“BENKI YA NMB KUUNGA MKONO JITIHADA ZA MAENDELEO KISARAWE”

MKUU WA WILAYA YA KISARAWE NA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA KISARAWE WAPANGA MKAKATI WA MAENDELEO WILAYA YA KISARAWE KWA KUSHIRIKIANA NA BENKI YA NMB.   Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Bi. Jokate Mwegelo, pamoja na Mussa Gama, Mkurugenzi wa Wilaya ya Kisarawe, wamefanya kikao muhimu cha ushirikiano katika Maendeleo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji (Managing Director & CEO) wa Benki ya NMB Tanzania, Bi. Ineke Bussemaker, akiongozana na Kiongozi wa Mahusiano ya Kibenki na Serikali (Head of Government Banking), Bibi Vicky P. Bishubo. Kikao kiliangazia maeneo makubwa matatu ambayo ni Elimu,…

Soma Zaidi >>

KAMPUNI YA GREEN MILES YAAGIZWA KUINGIA MIKATABA NA VIJIJI VILIVYOPO KWENYE KITALU CHAKE.

Longido,Arusha. Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Longido limeaiagiza kampuni ya uwindaji ya Green Miles kuingia mikataba na wananchi waliopo katika vijiji vilivyopo katika kitalu chake. Maagizo hayo yametolewa 13 September 2018,wakati wa kikao cha kawaida cha madiwani hao. Baraza hilo la madiwani chini ya mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Sabore Molloimet na mkurugenzi mtendaji, Jumaa Mhina,limepokea Taarifa za Kamati za kudumu za halmashauri fedha,utawala na mipango, kamati ya elimu, afya na maji, Kamati ya uchumi, ujenzi na mazingira na Kamati ya kudhibiti Ukimwi ambapo masuala mbalimbali yamejadiliwa ikiwemo…

Soma Zaidi >>

MWENGE WA UHURU WAWANUFAISHA WANANCHI WA KARATU.

Ikiwa ni siku ya pili tangu mwenge wa uhuru kupokelewa ukitokea mkoa wa Mara hatimae Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka amekabidhi Mwenge wa uhuru kwa mkuu wa wilaya ya Karatu Theresia Mahongo kwa ajili ya kuendelea na majukumu ya mwenge wilayani humo. Baada ya kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Ndg:Charles Francis Kabeho kukamilisha ziara ya mwenge wilaya ya Ngorongoro ambapo katika wilaya hiyo amewaagiza wakuu wa idara ngazi ya wilaya na halmashauri kuwa na nidhamu ya fedha za maendeleo na kuhakikisha wanawashirikisha viongozi wengine katika…

Soma Zaidi >>

KANUNI MPYA ZA MATUMIZI YA GESI KUONGEZA GHARAMA KWA WATUMIAJI.

Kanuni mpya za matumizi ya huduma za gesi za majumbani zinazotarajiwa kuanza kutumika hivi karibuni zimepigiwa kelele na wadau wa maswala ya gesi kwa kile ambacho kinaonekana ni kuwatwisha mzigo watumiaji wa mwisho wa nishati hii muhimu sana katika maisha ya kila siku ya mwananchi. Hayo yamesemwa leo katika mkutano wa wadau ulioitishwa na mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati nchini EWURA ukihusisha wadau mbalimbali wa sekta ya gesi wakiwemo wamiliki wa makampuni yanayohusika na uuzaji na usambazaji wa gesi hapa nchini pamoja na watumiaji wa kawaida wa gesi…

Soma Zaidi >>

CCM YAJIHAKIKISHIA USHINDI VINGUNGUTI, NGOME YA UPINZANI YAANGUKA

Dar es Salaam Wenyeviti saba wa Serikali za mtaa kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) na Chama cha Wananchi (CUF) kata ya Vingunguti wamejivua nyadhifa zao na kujiunga na chama cha Mapinduzi (CCM ) kwa lengo la kumuunga mkono mgombea udiwani wa kata hiyo, Omary Kumbilamoto. Wenyeviti hao, wametoa uamuzi huo katika mkutano wa kampeni wa kugombea udiwani, uliofanyika Relini ambapo wakizungumza baada ya kukabidhi kadi zao kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM ) mkoa, Kate Kamba wamesema wameamua kufanya hivyo baada ya kuchoshwa na…

Soma Zaidi >>

DC MURO AZINDUA KAMPENI YA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI.

