RIEK MACHAR AGOMA KUSAINI MKATABA WA MWISHO WA AMANI

Juba, SUDAN KUSINI. Kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini, Riek Machar, amekataa kutia saini mkataba wa amani na serikali, mkataba ambao ulikuwa usainiwe kwa lengo la kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vingi nchini humo. Mkataba huo unajulikana kama ‘mkataba wa amani wa mwisho’ uliokuwa umepangwa kusainiwa Agosti 28, 2018 na viongozi hao mahasimu na makundi mbalimbali mjini Juba. Sudan Kusini ni nchi changa duniani inayoendelea kukabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, kwa mujibu wa mpatanishi wa Sudan. “Makundi makubwa ya upinzani nchini Sudan Kusini, ikiwa ni…

Soma Zaidi >>

MWALIMU ALIYEMUUA MWANAFUNZI KWA KIPIGO MIKONONI MWA POLISI

Bukoba, KAGERA. Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia mwalimu wa shule ya msingi ya Kibeta iliyoko katika Manispaa ya Bukoba mkoani kagera, Respicius Patric, aliyempiga na kumuua kikatili mwanafunzi wa darasa la tano katika shule hiyo. Tukio hilo lilitokea Agosti 27, 2018, ambapo mwanafunzi Spelius Eradius (13) aliuawa na Mwalimu huyo kwa kipigo cha viboko, baada kutuhumiwa kuwa ameiba mkoba wa Mwalimu Elieth Gerald uliokuwa na vitu mbalimbali zikiwemo pesa Taslimu shilingi Elfu Sabini na Tano (75,000) na simu ya mkononi. Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, Kamishina Msaidizi…

Soma Zaidi >>

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AJITOLEA KUMSOMESHA MLEMAVU

  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde amejitolea kumsomesha na kumlea mtoto Christopher Edward kutokea kijiji cha Mtita, Wilaya ya Bahi jijini Dodoma ambaye amekatwa miguu yote miwili katika Hospital ya kibingwa ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma kufuatia kupatwa na ugonjwa wa kupooza miguu. Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo leo katika Hospital hiyo ya kibingwa wakati akikabidhi kiti cha matairi (wheelchair) kwa mtoto Christopher kilichotolewa na Hospital ya Benjamin Mkapa ikiwa ni njia ya kumrahisishia usafiri kumtoa sehemu moja kumpeleka sehemu nyingine katika…

Soma Zaidi >>

DC,MURO AFUNGUA MKUTANO WA WABOBEZI WA UTAFITI

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha,Jerry Muro amefungua mkutano wa wabobezi wa utafiti katika ukanda wa Africa Mashariki ” The Eastern Africa Research and Innovation Management Association, Tanzania Chapter, mapema hii leo. Mkuu huyo wa wilaya amemuwakilisha mkuu wa mkoa wa Arusha. Mrisho Gambo mkuu wa Wilaya amewapongeza Watafiti kwa Ubunifu wa kuwa na Jukwaa la Pamoja kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabiri wananchi wa jumuia ya Africa ya Mashariki. Pia amewaeleza juhudi mbali mbali ambazo zinafanywa na Serikali yaTanzania za kuwezesha taasisi za kitafiti na za Elimu ya juu…

Soma Zaidi >>

ALICHOSEMA CRISTIANO RONALDO BAADA YA KUSHINDA BAO BORA LA UEFA 2017/2018

Mshambuliaji nyota wa klabu ya Juventus Cristiano Ronaldo amefunguka na kuwashukuru mashabiki wake waliompigia kura na kuibuka mshindi wa bao bora la UEFA 2017/2018 ambapo kwa msimu uliopita alichukua Mario Mandžukić. Kupitia ukurasa wake wa twitter Cristiano Ronaldo ameandika >>>Shukrani kwa kila mtu aliyepigia kura. Hatutasahau kamwe wakati huo, hasa majibu ya mashabiki katika uwanja huo<<<. Ronaldo ametangazwa mshindi wa bao bora la mwaka 2017/2018 na Chama cha soka barani Ulaya (UEFA) baada ya bao lake safi maarufu kama (bicycle kick goal) alilofunga kwenye mchezo wa tarehe 03 mwezi Aprili mwaka…

