CHADEMA Z’BAR WATEMBELEWA NA UBALOZI WA MAREKANI NCHINI

ZANZIBAR. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, kimepata heshima ya kutembelewa na Balozi Mdogo kutoka Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, na kufanya mazungumzo katika masuala mbalimbali ikiwemo hali ya kisiasa na uchumi ilivyo bara na visiwani Zanzibar. Katika taarifa iliyotolewa leo Agosti 10 na Idara ya Habari na Uenezi CHADEMA, Ofisi ya Makao Makuu Zanzibar, imesema kuwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Taifa (BAZECHA), Mheshimiwa Hashimu Juma Issa, kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, pamoja na watendaji wa makao makuu wamepata ugeni huo. Mhe. Issa, amepata nafasi…

Soma Zaidi >>

UVCCM RUFIJI WASHIRIKI KAZI ZA KIJAMII, WATOA MSAADA WA VITU MBALIMBALI

Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (Uvccm) Wilaya Rufiji, chini ya Mwenyekiti wake Hodari Comred Juma Kwangaya Leo tarehe 10/08/2018 wamejitolea kushiriki kazi za kijamii na kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika kuelekea maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani Amesema kuwa, wameamua kujitolea kufanya Usafi pamoja na kuchangia damu katika Hospitali ya Wilaya Rufiji pamoja na kufanya Usafi Uvccm waliweza kutoa sabuni kwa wagonjwa na wauguzi wote waliopo zamu katika hospitali hiyo. Aidha amesema kwa kushirikiana na Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Mohammed Mchengerwa waliweza kufika katika shule ya…

Soma Zaidi >>

MAVUNDE AWATAKA WAHANDISI KUTUMIA MIFUKO YA UWEZESHWAJI WANANCHI KIUCHUMI KUKUZA MITAJI YAO

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde amewataka Vijana wanaosomea mafunzo ya Uhandisi kuunda makampuni na kutumia mifuko ya Uwezeshwaji wananchi kiuchumi ili kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa Uchumi wa Viwanda. Mavunde ameyasema hayo leo katika Viwanja vya Posta,Kijitonyama kwenye Kongamano la Wanafunzi wa Vyuo vikuu na vyuo vya Elimu ya Juu wanaosomea fani ya Uhandisi ikiwa ni maadhimisho ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Bodi ya Wahandisi nchini Tanzania. Mavunde pia amewahikikishia wasomi hao kwamba Serikali itasimamia mpango wa mafunzo kwa vitendo…

Soma Zaidi >>

FURSA YA AJIRA KWA WALIMU WA MASOMO YA SANAA – THE SCHOOL OF ST. JUDE ARUSHA

Location Other Arusha District Arusha Description REF: TSOSJ/HR/ACDM/SC/02/18 Subject: History & General Studies Duty Station: Usa River – Arusha, Tanzania The School of St Jude is a 100% charity-funded education institution that provides free, high-quality primary and secondary scholarships to 1,800 of the poorest and brightest students in the Tanzanian region of Arusha. To provide a high level of education to the school’s children and help those to learn new ideas and concepts to ensure the students meet the required standards of the Tanzanian education system. Key Responsibilities: Teach one…

Soma Zaidi >>

NAFASI 41 ZA AJIRA – AIR TANZANIA COMPANY LIMITED (ATCL), SIFA NI KUANZIA KIDATO CHA NNE

Air Tanzania Company Limited (ATCL) is in the process of revamping its operations and has introduced new equipment to its fleet. The Company is therefore inviting applications from qualified Tanzanians to all the following position. POSITION: CABIN CREW ( 41 POSTS) Qualifications Minimum Holder of “O” Level with Four passes , ONE of them should be English AB Initial Certificate from Recognized Aviation Institution Holder of a Cabin Crew Certificate from Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA) Fluent in both written and spoken English and Swahili. Knowledge of Extra International Language…