Mkuu wa Wilaya Arumeru, Jerry Muro hii leo amezindua kampeni maalum ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi itakayodumu kwa siku saba na kuhusisha wataalam kutoka serikalini na taasisi za kisheria kutoka halmashauri zote mbili zinazounda wilaya hiyo ya Arumeru. Wananchi Mbalimbali wameendelea kujitokeza ikiwa ni Siku ya Kwanza ya Kuanza Kwa Zoezi la Kusikiliza Changamoto zinazowakabili Wananchi wa Wilaya hiyo. Zoezi Hilo lililopewa jina la papo kwa hapo limewakusanya Pamoja Wanasheria mbalimbali kutoka Mkoa wa Arusha pamoja na Wakuu na Watendaji wa Halmashauri Za Arusha Na DC Meru. Miongoni…

Soma Zaidi >>

HICHI NDICHO ALICHOKISEMA OMMY DIMPOZ KWENYE SIKU YAKE YA KUZALIWA

    Msanii maarufu nchini wa muziki wa bongo fleva, Ommy Dimpoz kupitia ukurasa wake wa instargram amesema namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumjalia kuuona mwaka mwingine licha ya majaribu mengi alioyapitia kwa kipindi cha miezi mitano iliopita. “Leo 13th September ni kumbukumbu yangu ya siku ya kuzaliwa. Namshukuru sana Mwenyezi Mungu (ALHAMDULILAAH) kwa kunipa nafasi ya kuuona mwaka mwingine, kwani niliyoyapitia katika kipindi cha takribani miezi 5 kama ingekuwa sio mapenzi yake yeye (M/Mungu) basi ingekuwa imebaki history” – Ommy Dimpoz Ameseam kuwa, alichojifunza kipindi hicho chote ni kuwa kuumwa…

Soma Zaidi >>

CHADEMA YAMVUA UANACHAMA KIONGOZI WA MTAA KWA UBADHIRIFU WA FEDHA ZA UMMA

GEITA. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Geita Mjini kimemvua uanachama Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Moringe anayetokana na chama hicho, Bw Adrian Rwechungura, kutoka kata ya Buhalahala mkoani Geita kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma. Katika taarifa iliyotolewa na Jana Septemba 12, 2018 na Katibu wa Chadema jimbo la Geita Mjini, ndugu Kangeta Ismail, imesema kuwa kiongozi huyo wa serikali amejihusisha na ubadhirifu wa fedha za umma za mtaa wa Moringe, pamoja na matumizi mabaya ya madaraka katika utendaji wake hapo mtaani. Mbali na…

Soma Zaidi >>

UVCCM YAKOLEZA KASI YA USHINDI WA CCM MONDULI

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wameendelea kuongeza kasi ya ushindi wa (CCM) katika Jimbo la Monduli kwa kukutana na kuwajengea hamasa vijana kutoka makundi mbalimbali kama vile wajasiriamali, wafanyabiashara wa ndizi, wachonga vinyago, madereva bodaboda na bajaji, wanamichezo na wananchi wa rika zote katika jamii kwa kuwataka kumchagua Ndugu Julius Kalanga siku ya Jumapili tarehe 16/09/2018 kwa tiketi ya CCM kuwa mbunge wa Monduli. Aidha (UVCCM) imewataka vijana na wananchi wengine kuelewa, Julius Kalanga ana uwezo wa kuwawakilisha vizuri bungeni na anatoka katika chama kimoja na Mhe Rais…

Soma Zaidi >>

YONDANI AREJEA,JUMA MAHADHI MAMBO BADO MAGUMU

Daktar wa kikosi cha Young Africas Dk.Edward Bavu amethibitisha mchezaji Kelvin Yondani amepona majeraha yake na siku ya jana Jumatano ameanza rasmi mazoezi. Yondani alipata majeraha akiwa na kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ambapo majeraha hayo yamfanya aondolewe katika kikosi cha timu ya Taifa kilichokwenda nchini Uganda. Yondani anatarajiwa kuwa sehemu ya Kikosi cha Yanga kitakachoumana dhidi ya Standi United Jumapili katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Saa 10:00 Jioni. Aidha Dk.Edward Bavu amesema wachezaji wengine waliokuwa majeruhi na siku ya jana walianza kufanya mazoezi pamoja na…

Soma Zaidi >>