“WORLD VISION” YABORESHA SEKTA YA ELIMU KARATU.

Inakadiriwa wanafunzi zaidi ya 2000 wilayani Karatu mkoani Arusha waliopo darasa la kwanza hadi La Tatu hawajui kusoma na kuandika hii ni Sawa na asilimia nane ya wanafunzi wote. Kwa mujibu wa shirika la elimu duniani (UNESCO) Idadi hiyo ni Miongoni wa watoto milioni 264 na watu Wazima milioni 759 Walio nje ya mfumo wa Elimu wanaokosa Stadi za msingi za usomaji. Bi. Theresia Mahongo ni Mkuu wa wilaya ya karatu amebainisha hayo katika maadhimisho ya siku ya usomaji duniani yaliyoandaliwa na shirika la world vision ambapo amesema kiwango hicho…

Soma Zaidi >>

DKT MASHINJI:KAULI YA BAZECHA SIO KAULI RASMI YA CHAMA,HAYO NI MAONI YAO BINAFSI.

  Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Dakta Vincent Mashinji, amesema kuwa kauli iliyotolewa na Baraza la wazee wa chama (BAZECHA), sio kauli rasmi ya chama hicho bali ni matamanio binafsi ya wazee hao. Dkt Mashinji amesema hayo leo Septemba 11, 2018 kufuatia maombi ya BAZECHA kumkaribisha Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) taifa, Seif Sharif Hamad, kuhamia Chadema ili kuwania Urais kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika mwaka 2020. Katibu mkuu huyo (wa Chadema), ameongezea kuwa kauli ya wazee…

Soma Zaidi >>

TCRA KUWAKAMATA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI VINAVYOENDELEA KURUSHA HABARI NA HUKU VIKIWA HAVIJASAJILIWA.

Dodoma. Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), imesema ipo mbioni kuwachukulia hatua za kisheria wamiliki wa mitandao ya kijamii ya ‘Blogs, tovuti, TV online’ ambao wanaendelea kuweka habari kwenye mitandao yao huku hawajasajiliwa kuendelea kufanya kazi hiyo. Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 11, 2018 na Mhandisi wa TCRA Makao Makuu, Eng. Francis Mihayo, wakati akizungumza katika semina kwa wadau mbalimbali wa mawasiliano iliyoandaliwa na mamlaka hiyo jijini Dodoma. Eng Mihayo akizungumza na wadau waliohudhuria semina hiyo, amesema wapo baadhi ya wamiliki wa mitandao hiyo wamekaidi kutii agizo la serikali kupitia TCRA…

Soma Zaidi >>

MWENGE WA UHURU KUWASILI ARUSHA SEPT 12, ZAIDI YA MIRADI 20 KUZINDULIWA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo anatarajiwa kupokea Mwenge wa uhuru septemba 12 wilayani Ngorongoro ukitokea mkoani Mara, ambapo zaidi ya miradi 20 inatarajiwa kuzinduliwa. Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa baada ya kuupokea mwenge huo viongozi wa serikali watakao ambatana na kiongozi wa mwenge wanatarajiwa kuzindua miradi zaidi ya 20 ya maendeleo katika wilaya ya Ngorongoro,Karatu,Monduli,Longido,Arumeru, pamoja na wilaya ya Arusha mjini Katika kuelekea Tanzania ya viwanda Baadhi ya miradi inayi tarajiwa kuzinduliwa ni miradi kwa ajili ya kuboresha Sekta ya afya,Elimu,pamoja na miundo…

Soma Zaidi >>

CHADEMA YAMKARIBISHA MAALIM SEIF, KUWANIA URAIS ZANZIBAR.

John Marwa@darmpya. com Dar es Salaam. Baraza la Wazee wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (BAZECHA), limesema lipo tayari kumkaribisha Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Sharif Hamad, kuwania Urais wa Zanzibar kupitia chama hicho. Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 11, 2018 na Mwenyekiti wa Baraza la wazee Chadema, Bw Hashim Jumaa Issa, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu hali ya kisiasa nchini. Akizungumza na waandishi wa habari Bw. Juma, amesema kuwa kutokana na mgogoro unaoendelea ndani ya chama cha CUF, wameona kuna…

Soma Zaidi >>

MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI BAADA YA KUKAIDI AMRI YA JWTZ

