CHADEMA YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MONDULI, KOROGWE NA UKONGA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Kikao Maalum cha Kamati Kuu iliyokaa kwa siku mbili, Agosti 15-16, mwaka huu, jijini Dar es Salaam baada ya kupokea na kujadili kwa kina taarifa kuhusu chaguzi za marudio za ubunge na udiwani na hali ya kisiasa nchini; Chama hicho, kimefikia maazimio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya uteuzi wa wagombea ubunge katika majimbo ya Monduli, Korogwe na Ukonga, kupitia Chama hicho, kwenye uchaguzi wa marudio ambao kampeni zake zitaanza rasmi Agosti 24- hadi Septemba 15 na siku ya kupiga kura Jumapili Septemba…

Soma Zaidi >>

MAKONDA AFURAHISHWA NA MKAKATI WA TCRA KUWEKA MFUMO WA ANWANI ZA MAKAZI NA POSTIKODI DAR ES SALAAM.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda leo amefungua semina ya kimkakati inayolenga kulifanya jiji la Dar es salaam kuwa katika mpangilio wa kisasa na kuhakikisha mitaa yote inawekwa katika mfumo wa anwani za makazi na Postikodi Kama ilivyo kwa majiji makubwa ulimwenguni. Makonda amesema Mfumo huo ni ukombozi mkubwa kwa wananchi kwakuwa utarahisisha huduma kwa wananchi ikiwemo kuwezesha kila mwananchi kuwa na anwani, kuwasaidia wageni kujua maeneo,kudhibiti wezi na matapeli, ulinzi na usalama, kusaidia kampeni ya usafi pamoja na kusaidia Jeshi la zimamoto na uokoaji kufika…

Soma Zaidi >>

RAIS MAGUFULI, JAFO NA LUKUVI WAPONGEZWA NA THRDC.

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umempongeza Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jafo kwa kuwaonya wakuu wa wilaya na mikoa kutojichukulia sheria mkononi kwa kuwakamata na kuwaweka watu ndani. Akizungumza na waandishi wa habari Mratibu, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Onesmo Olengurumwa amesema hatua ya waziri Jafo pamoja na Katibu mkuu wa wizara hiyo Mhandisi Musa Iyembo kuonya wakuu wapya wa wilaya na wakurugenzi kutojichukulia sheria mkononi kwa kuwaweka ndani baadhi…

Soma Zaidi >>

LIPUMBA AMUOMBA SEIF WAUNGANE

Ugunja, ZANZIBAR. Ikiwa ni siku chache tu zimepita toka kujiuzulu kwa mmoja wa viongozi wakuu Chama cha Wananchi (CUF),  ndugu Julius Mtatiro, Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, ameibuka na kuomba mapatano kati yake na Katibu Mkuu wake Malim Seif Sharif Hamad. Prof. Lipumba ameyasema hayo katika mkutano wa ndani wa chama hicho uliowashirikisha baadhi ya viongozi toka upande wa Unguja ambapo amesema anaomba kumaliza tofauti zake na katibu mkuu Seif kwa ajili ya kujiandaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020. Lipumba amesema anatamani wanaposhiriki uchaguzi huo kuwepo na maelewano…

Soma Zaidi >>

AJIUZULU UDIWANI (CHADEMA) NA KUJIUNGA CCM, KAKONKO – KIGOMA

Diwani wa kata ya Katanga wilayani Kakonko mkoani Kigoma, Osca Kazihise Bulakuvye, amejivua uanachama wake wa CHADEMA na hivyo kujihudhuru nafasi yake ya udiwani ndani ya kata hiyo. Bulakuvye amechukua maamuzi hayo hii leo ambapo tayari amemwandikia barua Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Kakonko kumtaarifu juu ya uamuzi wake huo. Katika barua yake, Bulakuvye ametaja sababu kuu ya kujiuzulu udiwani na kujiunga CCM kuwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania. Aidha, Bulakuvye amesema kuwa kilichomkimbiza kwenye chamachake cha zamani (CHADEMA) kuwa ni migogoro…

Soma Zaidi >>

MAGUFULI AENDELEA KUMMALIZA MBOWE, HAI DIWANI MMOJA ANG’OKA

Diwani wa kata Romu iliyopo Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, Shilyimiaufoo mejiuzulu nafasi yake ya udiwani pamoja na kujivua uanachama wake wa Chadema na kujiunga chama cha Mapinduzi (CCM ). Kimaro amechukua maamuzi hayo hii leo ambapo tayari amemwandikia barua Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Hai kumtaarifu juu ya uamuzi wake huo. Katika barua yake, Kimaro ametaja sababu kuu ya kujiuzulu udiwani na kujiunga CCM kuwa ni kukosekana kwa demokrasia ndani ya CHADEMA ambayo inaweza kuisaidia jamii katika kutatua matatizo na kuleta maendeleo na mabadiliko ya kweli kwa wananchi wa…

Soma Zaidi >>

PAPA FRANCIS ALAAN VITENDO VYA UDHALILISHAJI DHIDI YA WATOTO

Vatican imesema kuwa inataka kusikiliza kwa kina hoja za wahanga zaidi ya 300 walioathirika na vitendo vya ukatili ili kujua nini kilichotokea dhidi yao kutoka kwa makaasisi wa kanisa hilo katika jimbo la Pennsylvania nchini Marekani na kuliita tukio hilo kuwa ni la kinyama. Hatua hii imekuja mara baada ya waendesha mashtaka nchini Marekani kubaini kuwa zaidi ya watoto 1,000 huko jimbo la Pennsylvania walifanyiwa ukatili huo. Askofu wa Kanisa Katolik nchini Marekani ameagiza kufanyika uchunguzi ambao utaongozwa na Vatican, Kadnal Daniel DiNardo ambaye ni Rais wa kundi la maaskofu…

Soma Zaidi >>

UN YATAKA KUACHIWA HURU MWANAHARAKATI NABEEL RAJAB

Bodi ya umoja wa mataifa UN,imetaka kuachiliwa huru kwa mwanaharakati wa haki za binadamu wa Bahraini Nabeel Rajab aliyefungwa kwa madai ya kufanya makosa ya kueneza habari za uongo na kukashifu mamlaka za kiserikali. UN inasema kuwa hukumu ya Nabeel Rajab ilifanyika kinyume cha sheria na ilikiuka uhuru wake binafsi wa kujieleza, ambapo hadi sasa Nabeel amekwisha tumia miaka mingi tu gerezani tangu alipokuwa akiongoza harakati zake za kidemokrasia mwaka 2011.Lakini serikali kwa upande wake inasema kuwa mashitaka ya Rajab yalitolewa katika mfumo wa uhuru na uwazi. Nabeel Rajab, mkuu…

Soma Zaidi >>