LHCR:UKATILI KWA WATOTO UMEONGEZEKA MARA TATU IKILINGANISHWA NA MWAKA JANA

Dar es Salaam. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania (LHRC), kimesema matukio ya watoto wanaliobakwa imeonekana kuongezeka maradufu ikilinganishwa na nusu ya kwanza ya mwaka 2017, ambapo watoto wa kike 259 tu ndio waliobakwa. Hayo yamesemwa hivi leo Agosti 31, 2018 Jijini Dar es salaam, na Mtafiti Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Fundikira Wazambi, wakati alipokuwa akiwasilisha Ripoti ripoti ya haki za binadamu nchini kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2018. Bw. Fundikira Wazambi amebainisha kuwa jumla ya watoto wapatao 2365 wamebakwa kutoka mwezi Januari…

Soma Zaidi >>

SHIRIKA LA UTU WA MTOTO ‘CDF’ LAWATILIA MKAZO WANAHABARI KURIPOTI MATUKIO YA UKATILI

Dar es Salaam. Shirika la Jukwaa la utu wa mtoto (CDF), limewataka waandishi wa habari nchini, kutilia mkazo katika kuripoti habari za ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto ili kuokoa gharama za kuwasaidia waathirika wa tukio hilo. Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam mapema leo Agosti 31, 2018 na Mkurugenzi wa shirika (CDF) hilo, Koshuma Mtengeti, wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari ya kuwajengea uwezo wa kuripoti matukio ya ukatili, ambayo yamedhaminiwa na shirika la maendeleo la sweden (Sida). Amesema kuwa, gharama za…

Soma Zaidi >>

MAVUNDE AIPONGEZA SEKTA BINAFSI KWA MCHANGO WA KUKUZA SEKTA YA VIWANDA NA FURSA YA AJIRA

Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde, ameishukuru Sekta Binafsi kwa mchango wao mkubwa inaoitoa katika Sekta ya Uchumi wa Viwanda na Fursa za Ajira inazozitengeneza kupitia uwekezaji. Mavunde ameyasema hayo leo Agosti 31, kwenye uzinduzi wa muonekano mpya wa kinywaji kikali cha K-VANT katika Hotel ya Serena Jijini Dar es salaam, ambapo ameipongeza kampuni ya Mega Beverages kwa kutoa fursa za ajira kwa wananchi zaidi ya 1000. Aidha, katika suala la uwekezaji Mavunde ameitaka kampuni hiyo (Mega Beverages), kuzalisha…

Soma Zaidi >>

SERIKALI YAWATAKA WAGANGA TIBA ASILI KUSAJILI VITUO VYAO NA DAWA WANAZOTENGENEZA

Dodoma. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amewataka Waganga wa Tiba asili nchini kuzingatia sheria na kanuni za kutoa huduma za Tiba Asili ikiwemo kujisajili, kusajili Vituo vyao vya kutolea Huduma pamoja na kusajili Dawa wanazozitengeneza. Taumko hilo amelitoa leo Agosti 31, wakati alipotembelea Kliniki ya Tiba Asili ya Golden Sanitarium iliyopo Jijini Dodoma, katika kuadhimisha Siku ya Tiba Asili ya Mwafrika, na kusema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya itaendelea kuhakikisha kuwa Tiba Asili ya Tanzania inaboreshwa na kuendelezwa hasa katika kuhakikisha Huduma…

Soma Zaidi >>

HUKO AMERIKA NCHI 03 ZAOMBA MSAADA KUKABILIANA NA WAKIMBIZI

Nchi tatu za Kusini mwa Amerika, Colombia, Peru na Ecuador zinaomba msaada zaidi wa kimataifa ili kukabiliana na ongezeka la wahamiaji kutoka Venezuela ambao wanazidi idara zao za huduma kwa umma, mwakilishi wa Peru amesema baada ya mkutano wa pamoja huko Lima kuhusu wahamiaji. Nchi hizi tatu zimepokea mamia ya maelfu ya Wavenezuela wanaokimbia mdororo wa kiuchumi na kisiasa nchini mwao, ambako raia wamekua wakijiwezesha wenyewe kwa kupata chakula na kuondokana na matatizo ya maisha ya kila siku. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, Wavenezuela zaidi ya Milioni 1.6, wameitoroka…