Soma Zaidi >>

WALIOHUSIKA NA SHAMBULIO LA MBISE KUCHUKULIWA HATUA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linalaani vikali tukio linalosambaa mtandaoni la kupigwa kwa mwandiishi wa habari wa Wapo Redio Sillas Mbise lililotokea Tarehe 08.08.2018 siku ya mechi kati ya Simba vs Asante Kotoko ya nchini Ghana, ikiwa ni maadhimisho ya Simba day. Aidha Polisi kanda maalum imeanza uchunguzi wa tukio hilo kwa kufungua jalada la uchunguzi wa picha ya video hiyo inayosambaa inayoonesha askari wa Polisi na mwandishi huyo wa habari ili kubaini ukweli. Sambamba na hayo Polisi jukumu lake kuu ni kulinda usalama wa raia na…

Soma Zaidi >>

MFUMUKO WA BEI WAPUNGUA HADI KUFIKIA ASILIMIA 3.3

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Julai, 2018 umepungua hadi kufikia asilimia 3.3 ikilinganishwa na asilimia 3.4 mwezi Juni, 2018. Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa sensa na Takwimu za Jamii, Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ephraim Kwesigabo amesema mfumuko wa bei kwa mwezi Julai mwaka huu, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2018 imepungua ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2018. Amesema kuwa, kupungua kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Julai,…

Soma Zaidi >>

AGIZO LA NAIBU WAZIRI MADINI LAWATIA KITANZINI WACHIMBAJI WADOGO NYARUGUSU

Jeshi la Polisi mkoani Geita linawashikilia wachimbaji wadogo watatu kutoka mgodi wa dhahabu uliopo katika kijiji cha Nyarugusu wilayani Geita kufuatia kukaidi agizo la Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, linalowataka kusitisha shughuli za uchimbaji katika eneo hilo. Majina ya wachimbaji hao ni pamoja na Abdul Ramadhan ambaye pia ni Mmiliki wa Leseni, Hezron Enock na Mai Kibanda ambao ni wabia wa mgodi huo. Wachimbaji hao wamekamatwa hii leo kufuatia agizo la Waziri Nyongo alilolitoa baada ya kufanya ziara kwenye mgodi huo ambapo amepokea malalamiko ya wananchi waliokaribu na mgodi…

Soma Zaidi >>

WAZIRI KAIRUKI AZITAKA KAMPUNI ZA MADINI KUTAFUTA SULUHU AMA KUKUBALI KUFUNGIWA

Waziri wa Madini Angellah Kairuki amezitaka kampuni za Mundarara na Sendeu Mining zinazofanya shughuli za uchimbaji wa Madini ya Ruby kukaa pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro wao na endapo itashindikana basi Serikali itachukua hatua za kuufungia mgodi huo. Agizo hilo amelitoa mapema leo alipotembela katika kijiji cha Mundarara Wilaya ya longido Mkoani Arusha kufuatia mgororo uliopo katika eneo hilo kutokana na muingiliano wa chini ya ardhi baina ya kampuni mbili za Mundarara na Sendeu Mining, zinazofanya shughuli za uchimbaji katika eneo hilo, hali iliyosababisha mzozo mkubwa baina ya kampuni hizo.…

Soma Zaidi >>

RAIS DKT MAGUFULI AISHUKURU SERIKALI YA UINGEREZA, WIZARA YA AFYA YASHUKIWA NA NEEMA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Magufuli ameishukuru Serikali ya Uingereza kwa kutoa misaada mbalimbali ikiwemo shillingi billioni 307.5 kwa lengo la kuunga mkono jitihada zake za kupambana na rushwa. Rais Dkt, Magufuli Leo ametembelewa na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza Penny Mordaunt ambapo aliongozana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Sarah Cooke pamoja na Mkuu wa ofisi ya DIFD nchini Beth Arthy. Amesema kuwa fedha hizo zimelenga kusaidia mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kuboresha Sekta ya Elimu pamoja na Sekta ya Afya ambapo kati…

Soma Zaidi >>