Bagamoyo, PWANI. Mwananchi mmoja mkazi wa mji wa Bagamoyo mkoani Pwani, ambaye jina halijafahamika amefariki baada ya kupigwa risasi akidaiwa kukaidi amri ya wanajeshi wakati akiingia kambi ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) iliyopo Bagamoyo. Tukio hilo la simanzi limetokea usiku wa kuamkia leo Septemba 11, 2018, kwenye kambi hiyo ya JWTZ ijulikanayo kama Mapinga Comprehensive Training Centre (CTC) katika kata ya Mapinga wilayani humo. Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa, amekiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtu huyu alipigwa risasi baada ya kuingia ndani ya kambi hiyo…

Soma Zaidi >>

MAHAKAMA YATENGUA UAMUZI WA CHADEMA KUMFUTA UANACHAMA DIWANI WA MAJENGO MJINI

Sumbawanga, RUKWA. Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Rukwa, imetengua uamuzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Rukwa, wa kumfuta uanachama na kumvua udiwani, Dickson Mwanandenje, aliyekuwa diwani wa kata ya Majengo Mjini wilayani Sumbawanga. Maamuzi hayo, yametolewa leo Septemba 11, 2018 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Rozaria Mugisa, baada ya upande wa mlalamikaji ukiongozwa na Wakili wa kampuni ya Budodi Advocates Zonal Law Chambers, Mathias Budodi, kuwasilisha hati ya dharura mahakamani hapo. Diwani huyo alituhumiwa kuwa msaliti ndani ya Chadema, akidaiwa kupanda jukwaani Agosti…

Soma Zaidi >>

CIA KUZINDUA MASHAMBULIZI YA NDEGE ZISIZO NA RUBANI DHIDI YA WANAJIHAD LIBYA.

Niamey, NIGER. Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA), linatarajia kuzindua mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu wa Al-Qaeda na kundi la Islamic State nchini Libya. Mashambulizi hayo yatatekelezwa kutoka kambi mpya ya kijeshi kaskazini mashariki mwa Niger, gazeti la New York Times limearifu leo. Kwa mujibu wa gazeti hilo la kila siku la Marekani likinukuu maafisa wa Nigeria na Marekani, operesheni za upelelezi zilifanyika kwa miezi kadhaa kutoka uwanja wa ndege mdogo wa Dirkou, ambapo usalama umeimarishwa tangu mwezi Februari mwaka huu. Akihojiwa na gazeti…

Soma Zaidi >>

NAIBU MKUU WA MAJESHI NCHINI COMORO AKAMATWA

Moroni, COMORO Naibu Mkuu wa majeshi nchini Comoro, Kanali Ibrahim Salim, amekamatwa kuhusiana na uchunguzi kuhusu jaribio la njama dhidi ya Rais Azali Assoumani, kwa mujibu wa familia yake. “Majira ya mchana siku ya jana Jumatatu, wanajeshi wawili walikuja na kibali wakimwomba Kanali Ibrahim Salim kufika kwenye kituo cha polisi kwa kesi inayomhusu kesi, “Alirudi karibu saa 11 jioni, akabadilisha nguo na kuondoka. tulipata taarifa kwamba alikuwa amezuiliwa katika jela la Moroni.” Mshirika wake wa karibu ambaye hakutaja jina lake ameliambia shirika la Habari la AFP. Kulingana na ndugu zake,…

Soma Zaidi >>

LULA AAPA KUPAMBANA DHIDI YA UAMUZI WA MAHAKAMA KUTOWANIA URAIS

  Brasilia, BRAZIL. Rais wa zamani wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, ambaye anatumikia kifungo cha miaka 12 kwa madai ya rushwa tangu mwezi Aprili mwaka huu, ataendelea na vita yake ya kisheria ili arejeshewe haki ya kuwania katika uchaguzi wa urais mwezi ujao, wanasheria wake wamesema. Tangazo hili linakuja wakati chama chake cha PT, kimepewa siku chache ambazo mwisho ni leo Jumanne usiku kuteua mgombea mwengine kuchukua nafasi ya Lula kuelekea uchaguzi wa Oktoba 07. Mwishoni mwa mwezi Agosti, Mahakama Kuu ya Uchaguzi ilitangaza kwamba Lula hana vigezo…

Soma Zaidi >>