi ya mmea wa Tangawizi. Mmea huu unafanana sana na Binzari ikiwa bado haijamenywa maganda yake. Pia  bidhaa hii inapatikana nchi nzima kwa bei nafuu kabisa na kila mtu mwenye uwezo wowote wa kiuchumi anaweza kununua aidha kwa kipande kimoja, fungu au kwa kilo pia. Zifahamu faida/umuhimu wa Tangawizi. Husaidia kupunguza kama si kuondoa kichefuchefu ni nzuri haswa kwa wale wanawake wenye mimba changa ambao husumbuliwa kutapika. Husaidia wale wenye matatizo ya gauti yaani sehemu ya viungo kuuma na kusikia…

Soma Zaidi >>

UPINZANI BADO HALI TETE, MWINGINE ATIMKIA CCM

Na Danson Kaijage,Chamwino LICHA ya wadau mbalimbali pamoja na viongozi wa Dini kukerwa na hamahama ya wanasiasa kutoka chama kimoja na kuingia chengine na kusababisha kurudiwa kwa uchaguzi mdogo bado mchezo huo unaendelea. Hali hiyo imetokea juzu baada ya aliyekuwa Diwani wa Chadema kata ya Chinugulu wilaya ya Chamwino, Amosi Henely Fumaa kuondoka Chadema na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM). Diwani huyo ambaye pia alikuwa wa Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Mtera, ametangaza kujiuzulu nafasi zote kwa madai kuunga mkono kazi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano. Akizungumza…

Soma Zaidi >>