Soma Zaidi >>

POCHETTINO, ZIDANE WANAONGOZA MBIO ZA KUMRITHI MOURINHO

Klabu ya Manchester  Utd imeendelea kufanya vibaya kwenye michezo ya hivi karibuni tetesi za Mourinho kuondoka klabuni hapo zimezidi kupata uzito katika vyombo vya habari licha ya Jose Mourinho mwenyewe kusema bado ana mahusiano mazuri na mabosi wa klabu hiyo na wala hafikiri kuondoka klabuni hapo kwa sasa labda ingekua klabu nyingine. Watu ambao wamekua wakipewa nafasi kubwa sana kumrithi Jose ni Pochettino, Zidane, Conte, Carrick na Wenger. MAURICIO POCHETTINO. Huyu ni kocha wa Tottenham kwa sasa ambae anapewa nafasi ya kwanza kabisa. Pochettino aliiongoza klabu yake usiku wa jana ilipoipa…

Soma Zaidi >>

UN WAISHTUMU BURMA KWA MAUAJI YA KIMBARI JAMII YA ROHINGYA

Newyork, MAREKANI. Jeshi la Burma lilitekeleza mauaji na ubakaji dhidi watu kutoka jamii ndogo ya Rohingya na kupanga mauaji ya halaiki kwa mujibu wa Tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa katika ripoti yake ya mwisho iliyotolewa jana Jumatatu. Tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa inaomba kiongozi mkuu wa ‘Tatmadaw’ (Jeshi) na Majenerali wengine watano kufunguliwa mashitaka haraka iwezekanavyo. “Serikali ya kiraia inayoongozwa na Aung San Suu Kyi imeruhusu hotuba ya chuki kuendelea kusambaa, imeharibu nyaraka na haikuonyesha wajibu wake wa kulinda jamii ya watu wachache dhidi ya uhalifu,…

Soma Zaidi >>

KANGI LUGOLA ‘NINJA’ KUWASWEKA RUMANDE ASKARI NCHI NZIMA

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Kangi Lugula almaarufu ‘Ninja’, amewahakikishia kiama askari wa jeshi la polisi ambao wamekuwa wakilichafua jeshi hilo kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo kuwabambikizia kesi wananchi wasio na hatia. Amesema hayo leo Agosti 28, wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya ziara yake anayotegemea kuifanya nchi nzima ili kujiridhisha na utendaji kazi na ufanisi ndani ya jeshi hilo na jinsi linavyohudumia wananchi katika misingi ya haki na sheria ambapo amewataka askari wanaolichafua jeshi hilo waache mara moja. “Nimeanza kutembelea…

Soma Zaidi >>

MAREKANI NA WASHIRIKA WAKE KUKUTANA KUTATUA SUALA LA KATIBA MPYA YA SYRIA

Dameski,SYRIA. Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, Staffan de Mistura, ametoa wito kwa Marekani, Ufaransa na nchi nyingine tano kushiriki mazungumzo mjini Geneva tarehe 14 Septemba. Mwaliko huo unakuja siku mbili baada ya De Mistura kukutana na wajumbe wa Urusi, Uturuki na Iran , amesema msemaji wa Umoja wa Mataifa Jumanne wiki hii. “Hii itakuwa fursa ya kujadili njia za kendeleza mchakato wa amani,” amesema Alessandra Vellucci. Staffan de Mistura alitoa wito kwa Iran, Urusi na Uturuki kushiriki mazungumzo tarehe 11 na 12 Septemba mjini Geneva kuhusu suala…

Soma Zaidi >>

UFARANSA WAZIRI WA MASUALA YA MAZINGIRA AJIUZULU

Paris, UFARANSA. Nchini Ufaransa Waziri mwenye dhamana ya Ikolojia na Mshikamano, Nicolas Hulot, ametangaza nia yake ya kujiuzulu kwenye nafasi yake, mwaka mmoja baada ya uteuzi wake. Hulot amesema kwenye radio France Inter kuwa amekua akijihisi peke yake katika shughuli zinazohusiana na masuala ya mazingira. “Nimechukua uamuzi wa kujiuzulu, ni uamuzi mzuri wa uaminifu,” Nicolas Hulot ametangaza kwenye radio France Inter Jumanne hii Agosti 28, 2018. Mtayarishaji huyo wa zamani wa makala kwenye televisheni amesema kuwa amechukua hatua hiyo bila hata hivyo kumshauri Rais Macron na Waziri Mkuu Philippe kwa…

Soma Zaidi >>