Soma Zaidi >>

WATU 18 WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA HELIKOPTA ETHIOPIA

Oromo, ETHIOPIA. Watu kumi na nane wamepoteza maisha katika ajali ya helikopta ya kijeshi iliyotokea katika mkoa wa Oromo, kusini mwa mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa. Tukio hilo limetokea jana Alhamis, ambapo watu wote waliokuwa ndani ya helikopta hiyo (wajeshi 15 na raia wa kawaida watatu), wamepoteza maisha katika ajali hiyo. “Helikopta hiyo, ambayo ilikuwa ya Wizara ya Ulinzi, ilianguka wakati ilikua ikijaribu kupaa angani kutoka Dire Dawa, kaskazini-magharibi mwa Ethiopia, kwenda Bishoftu (kilomita 40 kusini-mashariki mwa Addis Ababa) na ilikua na watu 18.” Televisheni Fana BC imeripoti. Hata…

Soma Zaidi >>

KUMI NA MOJA WAUAWA KATIKA SHAMBULIZI LA KUJITOA MHANGA IRAQ

Baghdad, IRAQ. Watu wasiopungua kumi na moja (11) wameuawa, ikiwa ni pamoja na maafisa wa usalama, katika shambulizi la kujitoa mhanga katika kituo cha Qaïm, mji ulio kwenye umbali wa kilomita 340 magharibi mwa Baghdad, kwa mujibu wa polisi.   Shambulizi hilo lililotokea mapema Agosti 29 liliwajeruhi maafisa watano wa usalama na raia 11, Mahmoud Jassem aliwaambia waandishi wa habari. Askari wawili na maafisa watatu wa Hashd al-Shabi, kundi lililosadia jeshi kulitimua kundi lenye msimamo mkali wa kidini la Islamic State (IS), ni miongoni mwa watu waliouawa. Vikosi vya Serikali…

Soma Zaidi >>

HATIMAYE RIEK MACHARI AKUBALI KUSAINI MKATABA WA AMANI SUDAN KUSINI

Juba, SUDAN KUSINI. Kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini Riek Machar hatimaye amekubali kutia saini mkataba wa amani na serikali. Tangazo hilo lilitolewa jana Alhamisi, Agosti 30 huko Khartoum, mji mkuu wa Sudan, nchi ambayo inasimamia usuluhishi. Mkataba wa amani ulikuwa tayari umeidhinishwa na serikali ya Sudan Kusini. Mkataba huu utasaidia kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimesababisha vifo vya watu wengi nchini humo tangu mwaka 2013. Hatimaye upatanishi wa serikali ya Khartoum umezaa matunda, hivi leo Agosti 31 mjini Juba nchini Sudan Kusini, kutokana na hatua hii ya…

Soma Zaidi >>

DC KIZIGO AKITAKA CHAMA CHA WALIMU KUSIMAMIA CHANGAMOTO ZAO

Mkuu Mpya wa Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Mh Sophia Kizigo, amekitaka Chama cha walimu Tanzania (CWT) wilayani humo, kuelewa kazi yake ni kutetea maslahi ya walimu sio chama cha wanaharakati wala siasa. Amesema kuwa, Serekali inatambua changamoto mbalimbali zinazowakabili zikiwemo upandaji wa madaraja na madai mengine,ambapo amewatoa hofu kuwa madai yao yanashughulikiwa Hata hivyo,amewahidi kwamba wataendelea kuboresha mazingira yao ya kazi ikijumuisha na miundombinu,huku akidai katika moja ya ziara alizozifanya, wazazi walilalamika kuhusu adhabu kali zinazotolewa kwa wanafunzi shuleni. “Mfano adhabu ya kuwafyatulisha wanafunzi matofali 1000 wanapofanya makosa, hili…

Soma Zaidi >>